Naibu katibu mkuu wa UVCCM Zanzibar, Jamal Kasim Ally akimkabithi fomu za kugombea nafasi ya uongozi wa UVCCM-NEC Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Bw Jerry Silaa jana katika ofisi za CCM mkoa mjini magharibi Zanzibar, (ktk) mwenye suti nyeusi ni Bw Abdallah Mwinyi-katibu wa vijana mkoa kusini unguja akishuhudia tukio hilo. UVCCM -NEC imetangaza nafasi zinazogomewa kua ni Mwenyekiti, Mkamu mwenyekiti, Katibu, wajumbe wa baraza kuu na wajumbe wa halmashauri.
Hata hivo mstahiki meya wa manispaa ya ilala alipohojiwa hakuweka wazi nafasi gani anayotaka kugombea kwani alikua bado anakusanya maoni na ushauri kutoka watanzania mbalimbali na kujipima mwenyewe ni nafasi ipi itakayo mfaa zaidi ili kuweza kuwatumukia wananchi vema.Tetesi kutoka kwa wadau wake wa karibu zinasema mstahiki meya anataka kugombea nafasi ya Mwenyekiti UVCCM-NEC.



biashara hiyo kila mtu sikuhizi anaitaka maana ina faida sana
ReplyDeletepoleni sana watanzania mliokuwa na hali ngumu A.k.a walalahoi jasho lenu linaliwa na wachache.
Hivi kuna nafasi hiyo Mwenyekiti UVCCM-NEC? Au ujumbe???????
ReplyDeleteHuyo anafaa ni kijana makini na mpenda maendeleo. Kwa hivyo watu wafanyeje? Wote wakauze machungwa au wote tulale hoi, kazi zisifanyike au kwa hivyo watu wafanyeje namuuliza ndugu yangu anon Sat Aug 04, 03:53:00 PM 2012, hayo maneno ya mkosaji kama unaipenda nchi yako toa mawazo ya maendeleo sio ya kuchochea chuki.
ReplyDeleteKaka songa mbele ktk kujenga chama Chetu.
ReplyDeletehe is a smart guy. real he deserve any post. BIG UP JERRY
ReplyDeleteImefika wakati hata wamiliki wa blog kuchuja maoni kuna maoni unayaona hayana nia njema zaidi ya kupandikiza chuki humu.....kama siasa tuifanye kwa masingi ya maendeleo.
ReplyDelete