Kaimu mgaga mkuu wa serikali Dkt. Donan Mmbando (kushoto) akizungumza na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland mara baada ya ujumbe huo kuwasili makao makuu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu mgaga mkuu wa serikali Dkt. Donan Mmbando (aliesimama mbele) akizungumza na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland.
Kamishina wa Idara ya Ustawi wa Jamii wa Wizara ya Afya Bw. Danford Makala (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu Ustawi wa jamii wakati wa mkutano kati ya Ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland na watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii leo jijini Dar es salaam.
Meneja Mkuu na mmiliki wa Hospitali zinazojengwa kwa kutumia makontena (Hospitainer) na kuweza kupelekwa kutoa huduma za afya maeneo yoyote kutoka nchini Netherland Bw. Rolof Mulder akiongea na watendaji wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuelezea namna kampuni hiyo inavyofanya kazi zake.
Watendaji wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
Nanyie wazungu mnaojichanganya na hao wabongo, kwanini msiwaseme au kuwashauri kwa namna moja ama nyingine kuhusu mambo ya rushwa na hali mbaya ya maisha ya watanzania wanaoishi?? Wengi tunateseka kutokana na utaratibu mbaya wa hao unaowaona nakupiga nao picha. Wao wanajiita macelebrate.... mngekua nangalau mnafanyia vikao huku kwetu tandale au manzese mngewaona hovyo sana.
ReplyDeleteWizara ya Afya msikubali containers hat siku moja sisi hatuhitaji hizo. Tunahitaji vitu vya kudumu. Hizo containers zipelekwe nchi zenye maafa au vita. We dont need short term solution for long term problems. Hawa jamaa wanatafutia ndugu zao market tu.
ReplyDelete