Tawi jipya la Benki ya CRDB Tabata jijini Dar es Salaam
Meneja wa tawi la CRDB Tabata, Hawa Sasya akiwa Ofisini kwake
Meneja wa Biashara za Kibenki, Burtony Mbogella
Ofisa wa Benki ya CRDB tawi la Tabata, Angel Kissanga akimuhudumia mteja
Meneja wa tawi la CRDB Tabata (wa tatu kushoto) akitoa maelekezo ya huduma mbalimbali za kibenki kwa baadhi ya wateja waliofika katika tawi hilo
Baadhi ya wateja wakipata huduma katika tawi la benki ya CRDB Tabata.
 
Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB, hatimaye imeamua kuwafikia Wakazi wa Tabata kwa kufungua tawi jipya eneo la Tabata Megengeni jijini Dar es Salaam.

Tawi hilo limeshaanza kufanyakazi tangu Julai 2 mwaka huu, ambapo limeonekana kuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Tabata na maeneo ya jirani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa tawi hilo, Hawa Sasya amesema kuwa wateja wa Tabata na maeneo ya jirani sasa wanaweza kupata huduma za kibenki katika tawi hilo.

Alifafanua kwamba, tangu kuanzishwa kwake tawi limekuwa ni mkombozi kwa wateja mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo na Makanisa, Misikiti na watu mbalimbali.

“Tawi lipo karibu na Kanisa la Kristo Mfalme, Tabata Magengeni, ambapo linatoa huduma mbalimbali zikiwemo za; Mashine ya kutoa na kuweka fedha (ATM) ambayo hufanyakazi kwa muda wa saa 24”alisema.

Alitaja huduma zingine kuwa ni pamoja na TemboCardVisa, Akaunti ya Hundi na ya watoto inayojulikana kama Junior Account pamoja na Akaunti ya Akiba.

Hata hivyo aliongeza kuwa, tawi hilo litakuwa likitoa Akaunti ya Tanzanite, na huduma za mikopo mbalimbali na huduma za bima.

Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake tawi limekuwa likitoa huduma ya kibenki kwa kutumia Simu ya mkononi (SimBanking), pamoja na Akaunti ya Wanafunzi ambayo inafahamika kama Scholar Account.

Meneja huyo aliwataka Wananchi na wateja wapya kutumia tawi hilo pekee katika eneo la Tabata ili kupata huduma za kibenki badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye matawi yaliyombali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Naipongeza sana benki ya CRDB kwa kuendelea kusogeza huduma zake karibu na wananchi. Mimi naikubali sana CRDB kwani ndio benki inayoongoza kwa mabadiliko ya msingi nchini.

    ReplyDelete
  2. Dah....nina furaha,,,,,,,,sana itaturahisishia muda.....

    ReplyDelete
  3. Umenichanganya, tawi lipo Tabata Magengeni au Jijini Dar, ni wapi hasa lilipo niende?!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...