Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya Viongozi na wananchi wa Kisiwa cha Pemba, katika Futari aliyowaandalia wananchi hao na kufuturu nao kwa pamoja katika Ukumbi wa Makonyo Chakechake Pemba jana.
Wake wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal (katikati) na Mama Asha Bilal (wa pili kulia) wakijumuika na wananchi katika hafla ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Rais iliyofanyika katika Ukumb wa Makonyo Chakechake Pemba jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wananchi wa Kisiwa cha Pemba, baada ya hafla fupi ya futari aliyowaandalia wananchi hao na kufuturu nao pamoja katika Ukumbi wa Makonyo Chakechake Pemba jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wananchi wa Kisiwa cha Pemba, baada ya hafla fupi ya futari aliyowaandalia wananchi hao na kufuturu nao pamoja katika Ukumbi wa Makonyo Chakechake Pemba jana.






Hizi pesa tunazotumia kufuturisha bora zingefanyia kitu kingine endelevu. Pesa hizo zingenunulia vitabu na vifaa vya kufundishia. Misaada na michango hiyo ingesambazwa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
ReplyDeleteWivu huo huyo anonymous wa kwanza! Wacha watu wale wakiwa wazima na michango watu wanatoa sana.
ReplyDeleteWadau, hivi ni lazima mtu au watu wanaofutarisha washiriki futari? Je, nikiwa mbali ninaweza kufutarisha watu bila mimi kuwepo? Kama wanaofutarisha wanashiriki futari, kwanini tusiseme kuwa makamo wa rais ashiriki futari na wananchi wa kisiwa cha Pemba? Au makamu wa rais afutarisha na kushiriki futari na wananchi wa Pemba?
ReplyDeleteAsiyejua maana.......
ReplyDeleteNaomba nieleweshwe: Hawa viongozi wanafutarisha kwa pesa ya serikali au pesa yao ya mfukoni?
ReplyDelete