Gari ya Naibu Waziri wa Afrika Mashariki likiwa limeanguma maeneo ya Tumbi Kibaha Mkoani Pwani huku umati wa watu ukiwa umefika ili kuokoa walikuwemo ndani ya Gari hiyo.kwa mujibu wa Mh. Abdallah anasema chanzo cha ajali hii ni lori lililokuwa linakuja mbele yako na dereva wake alikuwa akijaribu kulikwepa lori hilo na kwa bahati mbaya gari ikamshinda na kupinduka.
 gari hiyo baada ya kupinduka.
 Mmoja wa watu walikuwemo kwenye gari hiyo akitolewa baada ya kuanguka kwa gari hilo la Mh. Naibu Waziri wa Afrika Mashariki.
Naibu waziri wa Afrika Mashariki,Abdullah Juma Abdalla Saddallah amepata ajali jioni hii maeneo ya Tumbi Kibaha akitokea Bungeni kuelekea jijini Dar es Salaam.

Kufuatia ajali hiyo yeye na mkewe pamoja na watoto wake wawili wamenusurika ila dereva wake ndio ameumia vibaya na kukimbizwa hospital ya Tumbi-Kibaha kwa matibabu ya haraka.Picha na Mdau ABDULAZIZ

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Pole sana naibu waziri kwa ajali. Kama ulikuwa anatekeleza majuku yako ya kazi pole zaidi, lakini kama ulimtoroka Makinda kwenye vikao vya bunge na analalamika utoro, haya pole kidogo na usitoroke tena.

    ReplyDelete
  2. muschi b.c.August 08, 2012

    Mkuu ukirudi tu mjengoni nakuomba utoe hoja ya dharura Dr Maghufuli aongezewe kale kabajeti kake apanue ile road from Chalinze to Kimara haya malori hayatawabana tena. Pole sana mkuu!

    ReplyDelete
  3. POLE BROTHER ABDULLA PAMOJA NA FAMILIA YAKO YOTE,MUNGU ATAWAJAALIA AFYA NJEMA PAMOJA NA DEREVA WAKO.

    NDUGU YAKO.
    SUNDAY,USA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...