Since the President of Tanzania, Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, addressed the Nation on 31st July 2012, I have received numerous calls and messages from people asking me, “How much does a CT Scanner cost?”  This is because in his Speech, the President said some people are comparing the price of SUV Landcruiser (shangingi)  to a price of CT scan. He even said jokingly " Waje Tuwape pesa wakatuletee...Labda waende China", Well I have one message to Mr. President, 'even in China, You cannot get a CT for a price of a Landcruiser'.
 
The views am going to write are informed by  my 10 years experience in the Medical Systems Industry-having worked  for Philips Medical Systems and their sole Distributor in Tanzania. I want to share with my readers, and my fellow Tanzanians an insight of what real cost of CT Scan is. As an expert in Finance, I find it prudent to let my readers know what it takes to invest in CT Scan.

What is a CT Scan?
PHILIPS 64 Slice Brilliance CT
X-ray computed tomography, also computed tomography (CT scan) or computed axial tomography (CAT scan), is a medical imaging procedure that utilizes computer-processed X-rays to produce tomographic images or 'slices' of specific areas of the body. These cross-sectional images are used for diagnostic and therapeutic purposes in various medical disciplines.
How Much does a CT Scan Cost?  and that is just too broad of a question. It is a little like asking how much a car costs. A Toyota Corolla isn’t going to cost you much... you may be able to just pull it for 5M… but that 2012 Mercedes-Benz C-Class is going to be a touch more expensive.
So in order to make sure you get the CT Scanner you need for the right price you should be ready to answer the following questions:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Baada ya kuisoma mada hii mpaka mwisho, mwandishi anaonekana kuonesha kuwa CT scanner ni ghali sana. Ukiendelea mbele mwandishi anatoa bei tofauti za CT scan kati ya dola 400,000 na 1,500,000;na mwisho anaonesha kuwa ni kama KEJELI kulinganisha bei ya CT scan na bei ya Landcruiser. Hapa naamini kuwa mwandishi ameshindwa kuelewa kuwa wananchi wanapodai CT scan wanaangalia bei ya landcruiser zaidi ya moja. Yaani landcruiser kati ya 300-400 za wabunge. Yaani idadi ya landcruiser400 zidisha kwa dola $60,000...gawanya kwa bei yake ya juu ya CT scan $1,500,000.Kwa kifupi tukiondoa SIASA mengi yanawezekana

    YES WE CAN...

    ReplyDelete
  2. Ww anonymous wa kwanza ndio wale wasaburi wa siku zote, nani kakwambia mashangingi ya wabunge ni ya serikali? Huo ni ulimbukeni!

    ReplyDelete
  3. Hapa UK zipo za "used" £100,000 lakini ukavungue mwenyewe hospital!!

    ReplyDelete
  4. @Mchangiaji hapo juu, kama wanalinganisha na landcruiser nyingi basi tunaweza kusema bei ya CT scanner ni sawa na bei ya kalamu kwa sababu ukichukua bei ya kalamu moja ukazidisha mara fulani utapata bei ya CT scanner. Kama ni hivyo kuna significance gani kuifananisha na bei ya gari?
    However, ukweli ni kwamba hatushindwi kuwa na CT scanners nyingi lakini ili tuwe nazo ni lazima wataalam waseme kuwa hicho ni kipaumbele katika sekta ya afya. Ni kichekesho kutumia limited resources kununua CT scanners wakati kuna watu wanakufa kwa kukosa medical oxygen! Yes we need CT scanners, lakini hatujafikia hatua za kuzifanya kipaumbele.

    ReplyDelete
  5. yes nakubaliana na mdau wa kwanza hapo juu.hivi kuna ulazima wa kila mkurugenzi serikalini kuwa na landcruiser?nafikiri zipo gari za gharama nafuu zinaweza kutumika kama mbadala wa landcruiser.

    ReplyDelete
  6. Anonymous. Hebu na wewe acha kuweka maneno anbayo hayakusemwa na yule katibu wa daktari ambaye sisi tulimsikia live. Alisema bei ya CT scanner ni sawa na VX moja. Hayo ndio maneno aliosema. Rais JK alichosema ni sahihi na huyo mtaalamu alivhosema ni sahihi. Hao madaktari pengine na wewe nyie mmeshalia uanharakati tu. pamoja nayule nani sijui helen kijo. Badala ya kuwatetea wagonjwa anashiriki kuwaua. Kipigo cha Ulimboka ni findisho na ni laana atakayokuwa anatembea nayo siku zote za maisha yarke. Mtibuni na hata mkitaka kumbadilisha sura yake ibadilisheni tu. hana maana ndani ya jamii yetu huyo!

    ReplyDelete
  7. Labda mawaziri na wabunge waanze kutumia Bajaj ndio tutaweza kununua CT Scan kwa ajili ya Hospital zetu.

    ReplyDelete
  8. Mdau ulitangulia naona umefunguka kidogo... Landcruiser VX jipya na kodi yake ni 236Mil TZS. Sasa mawaziri wangapi wananunuliwa VX? CT scan ya $1,500,000 ishindikane kununuliwa kwa nini? EPA wahuni wachache walijinufaisha na 330BIL TZS. Maka wa CCM wa Kigoma wenyewe(mtu na ndugu ye) walikula 3.2BIL(takriban 10% cjui ndio ilikuwa posho ya udalali?)Hiyo hela ingetosha kabisa kununua CT scan ya bei ya juu.... mifano iko mingi.. SIASA za kifisadi na kutokuwa wazalendo ndio tatizo letu. Hata maneno ktk wimbo wa taifa ni kumkejeli mungu ndio maana majanga haya yanatukuta. Mbona wakipewa mikopo ya maendeleo (MCT mfano hawatengi hata 10%) kununulia CT Scan kwa manufaa ya wananchi 40mil ? Mungu ibariki africa mungu ibariki tanzania.

    ReplyDelete
  9. Ni bora kuboresha sekta ya Afya kwa nguvu zetu wenyewe.

    Tukiwatumia vizuri wanasayansi wetu wanaweza kutengeneza vitu kama hivi ,ila kwa sababu ukoloni bado upo basi mizengwe itawekwa.

    Pia ,kama sisi ni wanachama wazuri wa Umoja wa Mataifa iweje nchi rafiki zitutangazie kuwa zinatupa misaada isiyo na maana na wasituletee vitu vya umuhimu kama hivyo.

    ReplyDelete
  10. hata ikiuzwa bilioni inunuliwe, kama inaweza kuokoa maisha ya maelfu ya watanzania kwa nini isiwepo hospitalini? ina maana chombo hiki hakitanunuliwa sababu bei yake ni kubwa? mbona hospitali binafsi wanazo kwani wao walipewa bure? na hizo kodi zinazotolewa na wananchi kazi yake moja wapo iwe ni hii, badala ya watu wachache kujipendelea kama vile wao wameumbwa na udongo uliochanganywa na gold. chuchunge zebedayo njoo tiririka hapa!

    ReplyDelete
  11. goog explaination from 1st comment..kifupi hata tukiacha mashangingi yao hayo nchi ambayo inajali wananchi wake haikosi about 1.8billion kuwanunulia wananchi mashine itakayowaokua wengi kwa uwezo wa mungu wakapona kuendelea kuzalisha zaidi..pesa za rais kwa ajili ya safari zilizodaiwa kupotea kwenda hapo ethiopia tu zilikuwa sio chini ya 3.5bilion, sasa ina maana rais akiahirisha safari moja tu ya kwenda ulaya tunapata ct scan pengine 3...

    YES WE CAN DO THIS

    ReplyDelete
  12. Mimi kwa kweli mwandishi nimemuelewa sana tu. yeye amemnukuu Raisi kwenye CT kwamba wanalinganisha bei ya CT na Landcruiser moja. na mimi nilielewa hivyo. bila hii mada kuandikwa nilikuwa najua ni hivo. kwa hivyo kweli ni ajabu kulinganisha hivyo viwili.
    halafu mtoa hoja hapo juu. yale magari ya wabunge ujue sio ya serikali! ni ya kwao wanakopeshwa na wanakatwa kwenye malipo yao. angalia tu idadi ya magari ya wizara na serikali sio ya wabunge.

    ReplyDelete
  13. Nilivyoelewa mimi ni kuwa Mwandishi ameweka maoni yake kutokana na uelewa, ujuzi na mazoea yake ya chombo cha CT scan bila mtazamo wa kisiasa au Chama. Kiukweli ameeleza, ameelimisha na kuifundisha jamii haswa sie wengi tuliokuwa tunaziona hizo CT mahospitalini bila kujua dhamani wala umuhimu wake! Kulinganisha CT scan na Landcruisers ilikuwa ni kujaribu kutufafanulia kiundani dhamani(kibei) ya CT scan kiufasaha, badala ya kulaumu serikali kwa kila jambo! Thanks monfinance.com for that informative news! welldone and keep it up!

    ReplyDelete
  14. Anony Sat Aug 04, 05:15:00 AM 2012 umehitimisha vyema.

    ReplyDelete
  15. Mi nilisoma kwenye mtandao wa JF wameandika hivi! "Dr. Chitage: Mashine moja ya CT scan ni sawa na bei ya Toyata shangingi moja! ....Katibu wa jumuiya ya madaktari nchini ameweka wazi kuwa bei ya mashine moja ya CT scan ni sawa na bei ya kununulia shangingi moja.Alisema kama serikali ingekuwa na nia ya kununua mashine hiyo isingeshindwa. kwa habari zaidi soma gazeti la mwananchi la leo." hii ilikuwa post ya tarehe 1 July. Nikashangaa huyu Daktari mzima anahadaa watu. Ni kutaka tu uonekane nawewe umetoa hoja.Mwandishi hakukosea walisema CT MOJA NI SAWA NA SHANGINGI MOJA! Afadhali ametokea mtu wa kusema ukweli. sasa angalia maneno haya ya uchochezi yanaleta madhara gani kwa wananchi na serikali yao.

    ReplyDelete
  16. Nimesoma maelezo ya mwandishi, nampongeza kwa uandishi mzuri. Hata hivyo, ningependa kutoa angalizo kwa mwandishi pamoja na raisi.

    Kuongeza maoni ya mchangiaji hapo juu, Landcruiser zinatumika kama kiwakilishi cha matumizi yasiyo ya lazima yanayofanywa na serikali.

    Ni vizuri kukumbuka kwamba ulinganisho ni kati ya afya na usafiri wa watumishi wa serikali. Tunalinganisha kati ya gharama za maisha yanayopotea kila siku kwa kukosa vifaa vya kutambua magonjwa ikiwemo CT Scan, ulinganisho wa gharama za kupeleka watu India kufanyiwa matibabu ambayo madaktari wetu wanaweza kufanya bali wanakosa vifaa.

    Nawakilisha,

    Ignorant

    ReplyDelete
  17. Kwani sio kama serikali inashindwa kununua hivyo vifaa vya hospitali,bali wizara husika wanashindwa kufanya kazi ipasavyo,budget kila siku zinapitishwa mabilioni ya fedha wanashindwa kunua hivi vifaa ?

    Waziri husika yupo ? Viongozi wetu wengine wako wapi ? Pengine kama utauliza utaambiwa muhimbili ipo,kichekesho,hivi tuseme muhimbili tanzania nzima ndio tegemezi letu ? watu milioni 43 population yetu tunategemea muhimbili ?

    Tunaomba wasomi wetu wafanye utafiti wa kina katika suala hili,tunahitaji kila mkowa kuwe na hopital ya uhakika na vifaa vyote vya uhakika chekinga na matibabu,uwezo serikali inayo,rasilimali tunazo,uchumu mzuri na wa uhakika,wananchi hatufaidiki na rasilimali zetu.

    Viongozi wao wakiumwa na ukucha tu,wanakimbilia ulaya au india,wakatika kuna mamilioni ya wananchi wanateseka kwa kukosekana matibabu ya uhakika na huduma za uhakika.

    Hatutaki hospitali tegemezi kama muhimbili,tunataka kila mkowa kuwe na University hospital,ambayo itakayo kidhi kwa wananchi wote wa mkowa.

    Tununulieni hivyo vifaa,acheni ulafiiii

    Na Miunda UK.

    ReplyDelete
  18. Mdau wa hapo juu nakubaliana na wewe. Kwamba kwa magari matatu ya wabungebtayari kutakuwa na CT scan , recondition in China kwenye hospitali moja wa ya wilaya, mfano Bumbuli. Na tukiendelea kuuza haya magari kumi ili wabunge watumie magari ya kawaida, badi hata hiyo the most expensive tutaweza kununua tatu kwa hospitalinzet za rufaa, Muhimbili, Mbeya na Buganfo. kCMC wanayo na Moi wanayo.
    Mwandshi missed the point kuwa CT-scan sio disposable, haitumiki kwa mgonjwa mmoja then kazi umeisha, inatmiwa na watu wengi wakati gari la mbunge ni yeye tu. Kumbuka inapoingia analipia 20% ya ushuru.

    ReplyDelete
  19. NASHINDWA KUIELEWA NCHI YETU HII YA TANZANIA,IWEJE WATU BINAFSI WANAANZISHA HOSPITALI NA WANASAIDIWA NA SERIKALI KWA KIASI CHA PESA KINACHOKUWA KAMA NUSU YA BAJETI YA WIZARA YA AFYA WAKATI HOSPITALI ZAKE HAZIJAWA NZURI NCHI NZIMA. KAMA WATU BINAFSI WAMESEMA WANAANZISHA HOSPITALI KWA SHERIA ZAO AMBAZO HAZIPINGANI NA SHERIA ZA NCHI NI SAWA TU, LAKINI SERIKALI ISITOE MIHELA KUWAPA HAO.VYA NCHI VINABAKI VYA WANANCHI WOTE, ZA TAASISI BINAFSI ZINABAKI ZA TAASISI BINAFSI. SASA HAPA WATANZANIA NDIPO WANASHINDWA KUWAELEWA WANAOTUONGOZAAAA.

    KWA ZILE HELA WANAZOTOA KILA MWAKA ZAIDI YA BILIONI 50, SERIKALI INGENUNUA CT SCANNER 20 KWA KUPELEKA HOSPITALI ZA MIKOA 20. HAFU SERIKALI INGEONGEZA HELA KWA AJILI YA KUNUNUA CT SCANNER KWA MIKOA ILIYOBAKIA, NA HELA YAKE HAITAZIDI BILIONI HAMSINI.

    MIYE SIJUI AKILI ZA WANAOTUONGOZA ZINATUPELEKA WAPI??? UZALENDO WA KWELI KWA UHALISIA KWA SASA HAKUNAAAAA. HAIWEZEKANI TUKARUHUSU MASLAHI YA WANANCHI YAKAPELEKWA KWA WATU BINAFSI AU TAASISI BINAFSI, NCHI INAKOKWENDA NI KUBAYA. WANANCHI WATACHOKA, MANAKE HAWAWEZI KUKAA NA DHULMA HII...

    NOTE: BWANA MICHUZI WEKA HIYO TAFADHALI WATU WAKUNE VICHWA NA WAWE WAZALENDO WAKWELI SIO MANENO TU LAKINI MOYONI WANAO UBINAFSI WA KUFILISI NCHI

    ReplyDelete
  20. kwa ufupi mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri alielewa main point ya madaktari

    TUNAWEKA MAIN PRIORITY KWENYE MATUMIZI AMBAYO HAYASAIDII WATANZANIA WENGI KWA UJUMLA TUNASAHAU SEKTA MUHIMU KAMA ZA AFYA

    ila kwa wale wenzetu wa kufuata propaganda wao ni kufuata mkumbo tu hata spelling watakosoa ili waonekane wana point

    ndio hao hao walioshangilia interns kufukuzwa na ndio hao hao wanaolia ooh huduma hospitalini ni mbaya wakitegemea hao madaktari wachache waliobaki sijui wawe robots..... NA BADO MTALIA SANAAAA!

    ReplyDelete
  21. Watanzania mnalipa kodi then mnatetea serikali kwamba hawawezi nunua CT Scan. Kama waliweza kununua radar for billions how comes wahawezi nunua ct scan? watanzania msipodai na kushupalia watawala wafanye yaliyo stahiki msahau kupata hizo very basic needs. Na we mwandishi unajionyesha kwamba unazijua hizo ct scan that's fine but hujatoa mchango wowte wa kuichallenge resikali kununua ct scan ili kuokoa maisha ya watanzania, ninyi ndo wale wale wabongo wengi waloelimika na kufanikiwa but very selfish and useless to the society ,only there kutetea politicians,shame

    ReplyDelete
  22. Jamani ndugu zangu dawa ni kuikimbia nchi tu mambo majuu tu .999 any time any where. Tutazozana tu sisi wa chini wabunge na mawaziri kutibiwa wao nje ya nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...