Taswira za kunguru wenye baka jeupe kifuani katika mji wa Chalinze mkoa wa Pwani leo. Siku hizi kunguru wa aina hii wamepotea sana hususan mijini na badala yake kunguru weusi wametawala kila kona na kuleta kila aina ya kero, ikiwa ni pamoja na kukwapua kila aina ya vitu. Mwenye data zaidi tunaomba msaada tutani
Home
Unlabelled
wako wapi kunguru wa aina hii?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ao kunguru hapa Songea wapo kibao. Hawana fujo kama wale wause mwili mzima.
ReplyDeleteWameathiriwa na muungano
ReplyDeleteNgege anayejua kutumia ubongo wake!
ReplyDeleteHata hapa katika eneo la Kwembe Maduka Matatu wapo bali wale washenzi nao wameishafika hivyo nivurugu tupu. Hawa wenye baka jeupe wamebaki kama saba hivi
ReplyDeleteObserver
Kunguru hafugiki!.Hawa wenye baka jeupe,Daresalaam wamekuwa adimu.Watu wa fani hii watatusaidia
ReplyDeleteDavid V
Hao kunguru wenye 'vizibao' vyeupe, baadhi unaweza kuwaona sehemu za Dodoma. Ila wale weusi afiriti, wamejazana tele Zanzibar, enzi hizo ilifikia wakati wakawa wanafanyiwa 'usasi' kwa kero na bughudha zao, wanaweza kukukwapulia mpaka 'baraghashia' yako kichwani, hawana woga wala kusikia.
ReplyDeleteUnawatafuta umetumwa na mganga?! Nitakuletea tenga zima kwa basi ukiwahitaji!
ReplyDeleteHuyu kunguru wa Bara. Wale weusi tunaita kunguru wa Zanzibar. Kwa hiyo njoo bara utawaona kibao tu.
ReplyDeletePia wanapatikana kisiwani Pemba hususan maeneo ya mkoani. Kunguru hawa ni 'wapole sana' kulinganisha na wale weusi wasio na mabaka. Wale weusi hata 'kapelo' uliyovaa wanaipora na kutimka nayo!!, we acha tu
ReplyDeleteKunguru hawa waliathiriwa na uzuzu wetu wa kudandia mambo hovyo bila kufikiri. Kunguru weusi waliletwa ati kulisafisha jiji la Dar. Hivi mtu na akili zako timamu ukamtegemee ndege kukusafishia mji? Sisi kila tunaloambiwa na mzungu tunakubali tu. Kunguru hawa walikuwa nanaleta mandhari nzuri jijini kwa rangi zao. Hata milio yao ilikuwa maarufu kabisa. Hivi sasa jijini wamejaa kunguru hanithi wale wa kiZanzibari ukishika kitumbua anakupora, bah! Ingekua uwezo ninao ningaliwaulia mbali wote,nirudishe kunguru wetu wa kijambakoti.
ReplyDeleteSehemu yenye kunguru hawa wenye baka jeupe wakiingia wale weusi kamili, wenye baka huisha kwa sbb hawa weusi hula mayai ya ndege wa aina zote na hivyo huenda kwenye viota vya hao wenye baka na kula mayai yao. MBAYA SANA.
ReplyDeleteSio kapelo tu mdau wa hapo juu, sifa moja kubwa ya kunguru hawa weusi ni wapenzi sana wa chupi za akina dada zinapoanikwa. Inasemekana kinachowavutia ni ile harufu inayovutia ya kinachositiriwa ndani ya chupi hizorespoap, heheheheh!!!!
ReplyDeleteWenye baka jeupe ka huyo wapo Iringa wengi sana kama ilivyo dar kwa wale weusi kabisa, ila hawa wanabusara sana tena husaidia kuondoa sana sana ule uchafu ulooza, mfano mnyama kama paka, mbwa, na ndege wakifa wao hunyofoa kidogo kidogo nyama yao mpaka waisha inabaki mifupa tu
ReplyDeleteWewe mdau wa 9:58 kasome historia vizuri. Kunguru hao walikuwa introduced Zanzibar (na siyo bara) kwa kazi ya kusafisha mizoga. Hiyo ni karne ya 19 walipoletwa Zenji kwa kazi hiyo.
ReplyDeleteNani aliwaleta huku Bara? Nadhani wanao uwezo wa kusafiri na kwenye miaka ya sabini ndiyo wameanza kuonekana.
pemba wako wa kumwaga kama mganga wako anahitaji niambie nije nao kwa mtubwi.
ReplyDelete