Chama Cha Walimu Tanzania (CWT)kimetangaza kusitisha rasmi mgomo wa walimu na hivyo kuwataka walimu wote nchini kurejea kazini mara moja kuanzia leo ili kutekeleza majukumu yao ya kila siku kama kawaida.
Akitoa tamko la CWT kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kukiagiza Chama hicho kitoe maelekezo kwa wanachama wake kurudi kazini, Rais wa Chama hicho, GRATIAN MUKOBA (pichani), amesema walimu wanarudi kazini wakiwa wamekata tamaa kutokana na hukumu hiyo.
Amefafanua kuwa walimu wanaporudi kazini bila kuwa na mawazo yaliyotulia, utendaji wao utaathirika hivyo Chama kinatoa wito kwa Serikali kukutana na CWT kwa haraka ili kuendeleza majadiliano ya Madai mapya ya Walimu.
Kuhusu kulipa fidia ya hasara waliyoipata wanafunzi, Chama hicho kimesema kinasubiri taarifa rasmi ya Serikali kuhusu hasara hiyo kwa kuwa hakina uwezo wa kufahamu hasara waliyoipata wanafunzi.
Kwa mujibu wa Mwalimu MUKOBA wenye uwezo wa kuwasilisha hasara hiyo ni mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni Serikali.
Hapo jana Chama hicho kilipongeza kauli ya Rais JAKAYA KIKWETE yakusema Serikali inajali na kuthamini mchango wa Walimu nchini.


.jpg)
Hasara hamtaiona sasa hivi ndivyo ilivyo sekta hii ya elimu, mpaka baadaye, baadaye kiasi gani hakuna anayejua mpaka mtakapo kuwa na Taifa la watu mbumbumbu, mnakuta tu Rais mliomchagua anaongea utumbo umoja wa mataifa, ndipo hapo wazungu watasimama na kutoka nje ya kikao huku wakinong'onezana, huyu ndo Rais wa Tanzania? basi kama ndivyo basi huko Tanzania wamejaa viwete na huyu ndo Rais wao. Ndo maana yake,
ReplyDeletekwahiyo nisingeshauri Serikali kupenda kuwatania Walimu hiyo ni mbaya sana.
We mdau hapo juu nafikiri ndio unaongea utumbo kabisa! Si vyema kutoa mfano wa kiwete jifikire mara mbili maana ya kiwete na ufanisi wao!
ReplyDeleteSerekali imeoza imeoza tu kwa ajili ya uroho wetu waafrika. Nchi nyingi za kiafrika hazitofautiani! elimu ndogo ni kweli! ufanisi hafifu na huo ndio tuite ujinga na si ukiwete.
NdO hii niliyokuwa nazungumzia hapa, Sasa huyu mdau namba mbili anashindwa kutafisiri maana ya kiwete hii niliyoitaja hapo juu, na huo ndo umbumbumbu wenyewe, mimi simaanishi kiwete katika maana ya kiwete, mimi ninamaanisha kutokua na uelewa, ukiwete wa elimu ya kuweza kufafanua na kutafisiri mambo kisawasawa ndo ukiwete nilio maanisha hapa.
ReplyDeleteBe careful when reading comments from Elite people Ok!
Hiyo ni Lugha ya picha tu, wala siyo kiwete katika maana kiwete, honey got that?
WALIMU WALIKOSEA WANGEKUWA WATUMISHI WA CHAMA AU USALAMA WA TAIFA WANGEFAIDI PESA ZA NCHUI LAKINI WALIE TU
ReplyDeleteMheshimiwa Mukoba yuko strategic, amegundua kuwa hakuna haja ya kusuguana na serikali na wakati kuna sehemu wamekosea katika kufile mgomo. Wanarudi kazini wanaangalia kama hakuna mabadiliko wanarudi tena uwanjani huku wakizingatia sheria na taratibu za mgomo. Kimsingi serikali isipojua umuhimu wa mwalimu tutajenga taifa lisiloweza kuenda na wakati na kila siku tutakuwa ombaomba tu maana hatuwezi kutumia mbinu ya kujitafutia.
ReplyDeleteMukoba kaza uzi waalimu tuwe na maisha bora kama nchi zilizoendela.
kiwete alokusudiwa na anony wa kwanza ni kikwete
ReplyDeleteJamani hakuna elimu ya bure,,, Lipeni hela watoto wenu wasome vizuri kama hamtaki kwendeni zenu... walimu rudini kazini acheni ujinga na ndoo maana walimu wengi ni wale walio feli form 4 na six
ReplyDelete