Ankal akitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kotoka jijini Accra, Ghana, ambako baada ya kutangazwa kwa maombolezo rasmi ya siku tatu kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Hayati John Evans Fiifi Atta Mills. Rais huyo, aliyefariki Julai 24, 2012 kwa saratani ya koo, anatarajiwa kuzikwa Ijumaa hii katika mazishi yanayotarajiwa kuhudhuriwa na marais 16 pamoja na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mama Hillary Clinton.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hivi unko mimi nina swali....Hiyo T-shirt haichujuki wala haiishi wala haichaniki wala haina doa? mh! Hebu tueleze wadau wako tujue. Kwa kweli toka niijue hii blog yako hiyo tishirt nayo ilisha kuwa ina exist. Sasa kaka hapo imekaaje hii?

    ReplyDelete
  2. Ankal kila la heri......ACCRA mji wenye kumbukumbu nyingi katika maisha yangu.....ndio ulikuwa mlango wa mimi kuhamia ughaibuni.....

    ReplyDelete
  3. zeeee fulanazz ankal!!!! ha! ha!ha! super sana!

    ReplyDelete
  4. Hivi hiyo "Ze Fulana" yako, huwa ni kama vile 'emblem' yako au ni kitu gani? Ina maana unazo kadhaa zinafanana au ndio ile ile moja ya miaka hiyo kama ya dawa? Laiti kama ndio hiyo hiyo, basi unajuwa kutunza na umaridadi juu, hongera kwa kuienzi ZE FULANA yako, mana ingalipo tu, haichujuki na wala haichakai, utadhani imetengenezwa kwa kwa nyuzi za chuma!

    By the way, kila la kheri nchini GHANA na pia kwa kutuwakilisha Watanzania wote kwenye msiba (Mazishi) ya Hayati:John Evans Fiifi Atta Mills (1944-2012) May GOD rest his soul in eternal peace - AMEN.

    ReplyDelete
  5. inawezekana anazo nyingi za aina hiyo hiyo maana niliwahi kuwa na rafiki akienda dukani akipenda shati anayanunua saba hivi so inawezekana ankal ni mmojawao maana haiwezekani shati likawa hivyo siku zote au inawezekana ndio nembo yake pia hahaha

    ReplyDelete
  6. Duh! hiyo T-Shirt yako bado ipo tu,

    ReplyDelete
  7. wewe mtoa maoni hapo juu, kwa nini mnakuwa hamna kitu cha msingi cha kutoa maoni ??? mtu mzima kweli na ndevu chini,halafu unakuwa na akili zilizojaa pumba namna hii ?? eti T-shirt haiishi wala kuchanika !! swali gani hilo ?? is that common sense ? nina suruali nilishonesha India miaka 20 iliyopita ,mpaka sasa ninayo na bado mpyaa,of course naivaa siku moja moja kwenye event kama vile t-shirt ya Ankal. I hope i answered your NOT smart question dude. Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  8. Ankal kila heri.... ebu jaribu kudodosa, manake ww ni mwana habari,kuna mambo mengi hapo yanafanyika Accra=Dar(copyright)

    David V

    ReplyDelete
  9. ze fulanaz.......

    ReplyDelete
  10. Lishe Ghana,

    Ankal Waghana popo (njiwa wa usiku) kwao ni kitoweo !

    Jihadhari ukiona vipapatio vimebanikwa na tui la nazi la kuchaza,,,Mnhhh usile uliza kwanza!

    ReplyDelete
  11. Ankal Dakitari au (Mwalimu)au Sheikh aliyekukabidhi hiyo fulana, ah naona ni siri yako huwezi kumwambia mtu ni nani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...