Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga (Wabunge) wakati wa TAMASHA LA MATUMAINI ambapo wabunge wapenzi wa timu ya Simba wameibuka kidedea kwa penalti 3-2. Simba wamefunga penalti 3 wakati Yanga wakifunga 2.
(PICHA ZOTE NA GPL)
Wana yanga mmeona kiwingu kimeanza kutanda?jina linazidi kuchafuka sasa subirini mkutane na mnyama wa ukweli namaanisha wekundu kamili kwenye ligi au mashindano ya kagame cup naona safari hii huyo kocha anyoe upara na ajiandae kwenda kifanya biashara mitaa ya kariakoo Na kipigo kijacho hata cha mbwa mwizi kinanafuu mtatimua hadi wanachama
ReplyDeleteInafurahisha na kupendeza kwa waheshimiwa wabunge kujichanganya, hii ndio Tanzania tunayoitaka yenye amani na utulivu, kuna nchi nyingine muda wa kucheza ndombolo haupo,mtu anawaza wapi akimbiziye uhai wake hata familia yake haijui ilipo. Huu ni mwanzo mwema, matumaini yanapatikana,waheshimiwa mkirudi kule nyuma enzi za baba yetu wa Taifa, waheshimiwa wote walikuwa saizi moja,walipendwa na kila mtu. Utamaduni wa kujibagua kwa vyeo ni sumu usipewe nafasi, michezo haijui cheo wala fukara wote tushirikiane kuliongoza taifa. Yanga juu, mbele daima, simba ivunjwe ichanganywe na yanga tupate Timu kubwa na nzuri itatufikisha mbali.
ReplyDeletemdau,