JOSIAH KIBIRA UNIVERSITY COLLEGE OF
TUMAINI UNIVERSITY MAKUMIRA
P.O.BOX 1023 BUKOBA, TANZANIA
30.07. 2012

MKUU WA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA JOSIAH KIBIRA (JoKUCo) CHA CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA ANAKARIBISHA MAOMBI YA:
(1) KUJIUNGA NA CHUO KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013 KWA KOZI YA STASHAHADA YA TEKIHAMA KATIKA MAWASILIANO (DIPLOMA IN INFORMATION TECHNOLOGY-DIPL. IT)
KWA WANAOOMBA KOZI HII FOMU ZINAPATIKANA KWENYE TOVUTI YA CHUO www.jokuco.ac.tz NA PIA KUTOKA OFISI YA MDAHILI, JoKUCo, P.O.BOX 1023, BUKOBA, TANZANIA
MWOMBAJI AWE NA SIFA ZIFUATAZO:
(A) KREDITI 3 (THREE CREDITS) AU PASI 5 KATIKA CHETI CHA KIDATO CHA NNE NA CHETI CHA KIDATO CHA SITA CHENYE UFAURU WA KUANZIA “PRINCIPLE PASS” MOJA NA “SUBSIDIARY PASS” MOJA. AIDHA, MWOMBAJI AWE AMEPATA “PASS” KATIKA HESABU AU FIZIKIA KATIKA CHETI CHA KIDATO CHA NNE AU “SUBSIDIARY PASS” YA HESABU AU FIZIKIA KATIKA KIDATO CHA SITA AU
(B) AWE NA CHETI CHA TEKINOLOJIA NA HABARI (INFORMATION TECHNOLOGY-IT) CHENYE “UPPER SECOND CLASS LEVEL” AU ZAIDI.
-FOMU ZA MAOMBI ZINAPATIKANA KWENYE TOVUTI YA CHUO www.jokuco.ac.tz na pia kutoka ofisi ya Mdahili, JoKUCo, P.O. Box 1023, Bukoba, Tanzania.
-MAOMBI YATUMWE KWA MDAHILI WA CHUO, JoKUCo, BOX 1023, BUKOBA,TANZANIA
-MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI TAREHE 17.08.2012.
(2) MAOMBI KWA AJILI YA WAHADHIRI KATIKA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA JOSIAH KIBIRA YANAKARIBISHWA. WAOMBAJI WAWE NA SHAHDA YA UZAMILI (YENYE WASTANI WA B+) AU UZAMIVU KWA AJILI YA KUFUNDISHA MASOMO YA UALIMU, HISTORIA, JIOGRAFIA, KISWAHILI, KIINGEREZA, KIFARANSA, TEKINOLOJIA NA HABARI, MAENDELEO, IMANI NA MAADILI. MAOMBI YATUMWE KWA MKUU WA CHUO, S.L.P 1023, BUKOBA.
MAOMBI YATUMWE NA VIVULI VYA VYETI PAMOJA NA C.V YA MWOMBAJI
-MWISHO WA KUTUMA MAOMBI HAYO NI 23.08.2012.
WAHADHIRI WA KUFUNDISHA MASOMO YA SAYANSI KWA MWAKA WA MASOMO UJAO, MAOMBI YAO YANAKARIBISHWA PIA. MWISHO WA KUTUMA MAOMBI YAO NI MACHI 2013.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri
k.n.y MKUU WA CHUO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Huyu Josiah Kibira ameachana na kutengeneza movies sasa ameanzisha University??

    ReplyDelete
  2. mtengenezaji film ni mtoto na huyu wa university ni marehemu Babake, alikuwa ni aksofu wa KKKT Bukoba

    ReplyDelete
  3. Kwa jina la Baba na roho mtakatifu ,si unajua nchi hii kanisa limeshika nafasi ya kila kitu,na hizo zingine zinazotumika,hata wewe ukishakuwa mchungaji utapeta,hata kama ulikuwa jambazi,hivyo ndio memorandom inavyosema,no ujanja ujanja ru,ili kanisa lishike hatamu,no system iliosetiwa kinamna,kaka usishangae,ndio mfumo kristo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...