Baadhi ya Wanzania 38 waliokuwa wakimbizi Jijini Mogadishu wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kushuka katika ndege la Umoja wa Mataifa iliyowaleta nyumbani wakiwa na wake zao waliooa nchini Somalia baada ya kuishi huko kwa miaka 11,walikimbia vurugu za Januari 26/27 mwaka 2001.
Baadhi ya Watanzania waliokimbilia jijini Mogadishu nchini Somalia mwaka 2001 wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Zanzibar. Wa kwanza ni Mohammed Adam (38) akiwa amembeba mwanae mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume,wanaotazama kamera ni baadhi ya wake wa Watanzania hao ambao ni raia wa Somalia waliowasili wakitokea Mogadishu Somalia na ndege ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia huduma za kibinadamu.
Watanzania waliokuwa wakimbizi katika kambi ya Mogadishu wakielekea kupanda mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,Zanzibar.(Picha na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar).
pamba walizopiga baab kubwa. halafu kila mmoja kaja na mwanamke wa kisomali.
ReplyDeleteKARIBUNI NYUMBANI
ReplyDeleteKumbe Somali mambo mazuri bwana!!
ReplyDeletesomalia kama sio vita basi tanzania ingekuwa ipo chini ya somalia kwa umasikini, tanzania ni number 4 duniani kwa umasikini but kama hizo nchi tatu zitakuwa hazina migogoro ya kupigana na vita basi tanzania itakuwa number 1 duniani kwa umasikini
ReplyDeleteHawa watu ndio wanaotupakazia sana katika Jumuia za Kimataifa.
ReplyDeleteTokea lini Tanzania tukawa na Wakimbizi?
Angalia sasa wametahayari, wanarudi nchini wamezusha mambo kuwa kuna hali hatarishi nchini wakakimbia, UN imefanyia kazi taarifa ikaona hakuna ukweli wa madai yao sasa imewaingiza kwenye ndege imewarudisha!
Serilaki ipo tulivu inawakaribisha kwa mikono miwili!
Tena hawa jamaa ikiwezekana wapewe mikopo ya Saccos ili wapate kazi za kufanya waache uchochezi wa kutuchafua Tanzania Kimataifa!
Ukimbizi gani nyie Watanzania, semeni mmekimbia kwa njaa iliyotokana na uvivu wenu binafsi tu!
ReplyDeleteMbona wenzenu waliopo Tanzania Bara wanafanya shughuli zao na hawana ubwege kama wenu mliofanya?