Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini Accra leo Agosti 11, 2012 baada ya kumtembelea na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills aliyezikwa jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini Accra leo Agosti 11, 2012 wakati alipomtembelea kiongozi huyo mpya wa Ghana na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama manasi yakitayarishwa kwa ajili ya kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha Bomarts Farms Ltd. katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti 11, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa manasi yanayolimwa kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shmaba la Bomarts Farms Ltd. katika kijiji cha Dobrokatika eneo la Nsawam nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti 11, 2012. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya buluu ni Waziri wa Chakula na Kilimo Mhe Kwesi Ahwol.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia upandaji wa miche ya mananasi katika shamba la Koranco kijiji cha Obotweri nje kidogo ya jiji la Accra. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Koranco Farms Ltd. Bw Emmanuel B. Koranteng ambaye amekuwa akilima shamba la matunda kwa miaka 27. Mwalimu Nyerere aliwahi kumtembelea shambani hapo katikati ya miaka ya 1980 kujionea ukulima huo wa matunda.PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. UPANDAJI WA MANANASI KIWANGWA BAGAMOYO NIKAMA HUU NA YANAVUNWA KWAWINGI MNOO.
    BINAFSI NINASHAMBA HEKA HAMSINI HUKO. TATIZO HAKUNA MIPANGO MIZURI KTK UZAJI MANANASI MENGI YANAOZA BADO HAKUNA USAFIRISHAJI NJEE!

    ReplyDelete
  2. JAMAA KENDA KUJIFUNZA UKULIMA BORA WA MANANASI KWA AJILI YA SHAMBA LAKE AMBALO LIKO BAGAMOYO.

    ReplyDelete
  3. JK anajiuliza "hili nanasi mbona kama yale ya msoga?"

    ReplyDelete
  4. Mzee wa pamba tunaona kiatu hicho.

    ReplyDelete
  5. Raisi anashangaa nanasi. kwani kilimo kwanza mananasi hayamo

    ReplyDelete
  6. ALAAA KUMBE BASI NIKIRUDI NYUMBANI HATA OFISI SIENDI MOJA KWA MOJA MSOGA MARA UJUMBE WA GHANA UNAKUJA TEMBEA KUANGALI SOMO LIME PASI

    ReplyDelete
  7. Waulize soko liko wapi na wakulima wa kwetu waweze kufaidika.

    ReplyDelete
  8. WANDUGU......! SI VIZURI KABISA KUMDHIHAKI NA KUMFANYA KAMA KITUKO RAIS HALALI WA NCHI. HUU NI USHAURI WA BUREEE

    ReplyDelete
  9. Mananasi tunayo ya kutosha,omba watalaam wa zao la Kakao(KAKAO GHANA).Tujaribu zao la Kakao mikoa ya pwani,hali ya hewa kama Ghana.Ila kwa pamba tu,haushikiki mkuu.

    David V

    ReplyDelete
  10. Watu wamekosa heshima hata Rais wanamdhihaki!!!!!

    ReplyDelete
  11. WANANCHI HAMNA JEMA!!! IPO SIKU MTAMKUMBUKA.

    ReplyDelete
  12. Hivi uhuru wa kujieleza maana yake ni kila kitu kukidhihaki kwa vile kimefanywa na chama tawala hata kama ni kizuri? Wabongo wenzangu hamuoni aibu kila wakati kuendelea kumdharau Rais wetu wakati nchi za nje zinamheshimu. Binadamu yeyote hakosi kasoro lakini sisi tumezidi kwa dharau. Ngoja chama kingine kiingie madarakani tuone kama mtaweza kuendeleza dharau zenu hizo bila kushughulikiwa ipasavyo. Nasema tena - uzuri wa kiongozi huonekana baada ya kutoka madarakani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...