Habari za Kazi Kaka Michuzi, 

leo najitokeza kwenye Jukwaa lako kutoa malalamiko yangu kuhusu ucheleweshaji wa makusudi wa maombi ya Hati za Kusafiria unaofanywa na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kigoma. 

Lililonipelekea kuandika hili ni kutokana na ndugu yangu mmoja anaeishi Mkoani hapo kupeleka maombi ya Kuomba Hati ya Kusafiria akiwa na Vielelezo vyote hitajika. Kwa utaratibu aliambiwa mchakato wa kuidhinisha huchukua siku 2 au 3 kutegemea na hali ya kazi, lakini cha kutia shaka ombi lake limekaa hapo kwa muda mrefu bila kupatiwa majibu yoyote. 

Bila kuambiwa kama limekubaliwa au lina matatizo hivyo halitaweza kukubaliwa. Ilichukua karibu wiki 4 kwa majibu ya Ombi hilo kutoka na yeye kuweza kuendelea na Taratibu zingine hitajika. Alipoulizia, aliarifiwa kuwa Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kigoma amekuwa na tabia ya kukaa na mafaili ya maombi ya watu wa Hati za Kusafiria bila kuyafanyia kazi na amekuwa akiwakemea wasaidizi wake kumkumbusha habari za mafaili yaliyo mezani kwake mpaka hapo atapoamua kuyaangalia mwenye. 

Ki ufupi, Idara hiyo anaiendesha kama Idara Binafsi, akifanya atakalo bila kuangalia mahitaji ya waombaji na sababu za wao kuomba hati hizo kwa wakati huo. 

Hali hii imekuwa ni kero kwa Waombaji wengi wa Hati hizo kwa Mkoa huo, na wamekuwa wakutumia kigezo cha kuwepo mpakani, kuchelewesha maombi kwa nadharia ya kufanya uchunguzi wa uraia wa muhusika, lakini hali halisi, huyo Muheshimiwa anakuwa ameyakalia hayo mafaili kwa sababu anazojua yeye. 

Nisingependa raia wengine wema wa kutoka mkoa huo wa Kigoma, wateswe na jambo kama hili alilopitia ndugu yangu kwa sababu tu ya Uzembe wa Kiutendaji wa Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kigoma. 

Naomba unifikishie kero hii, na naomba unihifadhi identity yangu kwani hawa watu wa Usalama wakati Mwingine huwa kama chama Kimoja kikubwa, kinachotutafuna chini kwa chini. 

Ntashukuru sana kama litawakilishwa kadiri utavyoona inafaa, na hata kama utalifanyia uchunguzi kwanza kabla ya kuliwakilisha itatusadia wote wana Kigoma na watanzania kwa Ujumla. Natanguliza Shukurani zangu za dhati. Ndimi katika Ujenzi wa Taifa.

Mdau wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2012

    SHUKURANI SANA KWA KUTHUBUTU KUTOA MALALAMIKO HAYA, WAPO WENGI WATU WA NAMNA HII KATIKA MAOFISI NA SEHEMU MUHIMU ZA KAZI HASA KWA WALE WENYE KOFIA YA KUIDHINISHA MASUALA YA WATUMISHI, YOTE HII NI ROHO MBAYA/WIVU/CHOYO PIA NI KUTEGA KAZI KWA MTINDO WA MGOMO BARIDI, MTU YUPO KAZINI LAKINI MWISHO WA SIKU UKIPIMA KAZI ALIZOFANYA KWA MASAA YOTE NI ROBO TU. MMEPEWA DHAMANA FANYENI KAZI WAJIBIKENI NDUGU ZETU, MNAKUWA KAMA HAMNA UTU/DINI MWOGOPENI MUNGU, VIONGOZI/WATENDAJI WAKUU JIREKEBISHENI HIZO NI DHAMBI/UONEVU KWA WAHITAJI. NINA MENGI LAKINI BASI KWA LEO INATOSHA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2012

    Hili ni tatizo sugu kwa siye wafanyakazi wengi wa serikali. Tunashindwa kujiwekea ratiba ya ofisini kwa kila kitu. Nafikiri wananchi kwa ujumla wanatakiwa waulizie taratibu na muda utakaochukua kwa jambo lake kushughulikiwa na pia ajue kama huo muda aliopangiwa umepita anatakiwa aende hatua gani? Mfano mmoja niliende kuwatembelea wafunga gereza fulani huko vijijini siku ya jumapili.Kwenye kibao chao wameandika muda wa kuona wafungwa ni saa nne asubuhi. Ikafika saa nne tumeenda sehemu inayostahiki hatujaweza kuwaona. Na uongozi husika hawakutupa taarifa yeyote.

    Siye wananchi tumesubiri hadi inakaribia saa tano nikaamua niende nikawaulize.Nilivyofika pale wakawa wakali.Wananiambia una haraka gani?Nikawaeleza kwamba kwenye kibao chenu mumeandika tutawaona wafungwa saa nne asubuhi na sasa hivi inakaribia saa tano na hamjatupa taarifa yeyote. Hata hawakunijibu chocho,wakaondoka. Wananchi tukawa tunasubiri.

    Mara askari magereza akaniita, akasema anataka nionane na mkubwa wao. Yule mkubwa wao akaniuliza tatizo langu nini?Nikamweleza kwamba mumetuandikia kwenye kibao kuwaona wafungwa saa nne asubuhi na sasa ni saa tano, na hamjatueleza kitu chochote kama kuna mabadiriko yeyote. Na siye wananchi tunakazi pia za kujenga taifa,muda wetu mwingi unapotea hapa.Akauliza wewe nani?Nikamweleza miye mwananchi.

    Akanieleza kuwa tatizo ni maji, mashine ya maji ilikuwa mbovu. Wafungwa walikuwa wanachota maji na sasa wanamaliza hafu mtawaona. Nikamweleza kuwa inabidi wananchi wapewe taarifa hii mapema ili aweze kujipanga na shughuli zake bila kupoteza muda. Yule mkuu akasema sawa na akasema tumekosea.

    Wakati natoka nje kulikuwa na askari mmoja akawa anazungumza anasema,wananchi siku hizi wanajifanya wanajua.Miye nikamwacha nikenda zangu kuwaona wafungwa na tukaondoka zetu.

    Kwa hiyo siye wananchi tujitahidi kuhoji kila kitu kulinga na sheria. Muumba akipenda nchi itaanza kuchakamka kila sekta/idara na maendeleo yakaanza kwenda vizuri.

    Pole huyo mdau aliyepata usumbufu wa maombi yake. Ni changamoto hapa kwetu Tanzania kwa siye tunaotoa huduma kwa wananchi wenzetu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 03, 2012

    Afisa wa Uhamiaji wa Mkoa anachokifanya ki ukweli SIO KIBAYA na PIA SIO KIZURI.

    Kwa sababu,

    Kama ulivyogusia hapo ni mpakani hivyo wababaishaji ni wengi, kuna Warundi, Mabanyamulenge ,Wakongo na Wanyarwanda ambao wengi wao mnaishi nao kama ndugu na jamaa.

    Jambo ambalo ni baya zaidi na lisilo kubalika hawa Wageni wengi wana dalili za uhalifu kama tunavyo shuhudia wanaingiza Silaha haramu nchini na hali halisi wana mkono wa damu ni vile wanatokea nchi zenye vita, wengi wao wanashiriki uhalifu kama utekaji na ujambazi hivyo wanahatarisha sana amani nchini!

    Mara zote suala la Mipaka ya nchi na Utambulisho wa Uraia ni vitu tete sana.

    Ukizingatia hadi sasa nchi yetu haija kamilisha mchakato wa Vitambulisho vya Utaifa kwa watu wake wote nchini.

    Hivyo huyo Bosi wa Mkoa wa Uhamiaji amepewa jukumu ambalo limemzidi kimo kulingana hali yenyewe halisi na hana jinsi alichobakiwa nacho ni kufanya kazi kwa kuyakalia Maombi na mafaili ili kama mtu atakuwa sio mstahiki ataghairi kuomba Hati.

    Jukumu lake ni sawa na kulinda shamba lisilokuwa na uzio mbele ya genge la Kima!

    Kitu ambacho wewe na mimi daima hatuwezi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2012

    Ni kweli kabisaa hata mimi wakati naishi kigoma nilipata tabu sana kupata passport make niliambiwa eti niwalipie nauli ya kupeleka file langu kigoma mjini sasa nikajiuliza why mimi ndo nilipe nauli wakati ni kazi ya serikali hyo? then wakasema niwape hela ya kunisaidia haraka kama naitaka mapema nikawaambia sina ikabidi niachane na habari hyo hadi nilipohama kigoma. Rushwa idara ya uhamiaji ni nzito mno inategemea fungu lako hata ukitaka passport kwa siku moja unapata ila kama huna chako basi utasubiri miezi kadhaa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 03, 2012

    Mwacheni Bossi afanye kazi yake!

    Imejengeka mazoea kwa vile Bongo ni Tambarale kila mgeni anafikiri hapa ndio sehemu yake rahisi kuweza kupata Pasipoti.

    Tatizo kubwa la Mipakani pamoja na hiyo Kigoma yenu ni wingi wa Mabanyamulenge kiasi kwamba Raia halali wanazidiwa na Mabanyamulenge.

    Shida nyingine kubwa ni kuwa familia nyingi za maeneo ya Mipakani zimechanganyika sana!,,,unaweza kukuta Baba Raia lakini mama sio raia ,au Mama Raia lakini baba sio Raia.

    Sasa Kigezo cha Utaifa ni kipana sana, sio ile tu kuweza kuongea Kiswahili na kama mnavyojua Tanzania hatujakuwa na Vitambulisho kamili vya Utaifa/Uraia hivyo wengi Mipakani wanachukua mwanya huu kujichanganya.

    KWA HIVYO KWA MAZINGIRA HAYO HAPO JUU UNAKUTA YEYE BOSSI LABDA SIYOMWENYEJI WA HAPO HIVYO INAKUWA VIGUMU KUTAMBUA NANI NI MSTAHIKI NA NANI NI SIYO MSTAHIKI.

    MATOKEOYAKE INABIDI BOSSI ATUMIE MBINU YA 'MEDANI' YA KUYAKALIA MAOMBI/ MAFAILI ILI KUJARIBU KUPUNGUZA WIMBI LA WANAOJICHOMEKEZA ILI WAPATE PASIPOTI HUKU WAKIWA HAWASTAHILI NA PENGINE VIGEZO VYA URAIA HAWAJAKAMILISHA AU PENGINE SIYO RAIA KABISA!!!.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 03, 2012

    Kigoma tatizo lipo kwa Mabanyamulenge mnaowafuga na kuwafanya ndugu zenu ambao siyo Raia!

    Inawezekana huyo Afisa wa Uhamiaji wa Mkoa hapo KG siyo kwao hivyo wenyeji wa hapo hawatambui vyema.

    Hana lingine bali ni kuchelewesha taratibu za maombi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 03, 2012

    Wewe unaelalamika kucheleweshewa Hati ya Kusafiria Kigoma.

    Unafikiri kama ilivyo Tanzania yetu Bosi atatambuaje Raia na asiye Raia?

    Ni wazi yeye siyo mwenyeji hapo Kigoma na watu wa hapo hawatambui, labda angekuwa ni Bosi mwenyeji wa hapo ingekuwa sawa.

    Hadi sasa hatujakuwa na Vitambulisho vya Uraia sasa ninyi wakazi wa mipakani mtakuwa mnawachanganya sana Mabosi wa Malaka ktk michakato kama hiyo ya utoaji wa Pasipoti.

    Mimi binafsi napendekeza Pasipoti kwa wakazi wa mikoa ya Mipakani zitolewe Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji DSM, isipokuwa mikoa ya kati kama Morogoro,Singida,Dodoma,Tabora,Lindi na Shinyanga, ndio haina wasi wasi wowote maana makabila yake yanajulikana na sio rahisi mgeni kujipenyeza hadi kupata hati nyeti kama Pasipoti!

    Mpo hapo?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 03, 2012

    Kazi nzuri Bosi wa Uhamiaji!!!

    Mikoa ya Mipakani napendekeza Pasipoti na Hati muhimu zitolewe kwa DNA (Vipimo vya chembe asili)ili kutambua uhalali wa Kiuoo na unasaba!

    Tumeshapigwa sana mabao kwa waombaji wanaojichanganya Mikoa ya Mipakani.

    Ni muhimu hili zoezi la Vitambulisho la Taifa kwa uchache lianzie mikoa ya Mipakani kukusanya DNA samples kwa ajili ya (Biometric information) za Koo na Familia zote za Mipakani zipewe kipaumbele halafu baadae tukiwa na uwezo wa Ki Fedha liwe kwa nchi nzima.

    Hii ndio itakuwa njia pekee ya kudhibiti Raia haramu wasiostahili nchini.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 03, 2012

    Mdau, umesema kweli tena mno. ila nakuomba tabia ya kujificha ficha ktika mambo ya ukeli kama haya tafadhari iondoe . Ukweli ni ukweli tu mpaka mbele za Mungu. Yaani unamuogopa mkuu wa uhamiaji wa Kigoma ?? Je ?? atakaposhinda ubunge au uwaziri au akawa mkuu wa nchi ,sasa itakuwaje ???? huyu siyo mkuu wa uhamiaji,ni mtumishi wa serikali na serikali kwa ujumla inaundwa na wananchi na mwananchi ndiyo wewe, sasa kuna cha kuogopa tena hapa ??? wewe waone takukuru dawa wanayo. Zebedayo o Nasa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 03, 2012

    Nijuavyo mimi Pasi ZOTE za kusafiria zinatoka sehemu mbili hapa Tanzania.. Makao Makuu Dar es Salaam na PCO Zanzibar...

    ReplyDelete
  11. Mkuu wa Idara ya uhamiaji Kigoma ni baba yangu, sio siri mzee anapenda sana rushwa kama wewe au nyie hamumchekeshi yani hamrefushi mkono au rushwa basi itakula kwenu mnategemea mzee na sisi tukale polisi au tule kwa mshahara wa serikali na hela ya mafuta ya v8 mzee atoe wapi na bado hajanipa mimi pesa nikawachape fimbo wenzagu kitaa, refusha mkono utahudumiwa tu in 2days, bana pesa yako utacheza viduku hadi mzee aamue.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 04, 2012

    Mdau wa PILI umesema KWELI kabisa!!!

    Tatizo hapa ni HUYO BOSI, hicho kisingizio cha sijui Kigoma mpakani wala does not hold water!

    WaTanzania tunapenda sana visingizio kukwepa majukumu, ukihoji unaonekana "mkorofi" kama mfano wa huyo bwana jela aliesema "Wananchi siku hizi wanajifanya wanajua"

    Kwani nani asiejua kuwa hapa Dar ndio chimbuko la Passport za biashara?

    Basi tu, waliokabidhiwa majukumu wamegeuka miungu watu, wameshika makali, kisingizio eti mpakani, mbona ukimlainisha kiganja anakuita mzee na pasi unaipata baada ya siku cha che tu????????

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 04, 2012

    Ni ofisi nyingi za uhamiaji mikoa. Nenda mwanza na pengine. Wakati mwingine siyo boss bali wafanyakazi wa chini wanaotaka rushwa ili apeleke faili kwa boss. Imeshawahi tokea kwa binti yangu. Ilikuwa nenda rudi. Ikabidi niende kwa boss, kumbe alikuwa hajapelekewa faili. Boss alikasirika ile mbaya na kutukana sana wafanyakazi wa chini yake. Fomu zikasainiwa na sasa nina pasipoti.


    Bora wakucheleweshee lakini katu usitoe rushwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...