Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akikabidhi hati ya uteuzi kwa Mhe. Bahati Ndeserua Moshi kufuatia uteuzi wake wa kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mkoa wa Pwan. Kabla ya Uteuzi wake Mhe. Ndeserua alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Kibaha.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akikabidhi hati ya uteuzi (Instrument of Appointment) kwa Mhe. Seif Mwishehe Kulita kufuatia uteuzi wake wa kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mkoa wa Tanga. Kabla ya uteuzi wake, Mhe. Kulita alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi-Wilaya ya Mbeya, kulia kwa Mhe. Kulita ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Ignas Paul Kitusi.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Kiongozi, Mhe. Fakih R. Jundu (mwenye tai nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi Wafawidhi walioteuliwa kuongoza mikoa ya Tanga na Pwani, kulia kwa Jaji Mkuu ni Mhe. Seif Mwishehe Kulita Mahakama ya Mkoa waTanga, na Kushoto kwa Jaji Kiongozi ni Mhe Bahati Ndeserua Moshi wa Mahakama ya Mkoa wa Pwani, anayeshuhudia kutoka kushoto ni Msajili Mkuu wa Mahakama, Mhe Ignas Kitusi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...