Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh. Chiku Galawa akipeana mkono na Meneja Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyo wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini, Halima Dendegu.(Picha na Habari Mseto Blog)
Baadhi ya wageni wakipata futari.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Chiku Galawa (wa pili kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini,Mh. Halima Dendegu (kushoto) wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa wateja wake na kufanyika kwenye Uwanja wa Mkwawani jijini Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Taga,Mh. Chiku Galawa akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa ajili ya wateja wake.
Meneja wa Huduma kwa Wateja, Godwin Semunyo akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Meneja wa CRDB Tawi la Tanga, Evalist Mnyele.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteini mstaafu, Chiku Galawa (wa pili kulia) akiteta jambo na Meneja wa CRDB Tawi la Tanga, Evalist Mnyele. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini, Halima Dendegu na kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa CRDB, Godwin Semunyo.


I am tired and sick of this thing on MIchuzi blog "Futurisha Futari FUtari... " it's like a fashion now every where theyr trying to do that and I' m not sure if they all aware of religious principals! It's all abou eatin eatin and eatin man.. I am not a muslin but thats wat comes out of my mind after learning this from MICHUZI blog plse Nielimisheni KHaaaa,!!
ReplyDeleteBlog fun abroad
Naona kina mama bongo wanava diraa mavazi ya kisomali
ReplyDeletemichuzi huyo jamaa anaesema yupo abroad sijui wapi.kinachomkera nini?futari au waislam kufuturu ?wewe kama umechoka kuna habari nyingi tu humu zisome. usijilazimishe kitu usichopenda ukisome.nawala hii sio blog yako ukamfundisha michuzi cha kuweka. hujachangishwa pesa yakufuturisha wala hukuitwa ufuturu.angalia lako. usifanye watu wakakujibu yasio faa bure. kabla hujandika fikiria nini unaandika au pitia kabla hujaipost comment yako.
ReplyDeleteKabla Ramadhani tulikuwa tunaona Naam, awali kwenye libeneke hili tulikuwa tunaona nyamachoma mabilimbali zilizoandaliwa na makampuni mabali mbali kama mdau wa ukweli utakuwa unakumbuka. Ni mwezi mmoja tu kwa mwaka watu wanafunga na kufutarisha tayari umeshachoka. Mdau unatakiwa uwe mvumilivu wa Iman zingine sio unakurupuka tu. Pia kama utakuwa unazunguka humu utakuta habari za humu ni za msimu kunawakati huwezi kuingia kwenye libeneke bila kukuta habari kuhusu miss somewhere, tunavumilia siku inapita. Lkn wewe kidogo tu I am tired nakuonya usirudie tena mdau wa kwanza hapo kutoa maoni.
ReplyDeleteMimi ni Muislam wala hainichokeshi.
Mdau UK
Futurisha means Business!!
ReplyDeleteAsalam alaykum.
ReplyDeleteMimi ni muislam. Nahisi mdau wa kwanza alie toa maoni ni muuislamalichokuwa anataka kuonyesha kuwa mashirika yamekuwa yanatumia ftari kufanya matangazo ya Biashara zao.
Lkn akiwa sio muislam na ameuliza swali hatakama swali lake laonekana kijazba inatakiwa kujibiwa tu KTK Mwezi wa Ramadhan kwawale walio funga ni jambo kubwa kumpa mtu futari(chakula) lina malipo makubwa mnoo.
Baada ya kufunga kila mfungaji ameihisi hali yakukaa muda mrefu bila ya kula(njaa) hapa anapata mazowezi ya kutoa.
Kwahiyo baada ya Ramadhani tuna tegemea haya mashirika na Rais na wizara za serikali na watu binafsi ambao wana uwezo wamimine wavyakula ktk sehemu zinazo lelewa mayatima na wazee na kila asiye jiweza wapatiwe vyakula.
HIVYO KAMA RAMADHANI ITAKUWA IMETUFUNZA INABIDI TUONE WALE WALIO KUWA WAKITOA WAZIDI ZAIDI NA NJAA IWE NIMSAMIATI HAUPO TENA KTK JAMII YETU.
NADHANI NITAKUWA NIMEMJIBU MDAU.
NAKUOMBA BWANA MICHUZI USIIKALIE MAONI YANGU
+
Mwezi na ndio umo kumalizika tena, naona mara hii hizi futarisha na kufuturu zimehanikiza, basi na siku ya EID itapendeza tukisikia hao wote waliojaaliwa kufutarisha na wengineo zaidi kama wapo, basi pia waje kujumuika pamoja kwa chakula cha machana katika kusherehekea siku hiyo adhimu ya kuumaliza MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN panapo uhai na uzima INSHA ALLAH. Na sio Ramadhan tu ndio mjuwe kuna kujumuika pamoja, tunataka sasa iwe ni mojawapo ya desturi zetu kujumika pamoja, kutowa misaada ya hali na mali na kuwasaidia wasiokuwa na uwezo, mafukara, mayatima, dhalili na wenye hali duni, kushiriki nao kwa hali na mali kama baadhi yetu mlivyoonekana kujumuika nao katika Kuftari nao pamoja. Mwenyeez Mugnu atuwezeshe juu ya hilo, INSHA ALLAH. Nazidi kuwatakia RAMADHAN KAREEM.
ReplyDeletejamani mdau wa kwanza amoeba tu kuelimishwa,sasa ni hivii ndugu ktk mwezi wa ramadhani waislamu wanfunga kutwa mzima ya kumaanisha kua hairy usual kwa aliye funga kula chakula,kunywa maji au chochote kupita kooni mpaka jua likuchwe.Na ni kawaida kabisa kwa waumini wa dini hiyo kukusanyika na kupata chakula wakati wa jioni pamoja na ndugu,jirani au marafiki kwa dhumuni la kuimarisha upendo na amani kwenye jamii na Hilo ndio nguzo moja kuu ya ibada hii ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
ReplyDeleteNatumai unajua kusoma kiswahili na hayo yamejibu
kero lako au Kama unakerwa zaidi na hili la michuzi
kuweka picha za "futukuriha,futari,futari" basi nakushauri usifungue blog ambayo inathamini na kuheshimu maadili na taratibu za watu huru bila ya ubaguzi.
Ahsante.
N.b na Kama unapendelea page 3 ya the sun pia uko huru.
FUTARI/ KUFUTURISHA:
ReplyDeleteHao Wadau wasiotaka ni wajinga wa masuala ya Habari.
HII BLOGU NI JAMVI LA HABARI, ZIPO ZA MICHEZO, ZA SIASA, ZA KIDINI-KIKRISTO NA KIISLAMU , ZA KIJAMII ZA KIUDAKU NA PIA HABARI ZINAENDA KULINGANA NA MISIMU, IKIFIKA MWEZI WA DISEMBA EWE MKRISTO TUTAKUWA PAMOJA NA SISI WAISLAMU WAKATI LIBENEKE LITAKAPO TANGAZA KUHUSU KRISMASI.
HIVYO KUKEREHEKA KUONA HABARI ZA FUTARI MSIMU HUU NI KUKOSA AKILI ZA KUJITAMBUA TUPO MSIMU GANI.
ANGALIA MAMENEJA NA WAKURUGENZI WENGI WA MABENKI NI WAKRISTO WATU WENYE AKILI NA UWEZO KIFEDHA NA KIHALI NA WALIOSOMA ZAIDI YA NINYI WAKRISTO WACHACHE WAJINGA VIBWETERE HUMU JAMVINI, LAKINI LICHA YA KUWA WAO NI MABOSI WAKRISTO KUPITIA TAASISI ZAO WAMEUTHAMINI KUUHESHIMU MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA KIISLAMU NA WAMETOA FUTARI KWA JAMII YETU.
TUELEIMIKE, TUPATE MUAMKO NA TUACHE UTENGANO NA UCHOCHEZI BAINA YETU.!!!