Mratibu wa kampeni ya Elimu yao Jukumu letu Rebeca Gyumi akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda jinsi harambee ya uchangiaji mabweni inavyoendeshwa na makusudio ya harambee hii. TEA inakusudia kuchangisha jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 2.3 zitakazotumika kujengea hosteli 30 katika mikoa minane nchini.
Mheshimiwa Deo Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa akitoa mchango wake kuchangia ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike kupitia kampeni ya Elimu yao Wajibu wetu, kampeni inayoendeshwa na mabalozi wa Mamlaka ya Elimu (TEA).
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii na Mbunge wa viti maalumu(CCM) Mh. Margreth Sitta akitoa mchango wake kwa TEA katika kuchangia harakati za Mamlaka ya Elimu Tanzania kuhakikisha wanafunzi wa kike wanakuwa na makazi salama.
Mheshimiwa Vicky Kamata (MB)(Katikati) akijaribu moja ya huduma ya kuchangia kampeni hii ya ujenzi wa mabweni kulia kwake ni Nancy Sumari Miss Tanzania 2005 na kulia kwake ni Faraja Nyalandu Miss Tanzania 2006 ambao ni mabalozi wa kampeni hii.
Mh. Sophia Simba Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na Watoto akitoa mchango wake kuchangia kampeni hii bungeni. Ili kuchangia pia unaweza kutuma neno CHANGIA TOFALI kwenda namba 15564 ambapo utakatwa shilingi 250 tu za kitanzania.
Mbunge wa Kilosa Mh. Mustapha Mkulo (MB) akitoa mchango wake kuchangia kampeni hii. Mabalozi wa harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za watoto wa kike waliamua kwenda bungeni kuwaomba wabunge wachangie kampeni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. TEA mna akili kweli...mmeamua kuwafuata wenye nazo. Hapo lazima watoe (ingawa kimoyo moyo watakuwa wanalaani)

    ReplyDelete
  2. TEA wamelenga sana!

    Kwenda Bungeni mmechagua, mkitoka Dodoma sasa ni Dar Ofisi hadi Ofisi za Idara Wizara na Mashirika kwa Mabosi wote nchini!

    Lazima mabinti walale ktk mabweni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...