Msafara wa Matembezi ya hisani ukiongozwa na Brass Band ya JKT Makutupora kuelekea kanisa katoliki Dodoma kushiriki zoezi la changizo kwa ajili ya ujenzi wa jengo la makazi la watawa wa shirika la Mt. Gema wa Galgani jimbo Katoliki Dodoma. Msafara huo ulimuhusisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi, Askofu wa Jimbo Katoliki Dodoma Mhasham Gervas Nyaisonga watawa na wananchi wa kawaida.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (katikati walio mstari wa mbele) akishiriki zoezi la matembezi mapema leo hii wakati wa changizo kwa ajili ya ujenzi wa jengo la makazi la watawa wa shirika la Mt. Gema wa Galgani jimbo Katoliki Dodoma, kushoto kwake ni Askofu wa Jimbo Katoliki Dodoma Mhasham Gervas Nyaisonga na kulia kwake mkuu wa shirika hilo Sister Florence Mbeyu.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashsriki Mhe. Samuel Sitta ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye zoezi la harambee ya ujenzi wa jengo la makazi la watawa wa shirika la Mt. Gema wa Galgani jimbo Katoliki Dodoma akimsalimu kwa kumbusu Askofu mstaafu wa kanisa Katoliki jimbo hilo Mhasham Martias Isuja.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kushoto) akimkabidhi Askofu mstaafu wa kanisa Katoliki jimbo la Dodoma Mhasham Martias Isuja hati maalum ya upendo wa Kweli kutoka kwa shirika la Watawa la Mt. Gema wa Galgani jimbo Katoliki Dodoma, anayeshuhudia katikati ni mkuu wa shirika hilo Mtawa Florencia Mbeyu.
Baadhi ya akina mama wanaofaidika na huduma zinazotolewa na shirika la Mt. Gema wa Galgani jimbo Katoliki Dodoma waliohudhuria zoezi la changizo kwa ajili ya ujenzi wa jengo la makazi la watawa wa shirika hilo mapema leo hii katika viwanja vya kanisa Katoliki jimbo la Dodoma.
Baadhi ya watawa wa shirika la Mt. Gema wa Galgani jimbo Katoliki Dodoma wakiwa wamekaa mbele ya jengo la makazi la watawa wanalolijenga wakati zoezi la changizo kwa ajili ya ujenzi huo mapema leo hii katika viwanja vya kanisa Katoliki jimbo la Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mhe. Sitta duh! hapo umepiliza sasa. Halafu kina mama hao jamani mngewapa hata ndala wavae basi mbona wapo pekupeku?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...