Kaimu Afisa Mtendaji wa benki ya CBA Bw Julius Mcharo, akizungumza kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.katika futari hiyo Bw Mcharo aliwashukuru wateja wote wa CBA na kusema kuwa benki yake inaungana na jumuia ya waislamu nchini na duniani kote katika kuadhimisha mwezi huu mtukufu Ramadhan na benki ya CBA itahakikisha inaendelea kua benki imara na makini katika kuhakikisha kua kila mteja anapata huduma iliyo kamilifu na kukidhi matakwa yake.Bw Mcharo aliwatakia waislamu wote Ramadhan Karim.
Mkuu wa kitengo cha Makampuni wa benki ya CBA Bi Fatma Abdallah, akizungumza kwenye hafla hiyo ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...