Mwenyekiti wa Kamati ya Ukusanyaji wa Maoni ya Katiba mpya Mohamed Yussuf Mshamba akitoa Ufafanuzi wa namna ya Utoaji wa maoni unavyotakiwa huko katika kijiji cha Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni siku ya Pili tokea kuanza kwa mchakato huo huko Zanzibar kushoto yake ni Mjumbe wa Kamati Salim Ahmed Salim na kulia yake ni Mjumbe wa kamati Richard Lyimo.
Mjumbe wa Kamati ya Ukusanyaji wa Maoni ya Katiba mpya Richard Lyimo akifahamisha namna ya mchakato mzima wa kukusanya na kutoa maoni kwa wananchi unavyotakiwa huko katika Kijiji cha Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja kushoto yake ni Mwenyekiti wa Kamati hio Mohd Yussuf Mshamba.
Mwananchi wa Kijiji cha Kibuteni Pandu Haji Yakubu akitoa maoni yake mbele ya kamati ya ukusanyaji maoni huko katika kijiji hicho Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwananchi wa Kijiji cha Kibuteni Pandu Haji Yakubu akipeleka maoni yake kwa njia ya Barua mbele ya kamati ya ukusanyaji maoni huko katika kijiji hicho Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwananchi wa Kijiji cha Kibuteni Shemsa Hassan Ame akitoa maoni yake mbele ya kamati ya ukusanyaji maoni huko katika kijiji hicho Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwananchi wa Kijiji cha Kibuteni Riziki Wakili Haji akipeleka maoni yake kwa njia ya Barua mbele ya kamati ya ukusanyaji maoni huko katika kijiji hicho Mkoa wa Kusini Unguja.
Wajumbe wa Ukusanyaji Maoni ya Katiba Mpya wakiwa katika Kazi ya kuandika maoni ya Wananchi mbalimbali waliokuwa wakitoa maoni yao huko katika kijiji cha Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...