Salam,
Urban Pulse Creative na Freddy Macha wanakuletea taswira ya Notting Hill Carnival iliyofanyika jana tarehe 27.8.12.
Kihistoria sherehe hii ilifanywa siku 40 kabla ya Pasaka kipindi kinachoitwa LENT ( “Kwaresima“ )ambapo waumini wa Kikristo hujinyima, husali, hutoa sadaka, huomba msamaha, huungama makosa , kuwa karibu na Mwenyezi Mungu kwa kufunga (kama wafanyavyo Wayahudi na pia Waislamu kabla ya Idd El Fitri). Carnival hushereherekewa kidesturi mwezi wa pili na watatu (Brazil, Ujerumani, nk) lakini nchi mbalimbali ( mathalan Uingereza, Japan, Cape Verde nk) zimegeuza tarehe kufuatana na tamaduni au matakwa yao. London ni Jumapili na Jumatatu ya mwisho wa mwezi Agosti ambapo hamna kazi (huitwa Bank Holiday).
Eeh hii kali!kuungama kwa Mwenyezi Mungu kwa kutembea uchi,,hii kweli wanamtendea Mungu haki au imekaaje hii?
ReplyDeleteHapo ni ngono tupu na uasherati hakuna lolote !! tusidanganyane hapa,nia yao kubwa hapo ni kuonyesha miili yao tu hao kina dada, mbona wanaume hawako uchi uchi namna hiyo ?? hata sikielewi kilichomo akilini mwa wanawake,hii tabia ya kukaa uchi uchi waliambiwa na nani ?? Zebedayo msema kweli
ReplyDeleteSijui ni mtazamo wangu au ni muonekano kwa ujumla, Mbona mavazi hayaendani na kuabudu mungu aliye hai, ambapo katika kupunguza tamaa za kimwili na kuzingatia maombi, waumini hupaswa kujisitiri vema.
ReplyDeleteHakuna uhusiano wowote kati ya Ukristo na hii picha.
ReplyDeleteAidha Kwaresma inaadhimishwa na Wakristo wakatoliki zaidi.
Wakristo wengine wanafanya uliyoyasema kila wakati, hatuna muda maalumu wa kufunga ama kutubu dhambi.
Weka picha tu, na usitaje habari ya Ukristo hapo, sisi ni wavumilivu, ingekuwa watu wa dini nyingine ofini yenu ingechomwa moto leo hi hi.
Darasa kidogo kwa mwanajamii.
ReplyDeleteKama una maana ya Mungu wetu wa Mbinguzi lazima uanze kuandika jina la Mungu kwa "M" ni LAZIMA ianze kwa herufi kubwa, ukiandika mungu yaani "m" ndogo wewe una maana ya miungu wanayoabudu wasioamini.
Sasa hao wana carnival kama Mungu wao anaitwa mungu basi kuwa uchi inawezekana lakini kama anaitwa Mungu basi wamepotea wanapaswa kukosolewa
Hizi ni DILI sio Dini,DINI ya ukweli ni moja tu na sisemi ni ipi bali hanagaika kutafuta utaigundua.
ReplyDeleteWala hatusikii tamaa ya ngono ovyo kwani tunaona 'a lot of flesh and curvy' siyo tu ktk Carnival bali summer yote.
ReplyDeleteMkaazi
Notting Hill
London W10
Hebu watanzania jielimisheni.. Hii carnival ni nini, na ina maana gani na inachezwa na nani. tutandelea mpaka lini kuwa wajinga namna hii. Hili ni somo peke yake na limefanyiwa uchunguzi na watu wameandika vitabu juu yake. Someni someni someni sio kukurupuka tu.
ReplyDeletewewe mkaaji wa Notting Hill wacha zako za kushinda beach kuangalia ngono,tumia wakati wako kwenda shule, halafu wewe unayetuambia tusome, anza wewe kwanza, ingawa inavyoonyesha,unasoma sana vitabu vya ( play boy) hapo sawa kabisa mdau maana elimu unayojifunza humo ,inaendana na hizo picha.Zebedayo msema kweli
ReplyDeleteZebedayo anapenda Kuchangia Mada za watu Walioko Ugaibuni tu na kuwamaliza..Sasa yeye ajiulizi Ngoma zetu za mila na desturi za Kitanzania tunazozitukuza wanavaa kama hivi na viuno vinatingishwa mbele ya wazazi wetu na watoto wetu mbona hatulalimiki...Alafu tunasisitizwa tufuate Mila zetu...Acheni Kasumba..Huku kuvaa hivyo kawaida tu kwasabu ngono is not a problem bado kama Bongo..Perverted mkubwa kweli weye
ReplyDeleteMdau namba moja hapo juu, hivi hujui kama ni sisi tulimlazimisha Mwenyezi Mungu kuvaa nguo, yeye alitaka tusivae nguo, unakumbuka hiyo au umesahau? na aliuliza "mmejificha mnasema mko uchi, nani kawaambie mko uchi au mmekula lile tunda nililo wakataza?"
ReplyDeleteKwahiyo hawa jamaa wako sawa kabisa, tena walipaswa kaacha hata hizo bikini walizo vaa.
Naiitwa, Xavery komba-Mbinga
Wasomaji mnaojiuliza maswali kwamba hii ni dini au si dini hamjakosea kuuliza. Ila kihistoria, asili au ilivyoanza maana yake ndiyo hiyo...ilifanywa siku arobaini kabla ya Pasaka. Kusheherekea kwa kila namna kabla ya kujinyima. Neno Carnival ndiyo asili yake. Carne (nyama) Vale (kwaheri)...Kwaheri nyama au kwa heri starehe na kula. Baada ya tafrija ya siku chache zama za enzi hizo walianza sasa kujinyima na kumwomba Mwenyezi Mungu awasamehe. Hiyo ndiyo maana na asili ya Carnival. Kuna nchi za Kiafrika (Msumbiji, Angola, Cape Verde nk) ambapo shughuli hii leo hufanywa. Kama inakinzana na imani fulani au hapana hilo ni suala jingine...lakini maana yake ndiyo hiyo wasomaji wapendwa mnaotaka kujifunza tamaduni mbalimbali ulimwenguni zikoje na zilianzaje.
ReplyDelete