Gari ya Abiria aina ya Isuzu Journey ikiteketea kwa moto mchana wa leo maeneo ya Buguruni Rozzana jijini Dar es salaam.Chanzo cha moto huo hakikujulikana mara moja na hakuna aliejeruhiwa wala kupoteza maisha katika ajali hii ya moto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Sasa ndugu zangu kama dash board haionyeshi chochote hata ukimuuliza dereva wa daladala gari ina mafuta kiasi gani anatoka na fimbo ya kupimia unategemea nini kama kuna shoti yoyote ni moto tu na watu nje ndo wanapiga kelele motooo mtooo ndo na dereva anasimama Tanzania tambarare

    ReplyDelete
  2. Naam, vipi huyu kalipa ile elfu 40 ya fire au vp? Kama kalipa hiyo huduma aliyolipia imemsaidia vp? Je waliolipia na watakaolipia baadae ikiwatokoe tatizo kama hili watanufaika vp kutokana na huduma waliyolipia? Mamlaka husika wanajiandaa vp kukabiliana na tatizo kama hili? Kuna fire engine ngapi Dar nzima na zipo kwa interval gani? Zabedayo msema kweli naomba majibu tafadhali,..... bila shaka hapo hiyo gari iliwaka mpaka moto ulipozimika wenyewe.

    Bongo tambarareeeeeeeeee, tupo sana huku kisiwani Ukerewe!

    Mdau UK.

    ReplyDelete
  3. Ziungue ili zipunguze msongamano wa magari mabovu barabarani

    ReplyDelete
  4. Kwa hali hii bora nifie ughaibuni

    ReplyDelete
  5. Sasa fire stika imesaidia hapo?TRA ninataka jibu!

    ReplyDelete
  6. Anon wa kwanza...

    Dashboard haioneshi 'shoti' ya umeme!

    Nami nilikuwa nasema hivyo hivyo yaani ah! Dili ya bima tu hiyo! mpaka Nissan spirit 3 door yangu ilipotaka ungua pale TAZARA aka pita fundi yuko pale karakana aka disconnect battery but it had already started to burn.

    Chanzo short circuit ya booster la music system.

    ReplyDelete
  7. Sasa watu wanalipishwa pesa kwa ajili ya gari ya zimamoto na sticker n.k. mbona hatuzioni hizo gari hapo??

    ReplyDelete
  8. Zebedayo hawezi kujibu hii.

    Zebedayo uje utembee Ughaibuni uone wenzetu walivyoendelea.

    Ughaibuni hakuna ujinga huu wa kuendesha gari mpaka unakaanga injini.

    ReplyDelete
  9. Weee zebe----zebedayo bahati yako ulikuwa haupo kwenye huo mkweche tungekuzika majivu tu. heee kwani nchi haina watu wa fire gari mpaka vyuma vinayayuka hamna mzimaji. bongo sirudi.wamrudishie elfu 40 zake walimtapeli eti za fire mijizi tu. by salum

    ReplyDelete
  10. Gari la fire lifuate nini. Tanzania ni nchi ya mwenye kisu ndiyo mla nyama. Lakini ipo siku.

    ReplyDelete
  11. Hii ndio Bongo bana, pesa za sticker ulaji wa WATU bana! kama veve bisha kuja uliza baada ya mwaka moja hakuna kitu dani ya A/c nasema hakya mama!

    ReplyDelete
  12. Mnaulizia fire stickers? alfu 40 walizochukua TRA wamepeleka wapi? wamepeleka ngurdoto muda ukifika wanaenda gawana, serikali dhalimu kwenye nchi ya watu dhabit.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...