Mwenyekiti wa Tume ya Mabdiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Jospeh Warioba, akiongea na Wawakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri waliofika ofisi za Tume jijini Dar es salaam jana (Jumanne, Agosti 14, 2012) kubadilishana mawazo. Kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa MCT, Bw. Kajubi Mukajanga. Kulia ni Katibu wa Tume Bw. Rashid Assaaa.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba (katikati) akimtambulisha Mwandishi wa Habari Mkongwe, Bw. Ahmed Rajab (wa pili kushoto) kwa Wajumbe wa Tume. Kulia ni makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na kushoto ni Mjumbe wa Tume, Dkt. salim Ahmed Salim (kushoto) na Katibu wa Tume, Bw. Rashid Assaa. Bw. Rajab alikutana na Wajumbe wa Tume kubadilishana mawazo katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana(Jumanne, Agosti 14, 2012).
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Bw. Neville Meena (kulia) akiongea katika mkutano wa kubadilishana mawazo na uongozi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana.
Waandishi wa Habari Wakongwe, Bi. Pili Mtambalike (kulia), Bw. Allan Lawa (katikati) na Bw. Suleiman Seif wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Jospeh Warioba, akiongea na Wawakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri waliofika ofisi za Tume jijini Dar es salaam jana.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kati ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Jospeh Warioba na Wawakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri waliofika ofisi za Tume jijini Dar es salaam jana.(Picha na Tume ya Katiba)


Huyu ndiye Ahmed Rajab mwenye chuki na Watanganyika?? Kwa kweli Mungu kamlaani kwa kumpa nywele za kipilipili. Ndiyo maana yuko frustrated.
ReplyDeleteAhmed Rajab mwenye chuki na Watanganyika?? ................
ReplyDeleteJe, ni yule aliyekuwa Mhariri wa gazeti la African Event (london) --gazeti la "Sultan wa Zanzibar" - Sayyid Sir Jamshid bin Abdullah Al Said?
Mwenye chuki na waTanganyika au MSEMA KWELI???!
ReplyDeleteAnonymous...wa kwanza inaonekana huyu Mwandishi anakukosesha raha. Mimi nadhani tatizo si kwamba yeye anachukia waTanganyika, bali unamchukia kwavile anafichua 'UDHALIMU' na 'UJANJA' wa kikoloni wa Tanganyika dhidi ya Zanzibar!
ReplyDeleteBravo Ahmed Rajab!
Hii ndiyo shida ya baadhi ya waafrika kama mimi . Huyu Ahmed Rajab inawezkana baadhi hawafurahishwi na anachokiandika lakini ukweli iku zot unaumma. Wanapoteza dira kwa kumhusisha na
ReplyDeleteUsultani. Ni vyema mkapata waifu wake kujua yeye ni nani hasa katika masuala ya pan africanism. Muulizeni Dr Salim Comrade mwenzake
walikuwa Umma party pamoja .
Kwa sababu tu anaitetea Zanzibar ameshakuwa msaliti . Mnajuwa kupotosha ukweli kama mnavyopotosha historia ya uhuru wa Tanganyika na mapinduzi ya Zanzibar. Haisangazi mliwataja Kamaliza, Kambona na Shaba raia na mkawakandamiza kina Fundikira na Takadiri waliopigania uhuru, kama mlivyopotoha kwamba Umma party haikushiriki mapinduzi. Si alikuwa Babu mjulisha Nyerere na Mao Tse Tung. Bila Babu Nyerere angeujuwa Ujamaa ? Kama Chuki basi ni Yenu nyinyi.Ukweli Unauma siku zote.
Kumbuka G55 i walitaka Tanganyika je wakitaka kumrudisha Muingereza ?