WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI YA WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI,MH. ZITTO ZUBERI KABWE AKIWASILISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kanuni ya 99(7),toleo la mwaka 2007 na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,napenda kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mafungu ya Wizara ya fedha – Fungu 50 Wizara ya Fedha, Fungu 21 Hazina, Fungu 22 Deni la Taifa na Fungu 23 Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali. Vile vile Fungu 10 Tume ya Pamoja ya Fedha na Fungu 13 Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi.
Mheshimiwa Spika, mafungu yote yaliyo chini ya Wizara ya Fedha yanaomba kuidhinishiwa na Bunge lako tukufu jumla ya shilingi Bilioni 4,208 (trilioni 4.2) ili yaweze kutekeleza majukumu yake. Mafungu haya maombi yake ya Fedha ni sawa na asilimia 28 ya Bajeti nzima ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2012/13.



Fungu 13 kitengo cha udhibiti wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi
ReplyDeletehahahaha kweli mmarekani kiboko tutaendelea kumtumikia mmarekani mpaka siku parapanda italia
kweli sisi waafrica ni kina kunta kinte mpaka mwisho.
Hii hotuba imetulia. Imejengwa kihoja na haonyeshi kuikandia Serikali bali inatoa mapendekezo kwa Serikali kutafakali na kuchukua yale yanayofaa kwa Mustakabari wa Taifa. Hii ndivyo inavyopaswa kuwa baina ya Vyama vya Upinzani kuchambua na kutuo upande mwingine wa jicho badala ya lile la Serikali kuliko tushuhudiavyo Mijadala Bungeni. Mijadala ya Masuala Nyeti Bungeni ifuate mlengo huu. Mhe. ZZK anaonyesha Ukomavu
ReplyDeleteHivi hilo rungu la bunge ni la dhahabu au shaba? Limenunuliwa wapi na shilingi ngapi?
ReplyDelete