Pamoja na kwamba mji wa Moshi ndio unaosifika kwa usafi hapa nchini.lakini hawajafanikiwa kudhibiti ufanyaji biashara wa kiholela unaofanya na wakazi wa mji huo katika maeneo ya pembezoni mwa barabara za mji huo kama kamera ya Globu ya Jamii ilivyoweza kuzinasa taswira hizi siku za hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hamidu HamiduAugust 11, 2012

    Karibu asilimia tisini ya wafanyabiashara za mitaa za kuzunguka kwenye jua kali ni akina mama,du poleni sana mama zangu.

    ReplyDelete
  2. safi sana matunda yote hapo ni mazuri matamu na ni nature sio yale ya kupandikiza kwa madawa

    inshaallah kwa uwezo wa allah nikifika tz nitajitahidi nifike mpaka moshi.

    ReplyDelete
  3. angalia jinsi ambavyo muuza chungwa hamwagi uchafu pembeni, kama wanaweza kumaintain hali ya usafi kwa kiwango hicho kwa nini wasiruhusiwe kufanya biashara.

    ReplyDelete
  4. Wee wa ajabu kweli! Ulitaka wafanyie wapi biashara zao. Wenzio wanafuata masharti ya usafi iyo ndio mhm. Hiyo mikoa mingine vipi? jirani zao jeneva ya Tz kama mnavowaita mvua ikanyesha kidogo kunanuka hapafai. Waache wapate mlo wao wa siku.

    ReplyDelete
  5. Wee wa ajabu kweli! Ulitaka wafanyie wapi biashara zao. Wenzio wanafuata masharti ya usafi iyo ndio mhm. Hiyo mikoa mingine vipi? jirani zao jeneva ya Tz kama mnavowaita mvua ikanyesha kidogo kunanuka hapafai. Waache wapate mlo wao wa siku.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli Moshi unaweza kusema biashara zinafanyika kiholela, lakini tofauti kubwa na miji mingine ni kwamba biashara hizo zinafanyika katika mazingira ya usafi. Kwa mfano, picha ya pili kutoka chiniinaonyesha akina mama wakiuza machungwa lakini chini hakuna ganda hata moja. Katika picha ya chini sioni uchafu wowote katika sehemu hiyo ambapo akina mama wanauza matunda.

    ReplyDelete
  7. Mimi sidhani kama suala ni kuwaondoa wananchi wanaotafuta riziki zao kwa njia halali, pamoja na kufanya Biashara pembezoni mwa barabara bado mazingira yanayozunguka Biashara hizo ni masafi na yanapendeza. Mimi naunga mkono uamuzi wa manispaa ya Moshi kuwaruhusu wafanyabiashara ndogo ndogo nyakati za jioni baada ya muda wa kazi.

    ReplyDelete
  8. mdau wa pili na mie kama wewe hapo nimeona matunda tu. jamani kuwa mbali na nyumbani nako kuna mateso yake manake ningekuwa dar ningedandia basi hadi moshi.
    mungu akipenda nitakuja moshi kwa ajili ya hayo matunda.

    ReplyDelete
  9. Huku kuuza vyaakula chini is not healthy hata kama wanajitafutia ridhiki but sheria zifuatwe na masuala ya afya pia.ni vizuri yatengwe maeneo maalumu ya soko ili wapange vitu nyao kwenye meza,hii itarahisisha pia manispaa husika kukusanya ushuru kwa maendeleo ya pahala husika.tuache kushabikia utaratibu usiofaa kwenye jammi zetu regardless wheather ppl r trying to make their daily bread.sheria zifuatwe na afya ya mlaji izingatiwe otherwise tutakuwa tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele

    ReplyDelete
  10. Ni kweli, kuna ufahamu na utekelezaji wa USAFI wa hali ya juu sana.

    Picha ZOTE hakuna hata trace ya waste za bidhaa zao.

    Lakini hata Dar naona wauza machungwa wanatoa mifuko, wauza madafu wanazingatia usafi. Tunajaribujaribu sema tumeelemewa.

    ReplyDelete
  11. wewe unayetaka kupanda ndege eti uje ule matunda Moshi, wacha kejeri zako, wewe baki huko huko tu kula matunda frozen, tuache sisi tuliositahimili tufaidi nchi yetu. cheki huyo mama na matunda yake ,yaani ni mradi wa $ 30 tu au chini ya hapo, hapo ana watoto wanakwenda shule,na hapo kama unavyomuona kanona na ana afya njema na simu anayo. Huko ndiko kujitegemea ,siyo kuilalamikia serikali kila kukicha ( hatuna kazi) wengine majuzi tuliwaona wana zuia wall street huko USA ,kisa nini ,hawana kazi.In bongo we live from our own means. Na mukome kutuita eti nchi masikini. Please ,stop that crap name now. Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  12. NIMEFURAHIA SANA MADA HII NAOMBA NISEME MACHACHE. MICHUZI NAOMBA IRUDISHE TENA.

    1. MAKAMPUNI YA SIMU, BENKI YANGEWASAIDIA BAISKELI ZA BIASHARA ZA KUSUKUMA NA YAWE NA SEHEMU YA TAKA. ITAWASAIDIA SANA AKINA MAMA.

    2. TOKA MADIWANI WA CHD KUWA WENGI KWENYE MANISPAA YA MOSHI. WAMEKUWA WAKITETEA SANA HAWA FANYA BIASHARA KUENDELEA KUZAGAA MITAHANI BILA KUJALI SUALA LA WENDA KWA MIGUU WAPITE WAPI NA HATA MAGARI YA PACK WAPI.

    3. MADIWANI NA HALMASHAURI TATUENI HILI MAPEMA NI KERO SANA HATUJAZOEA UCHAFU HUU NA KERO HII

    4. UKWELI NI KWAMBA MJI UNAANZA KUHARIBIKA MAMA KINABO = MKURUGENZI HANA SUPPORT NZURI YA MAENDELEO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...