Baadhi ya Mabalozi wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe wakati  akizungumza nao  katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya Mabalozi wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe wakati  akizungumza nao jana katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza masuala mbalimbali na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini jana katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam. Pichani ni Mhe. Balozi Juma Mpango (kushoto) wa Kongo DRC ambaye pia ni Kiongozi wa Mabalozi hapa nchini, na Balozi Rajab Gamaha (kulia),  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa waziri kuongea na mabalozi SI HABARI, habari tungependa kujulishwa kaongea nao nini? na siyo ule mwimbo wa kila siku wa waandishi wa habari kwamba "AKIZUNGUMZA MASUALA MBALIMBALI " Kujaza picha kama hizi hazitusaidii chochote sisi tunaotaka kujua habari kupitia blog hii

    ReplyDelete
  2. sawa kabisa mdau wa kwanza, kaongea nao nini? kuhusu kufuturisha au kwamba keshawahi kufika kwao?

    ReplyDelete
  3. Wadau wa kwanza na wa Pili hapo juu tuko pamoja kabisa!

    Suala ambalo ni la moto likiwa juu ya meza yake Mhe. Membe ni kuhusu msuguano wa Tanzania na Malawi juu ya Ziwa Nyasa.

    Malawi ni jogoo aliyewika usiku wa manane.

    Ni desturi yetu kuwa jogoo akiwika usiku ni dalili ya uchuro na hivyo itifaki inayofuata ni jogoo huyo kupigwa kisu kwa kuchinjwa alfajiri inayofuata kabla hakujakucha!

    ReplyDelete
  4. Malawi hakuna sababu kwa nini tusielekeze angalau majaribio ya nguvu zetu za Kijeshi huko!.

    Hawa Malawi ni kama wametupatia 'punching bag' kama mazoezi ya Ndondi ili tuweze kujifua Kijeshi kupitia kidomo domo chao.

    Ya nini tabu na fedheha kwa kudharauliwa na kujaribiwa wakati mabomu na Makombora yanatulipikia wenyewe Mbagala na Gongolamboto?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...