Kaka Michuzi,
Kuna mizani mpya na ya kisasa ya kupima uzito wa magari ukiwa unatokea chalinze kwenye Msata. Sikumbuki vizuri lakini nadhani ilifunguliwa mwaka jana na imefanya eneo lile kuvutia sana. Hivi majuzi nilisimama pale na nilishangazwa nilipoingia kwenye kile choo kilichoko pale ambacho nacho ni kipya na hakijatumia zaidi ya mwaka mmoja.
Kwenye picha nilizoambatanisha utaona kwa nje jengo la choo kile linaonekana zuri na jipya. Ila ukiingia ndani utashangaa kuona aina ya ujenzi na upigaji wa rangi ulivyofanyika. Tayari kimeoza na kinatia kinyaa utadhani kina miaka kumi au zaidi tangu kijengwe. Pamoja na uchafu wa hali ya juu, mambo ya maji yameharibika, rangi imebabuka na mfumo wa vyoo haufai kabisa
Je, haya nayo sio matumizi mabaya ya fedha za umma katika ujenzi wa miundombinu? Tanroad na wizara ya ujenzi hawajaona hili?
Bandika kwenye blog yako labda wahusika wataona na kuchukua hatu maana inatia aibu...na ujumbe umfikie Mzee Magufuli.
Ninaomba usibandike jina langu kwenye blog...yatosha kusema imetumwa na Mtanzania
Mungu akubariki
JAMANI JAMANI,HIKI CHOO NI KICHAFU MNO KWA AFIYA YA BINADAMU,NAHISI HATA NGURUWE HAWEZI KUJISAIDIA HAPA.
ReplyDeleteMdau umefenya jambo la maana sana kufichua uozo kama huu.
ReplyDeleteJapo huhitaji kuuliza kama ni ufisadi au lah. Ufisadi ulishakuwa ni utamaduni wa watz wengi (sio wote). Na huo ni muendeezo wa utamaduni huu. Mizani inaingiza pesa nyingi sana lakini wanashindwa kukarabati choo. AIBU KWAO!
wow
ReplyDeleteWatanzania tuache utani misala yetu ni aibu tupu. MSALANI NI MAHALI PA KUPUMZIKA KWA HIYO PANATAKIWA PAWE SAFI. PAMOJA NA UDUNI WA UJENZI WATUMIAJI WAWE WASTAARABU NA MALAKA IWEKE UTARATIBU WA USAFI. ANGALIA TU UKUNGU ULIVYOTANDA KUTOKANA NA SEHEMU HUSIKA KUTOFANYIWA USAFI!!!!!!!!
ReplyDeleteMdau, yaani ningelikuwa wewe nisingeficha jina ,majina yangu yote na ya marehemu babu ningeliyaweka tena kwa herufi kubwa kubwa , yaani duh !!!! jambo la maana kama hili bado unaogopa nini ???? kwanza Magufuri lazima angekupa mkono wa Idd na soda ya kopo juu. Huu ni sawa na ufisadi , kwani wagonjwa siyo mawaziri tu wako pia wa chini yao kama hivi,wameoza harufu ya kutupa. Waliojenga hapo warudie kisha pawe na mtu au kampuni ya kufanya usafi au mama mmoja au wawili apewe ajira ya usafi kila siku-laki 3 kwa mwezi huyo mama hapo kijijini atakuwa kaulamba. Kingine , jamani hivi vyoo vya kuchuchumaa ,vipigwe marufuku, utakunya vipi umechuchumaa ???? hii kuchuchumaa ni wakati uko darasa la kwanza hadi la 7. umri ukienda magoti yanaanza kuuma ,yaani huwezi kuchuchumaa. Naomba kuuliza je ?? jengo la Bunge lina vyoo vya kuchuchumaa ???. mahoteli yote makubwa sijaona vyoo hivi, kwenye ndege nako hata ile ya abiria 300 hadi 400 hakuna vyoo vya kuchuchumaa na hakuna dada wala kaka wa kufanya usafi ndani ya ndege masaa 12 angani na kila mmoja anakwenda kukaa kwenye choo hicho hicho alichokaa mwenzake ,sisikii kuugua mapele wala makurutu-jamani tubadilike. Jina langu ni Zebedayo msema kweli kutoka Mwanza Tanzania.
ReplyDeleteTwamshukuru sana mdau kwa taarifa hizi muhimu. Naamini Mchapakazi wetu Mhe. MAGUFULI akiiona hii habari atawawajibisha wahusika. Kwa kweli inatia aibu sana jinsi ambavyo baadhi ya watumishi wa Serikali wanavyofanya ufisadi kama huu bila hata aibu. Ankal, kama unayo email ya Mzee Magufuli, tafadhali mtumie yeye moja kwa moja then awashe moto kwa wahusika kama kawaida yake.... Tunahitaji wazalendo kama huyu mdau wetu wa kufichua maovu kama haya....
ReplyDeleteTusilaumu tanroad watu wengi hawajui kutumia vyoo vizuri inabidi wafundishwe,tumeona unaweza kumkodisha mtu nyumba ina choo kizuri cha kisasa lakini baada ya miedhi michache ukienda kukikagua utakuta kimeharibika na ni kichafu.Inabidi watanzania pia wafundishwe namna ya kutumia vyoo.
ReplyDeleteDUH KWA KWELI HII NI AIBU SANA MIE NILIPITA WIKI HII NIKAFURAHI KUONA SASA TATIZO LA KUCHIMBA DAWA LIMEIISHA MARA NIKAONA WATU HAWAINGII WANAENDA KICHAKANI NDIO NAJUA SABABU KUWA HAKUFAI. WATZ TUBADILIKE JAMANI TUWE WADILIFU
ReplyDeleteZebedayo,hongera sana .Yaani hata mimi yananikuta haya ya kuchuchumaa,haina raha kabisa , yaani unajuta kwa nini umebanwa choo. Na mabwana afya wetu pia nasikia eti huwalazimisha wenye migahawa kuweka vyoo vya kuchuchumaa, hawa watakuwa ni mabwana afya kweli au ni chai maharage.
ReplyDeleteHaya ni mambo ya kusikitisha sana,mwaka 2012 tuko katika hali ya namna hii kweli inatisha.Niliwahi kuwaambia watu kwamba choo na jiko ni sehemu zinazotakiwa ziwe safi kuliko sehemu yoyote majumbani kwetu au mazingira yoyoyte ambayo mtu anaishi/kufanya kazi au biashara wakanicheka sana,nilikuwa natafuta nyumba zote zilikuwa nzuri lakini kuingia sehemu hizo mbili nilishindwa!!nikawaeleza madalali 'nyumba ni choo'nilionekana kama nimetoka outer space.Unakuta sebuleni kumepambwa kwa lulu na almasi,lakini loo omba Mungu usipatwe na haja ukaingia msalani UNAKUFWAAA!!!huko jikoni ndo ukiingia ukaletewa chakula utaaga dakika hiyohiyo,iwe ni nyumbani au sehemu yoyote ya biashara.Tunahitaji mafunzo ya kutumia vyoo,na kutunza vizuri majiko yetu.Niliwahi kuwaambia watu kuwa nikitaka utulivu naingia chooni nakaa tu na kusoma bila kusumbuliwa na kikombe changu cha chai au juice yangu walinishangaa.Kwa nini chooni kuwe kuchafu na harufu mbaya kama kunajaliwa kama sebuleni??
ReplyDelete