Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Watoto Ummy Mwalimu akicheza ‘kwaito” na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kibaigwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa mabweni 30 nchi nzima kwa mtoto wa kike.
Waziri kivuli wa Elimu na mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Susan Lyimo akiongea katika hafla ya uchangiaji wa mabweni. Katika hafla hiyo jumla ya shilingi 37,214,000/= zilipatikana ikiwa ni ahadi pamoja na fedha taslim.
Mgeni Rasmi, Waziri kivuli wa Elimu na mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Susan Lyimo akipokea mkasi kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya TEA Dkt Naomi Katunzi kwa ajili ya kuzindua rasmi harambee ya ujenzi wa mabweni 30 kwa ajili ya watoto wa kike wa sekondari nchini.
Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Kibaigwa Mhe. Job Ndugai Akivuta utepe uliokatwa na mgeni rasmi Mh. Suzan Lyimo huku tukio hilo likishangiliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na TEA.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa mchango wake na akihimiza watu wengine wachangie katika ujenzi huo. Ili mradi huo ukamilike jumla ya shilingi za kitanzania shilingi bilioni 2.3 zinahitajika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2012

    Haya ndio maendeleo tunayopenda kuyaona,katika shughuli za kijamii itikadi za kisiasa zinawekwa pembeni, kama hivyo waziri kivuli wa upinzani kahudhuria kwenye shughuli za maendeleo, hii safi kabisa na haya ni matokeo ya sera nzuri za serikali ya CCM sidhani kama ingekuwa ndio kina mwagadamu wameshika mpini wangeyakubali haya.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2012

    Fundisho zuri. Hii inaonesha kuwa Watanzania tukiungana bila kujali tofauti ya vyama vya siasa tunaweza kufanya makubwa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2012

    Mgeni rasmi ni Mh Ummy au Mh. Suzan maana maelezo hayaendani na picha halisi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...