Mzimu wa ajali za barabarani umeendelea kulitikisa Taifa letu baada ya kutokea kwa ajali mbaya sana siku kadhaa zilizopita huko mkoani Tabora na kupelekea vifo vya watanzania 17 na wengine 78 kujeruhiwa vibaya sana baada ya basi la abiria la Sabena kuanguka,Asubuhi hii watu wengine kadhaa wameripotiwa kupoteza maisha huku wengine zaidi ya 15 wakiripotiwa kujeruhiwa vibaya baada ya ajali mbaya iliyohusisha magari manne iliyotokea eneo la Makole kilichopo karibu na eneo la Mto Wami mkoani Pwani.
Ripota wa Globu ya Jamii ambaye ametuletea taarifa hii anaripoti kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili na lori la Mafuta na kufanya barabara hiyo kufungwa na hakuna gari yeyote inayoweza kupita huku majonzi yakiwa yametawala katika eneo hilo.
Katika eneo la Lugoba mkoani Pwani pia kumetokea ajali nyingine ya lori la mafuta kushika moto ambapo nalo chanzo chake hakijaweza fahamika mpaka sasa.
Wananchi wa eneo hilo wamejazana katika eneo la tukio huku wengine wakijizolea mafuta yanayoka kwenye gari ambalo lilikuwa limepamba moto wakati wote.
Globu ya Jamii inafanya jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani ili aweze kutupatia taarifa kamili juu ya matukio ajali hizo.


jamani watanzania poleni kwa kweli hili ni janga kubwa coz hatutaisha kufuta machozi,tumuombe sana mungu atusaidie na kutulinda
ReplyDeletekwa mtindo huu madereva feki watatumaliza
ReplyDeleteHII NI KAWAIDA TU HAPA TANZANIA. TUMSHAZOEA. MADEREVA WAMEKABIDHIWA KIBALI KUTMALIZA WATANZANIA
ReplyDeletePolis washindwa kuzibiti ajali..mm naona sasa ni muda umefika..wakabiziwe jeshi là wananchi kuwazibiti hawa wauaji..na wote wamiriki wa mabasi...watz tuamke usingizini..kwa sababu wamiliki wa mabasi wengiwao sio watz halisi ndio maana hawajari lolote kuhusu hizo ajali coz wanaokufa na kuumia sio ndugu zao kabisa..naomba wahusika walifanyie kazi hili swala pliz tumechoka na kuzika ndugu zetu kwa vifo vya kirazima..ni mm mdau wenu..tajiri wa mawazo endelevu.
ReplyDelete