WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI YA WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI,MH. ZITTO ZUBERI KABWE AKIWASILISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kanuni ya 99(7),toleo la mwaka 2007 na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,napenda kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mafungu ya Wizara ya fedha – Fungu 50 Wizara ya Fedha, Fungu 21 Hazina, Fungu 22 Deni la Taifa na Fungu 23 Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali. Vile vile Fungu 10 Tume ya Pamoja ya Fedha na Fungu 13 Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi.

Mheshimiwa Spika, mafungu yote yaliyo chini ya Wizara ya Fedha yanaomba kuidhinishiwa na Bunge lako tukufu jumla ya shilingi Bilioni 4,208 (trilioni 4.2) ili yaweze kutekeleza majukumu yake. Mafungu haya maombi yake ya Fedha ni sawa na asilimia 28 ya Bajeti nzima ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2012/13.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Fungu 13 kitengo cha udhibiti wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi

    hahahaha kweli mmarekani kiboko tutaendelea kumtumikia mmarekani mpaka siku parapanda italia

    kweli sisi waafrica ni kina kunta kinte mpaka mwisho.

    ReplyDelete
  2. Hii hotuba imetulia. Imejengwa kihoja na haonyeshi kuikandia Serikali bali inatoa mapendekezo kwa Serikali kutafakali na kuchukua yale yanayofaa kwa Mustakabari wa Taifa. Hii ndivyo inavyopaswa kuwa baina ya Vyama vya Upinzani kuchambua na kutuo upande mwingine wa jicho badala ya lile la Serikali kuliko tushuhudiavyo Mijadala Bungeni. Mijadala ya Masuala Nyeti Bungeni ifuate mlengo huu. Mhe. ZZK anaonyesha Ukomavu

    ReplyDelete
  3. Hivi hilo rungu la bunge ni la dhahabu au shaba? Limenunuliwa wapi na shilingi ngapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...