Unko Michuzi
Naomba usinibanie hii,
Wakati nasafiri kuelekea nje nimeona kuwa watu wote wenye passport zisizokuwa za Tanzania wanatozwa DOLA 10 kila mmoja huku wakionyeshwa barua iliobandikwa kwenye desk kuwa BUNGE limekaa na kuamua Kuongeza Ushuru wa kutumia uwanja wa ndege kutoka Dola 30 mpaka Dola 40. 

Cha kushangaza nikwamba ukilipa hiyo dola 10 hupewi risiti ila ticket yako inagongwa muhuri unaosema KALIPA. sasa HUU SI WIZI WA MCHANA MCHANA ukiuiliza unaambiwa kaulize TRA hawajatupa RISITI. Halafu cha ajabu zaidi ni lazima ilipwe kwa DOLA hawapokei shilingi. JAMANI HUU SI WIZI MAANA HUU MUHURI USIOISHA NA HESABU ZISIZOKUWA NA RISITI WALA DAFTARI..tunaibiwa maana ninavyojua mimi ukinunua ticket inajumuisha na makato ya uwanja wa ndege. 
Kama bunge limepitisha si vibaya lakini kwanini wasitoe risiti tukajua kuwa hizo kumi kumi wanazokusanya zinaingia serikalini na si kwenye mifuko ya wajanja......
Ndimi Mdau Yangu Macho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Hii ndiyo bongo yetu bwana. Unalipa keshi na hakuna risiti na hakuna wa kumuuliza. Tunashindwa kusimamia mapato yetu lakini tunaweza kwenda nje kuomba misaada kwa ajili ya bajeti ya kila mwaka.

    ReplyDelete
  2. aaaaahhh acha nicheke kwanza!hivi bado wanatoza!!??kama ni mapato lazima tujue wameingiza kiasi gani kwa sababu hii ilinikumba mwaka 2009 nikagoma kulipa na nikawaambia hiyo kodi waweke pamoja na tiketi au kuwaonya abiria pindi wakatapo tiketi za nje nikapita kiraini.Naomba wahusika wafanye uchungu,kama ni mapato basi yanaweza kusaidia kwenye bajeti za serikali.kumbe serikali ina njia nyingi za kukusanya kodi lakini pesa zinaishia mifukoni mwa wachache,fikiria abiria wangapi wanasafiri kwenda nje ambao si waTZ,na hiyo dola 10 ipo toka 2009.Kwanza ni aibu kudai tozo bila kichwa wala miguu halafu bado unaitwa uwanja wa ndege wa kimataifa.

    ReplyDelete
  3. kuna haja ya wahusika kuliangalia hili na kuchukua hatua sahihi.

    ReplyDelete
  4. Naam, wana njaa kali sana hapo uwanaja wa ndege, nilishuka hapo 2009 kupata pen tu ili nijaze form ilikuwa kazi nilitamani nifanye U-turn.

    Nitaanza kuacha kuangalia hizi blog na magazeti ya Bongo muda si mrefu maana kila nikiingia humu nitakuta taarifa inayonitia hasira ama kunitia majonzi. Kwaherini wadau nimechoka.

    Mdau UK.

    ReplyDelete
  5. Mie juzi tu hapa wamenitoza hiyo dola kumi ingawa nina passport yangu ya kibongo, eti wanadai ni ushuru mpya wa airport, tumebishana kwelikweli wakagoma kunipa boarding pass mpaka nilipe hiyo pesa, muda wa kuondoka ukawa unafika wakasema wao hawajali hata nikiachwa na ndege kwakuwa wametumwa na wakubwa wao, finally nililipa lakini kwa hasira kubwa. Lakini niilifidia kiaina, nilikuwa na excess luggage kilo 19, wakaniomba rushwa nikawapa Danish Kroner 50 ya zamani, wenyewe wakaamini ni hela nyiiiiiiiingi, kumbe si chochote, watakoma watakapoenda kui-change!

    ReplyDelete
  6. Ndugu yangu aibu kwa sisi wageni tusiokuwa wabongo tukishuka tunalipa dola 100 na hakuna risiti...Kuna mtu kavaa magwanda anakufuata nje unampa dola yako na pasipoti wewe unasimama pembeni unawaza kwamba ndio umeingizwa tauni au ndio ulaji wa mtu hapo eapoti...Ni aibu kwa wageni na sisi tunaoambiwa nyumbani kuzuri turudi kusukuma gurudumu la maendeleo!

    ReplyDelete
  7. aisee hata mimi leo Zebedayo msema kweli, swala hili limeniingia -kumbe kuna ushenzi na ushetani wa namna hii hapo Airport ???? Jamani msiogope kurudi, sasa hao ,dawa yao anayo Dr Harrison, watakoma ubishi,hii wala isiwape homa na kususia kusoma blog ya michuzi,Michuzi hahusiki na hizi dola 10, 10 ni hao manyan'gau wa hapo uwanjani. na tunapowaumbua namna hii ndo dawa ,siyo kususa. Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  8. Wapo wapi wale wala vumbi wanaosema "eeeh bana bongo tambarareeeeeeeeee leooo........!!!!"

    Wameniingiza mkenge nikaamini kwamba bongo siku hizi fresh, nilipofika bongo tuu baada ya kukaa ughaibuni miongo kadhaa, kwanza nikakuta bomba la maji, nikafungua lakini hayatoki maji.

    Nikawapigia simu emirates airline air kufupisha likizo yangu.

    Bwieni peke yenu umbi lenu.

    Bora uishi Lagos kuliko bongo.

    ReplyDelete
  9. Msilalamike ni kodi ya kununulia ndege mpya 2 za ATCL(Utani).Kuna dada nilikorofishana naye kwenye ile ndege ya alfajiri ya kwenda Nairobi kwa sababu ya hiyo dola 10.Lakini baadae ugomvi ukaisha,tukapeana na anuani za barua pepe.

    David V

    ReplyDelete
  10. Kwakweli hapa huwa tunapiga makelele lakini hakuna kinachofanyika hili swala na mimi nimelisikia kwa mke wangu alikuwa tanzania juzi amerudi nchi inatia hasira sio siri texi yeyote inatakiwa iwe pamoja na tikert yako sasa jamani kama unastukizwa inakuwaje na halafu kama unalipa kitu hakuna risit hii pesa inakwenda wapi?sababu kama risiti hazijatengenezwa basi inamaana hiki kitu hakijaaamuliwa mpaka kutengenezewa malipo!huyu kikwete na wahusika wako wapi jamani mbona watu wanaonewa sana hii nchi bila kuwekewa vitu kwenye system?

    ReplyDelete
  11. JAMANI MIMI NIMEPITA HAPO MARA NYINGI SANA NA SIJAWAHI KUTOA WALA KUULIZWA KITU KAMA HICHO,NA PIA KODI YA UWANJA HAIPO,KANAKWAMBA KILA ABIRIA ALIPE HIO KITU HAIPO DUNIANI WEWE KAMA UNATOA HIO DOLA KUMI BASI UMEINGIZWA MJINI.

    ReplyDelete
  12. ha ha! Naimagine emirate airbus 320 yenye kujaza abiria 300 halafu yoote hiyo inaingia mfukoni!! Mahekalu yasijengwe kwa nini?

    ReplyDelete
  13. Hata mimi waliniomba hiyo hela mwezi uliopita tu,nikawaambia hivu huu ndio utaratibu gani, kwa nini hii pesa isijumuishwe katika tiketi eti wanasema ilishatangazwa kwenye vyombo vya habari na imepit. nikawauliza tena hivi hawajui kama wapo huqa wakipita airport hawana hata senti, na pengine wanasafirishwa tu sasa itakuwaje na mkiwazuia,wanakwambia hiyo sio issue yao. nikakubali kulipa nikawaambia lakini naomba mnipatie risiti ili nikamdai muajiri wangu maana si mara ya kwanza kupita hapa sasa nikimwambia namdai dola kumi bila uthibitisho hatonielewa. Basi mara huyo mhudumu kamnong'oneza mwenzake wananambia wewe ulishalipiwa kwenye tiketi. Jamani hivi mambo haya mpaka lini Tanzania. Tunadharaulika hivo.

    ReplyDelete
  14. Inatia hasira na kusikitisha, nilikua narudi UK mwezi huu wa nane, nilidaiwa hiyo dola kumbi kwa nguvu zote, niliwaeleza sina pesa, walijibu tafuta mwenye m pesa atume, ilinishangaza kulipia kwa m-pesa, baada ya kubishana sana ilibidi niombe pesa kwa ndugu zangu waliokua nje, nililipa shs 16elfu ila nilipewa risiti, utaratibu mbovu wa kulipisha

    ReplyDelete
  15. Matatizo kama haya ya kidhalilisha nchi yetu yapelekwe kunako husika. Na hata waandishi wa habari huwa hawasomi Michuzi.Ila kama kweli kuna kiongozi wa ngazi ya juu anayekusanya hizo hela bila kutoa risit analiletea aibu taifa kwa faida ya tumbo lake au matumbo yao maana wakati mwingine anakuwa si mmoja.Watanzania tunajulikana kwa kulalamika bila kuchukua hatua.Mimi napendekeza kwamba bwana michuzi katika kuboresha blog yako tunaomba umtafute mwandishi wa habari aorodheshe malalamiko yetu.Swala siyo kulipia mbona huku ugaibuni tunalipia ma road toll kila siku? Swala ni kutolewa kwa risit.Nimetoka huko juzi, nilichojifunza nikwamba siku hizi TZ kila mtu ana avoid evidence hahahahh....

    ReplyDelete
  16. Yaani ukifika uwanja wa ndege ni tafrani tupu,kila mfanyakazi wa hapo ni njaa tupu,wamekaa na kukodoa macho na kuwaza pesa tu!kuanzia wafanyakazi wa chini hadi wa ngazi za juu,sijui wanafikiri wasafiri wana magunia ya pesa?Ni Rushwa tu inanuka uwanja wa ndege kuanzia wabeba mizigo,wasukuma matoroli,uhamiaji,ushuru n.k!Tumechoshwa na bongo ni bora tuishi huku huku nchi zilizoendelea wenye system ya maisha.

    ReplyDelete
  17. JAMANI HAKUNA ANAYESAFIRI NA CAMERA? MPIGENI PICHA ANAYEKUSANYA HIZO DOLA KUMI HALAFU TUMUWEKE KWENYE VYOMBO YA HABARI WAHUSIKA WATUAMBIE JE HII NI HAKI? HII TABIA WAMEIGA NIGERIA IPO SANA ILA MARA NYINGI WANAOFANYA HIVI NIGERIA SIO WAFANYAKAZI WA EAPOTI NI MATAPELI TU. RAFIKI YANGU MMOJA ALIKUMBWA NA HAYO HUKU NIGERIA BAHATI ALIKUWA NA UN PASS ALIPOITOA TU ILE YA KIBLUU JAMAA AKAKIMBIA KAMA MWIZI.

    ReplyDelete
  18. Airport Dar Tanzania inatumiwa kama SACCOS na wezi wakishirikiana na Mabosi wa Kibongo.

    Kama ni mimi silipi nipo radhi nisafiri kwa basi hadi Kenya au Kia niaanze safari huko.

    Ufisadi tuukatae kuanzia ngazi za chini za US$ 10 hizi!

    ReplyDelete
  19. HUO NI WIZI MCHANA KWEUPE!!!

    ReplyDelete
  20. wahusika wenyewe ndio walaji amna yoyote atakayeweza kuliangalia hili swala na kulichukulia hatua sahihi.

    ReplyDelete
  21. Kodi ya nini,wafanyakazi wa hapo airport sasa,choka mbaya wanaomba hao,weka begi tusearch lo ! tuachie basi change ,na hilo wigi hee

    ReplyDelete
  22. Wengi hutoa hoja zisizokuwa na "utafutaji wa suluhisho" Hapa tunahitaji watu kama huyu bwana hapo juu Projestus ambae anashauri nini cha kufanya ili kujiepusha na kero. Haitakuwa ni busara just kulalamika kila siku bila kutoa ushauri wa jinsi gani ya kutatua tatizo.Jamii hurudi nyuma pindi watu wake wanapolalamika bila KUSHAURI NINI CHA KUFANYA. Tusidanganyane na zile kauli za kwamba "HATA NIKISHAURI HAKUNA ATAENISIKILIZA"
    Mwisho napenda tena kucomment kuhusi msema kweli Zebedayo ambaye sifichi kusema kuwa ni mtu ambae anachukia sana wale wanaotoa hoja wakijionesha kuwa wapo ughaibuni.Ingawa this time kawa cool lakini haachi ule ubaguzi wake na chuki zake kwa watanzania tunaoishi ughaibuni Bado narudi tena leo na maelezo niliyioyawahi kuyatoa hapo siku za nyuma, kuhusiana na comment anazozotoa Zebedayo. Mimi naamini huyu bwana ana chuki na fikra yoyote ya ughaibuni na nasema tena kama aliwahi kuishi ughaibuni na akapigwa patrieshen asiweke chukikwa wale wanaoishi ughaibuni

    ReplyDelete
  23. UMUHIMU WA CAMERA KTK SEHEMU NYETI:

    Pana umuhimu wa sasa kufunga 'Surveilance Camera' kwa siri katika sehemu zote nyati za huduma halafu link mojawapo inamfikia direct Mkuu wa nchi ndg. Mhe. JK ili awe anashuhudia wezi wanavyofanya !

    SEHEMU ZA KUFUNGWA CAMERA HIZI:
    -BENKI KUU
    -TRA NA IDARA ZOTE ZA MAKUSANYO
    -BANDARI
    -AIR PORT ZOTE KUU
    -MIGODI MIKUU YOTE YA MADINI
    -MBUGA ZA WANYAMA HASA VIWANJA VYAKE VIDOGO VYA NDEGE
    -VIWANDA VIKUU
    -MITAMBO MIPYA YA GESI NA MAFUTA
    -MASOKO YA HISA

    Na sehemu zinginezo kwenye mitiririko zaidi.

    Ni jambo la fedheha sana wakati Raisi wa nchi anahangaika kujenga Uchumi wa nchi wengine wanabomoa, mfano hao wakusanyaji wanaleta madhara haya hapa chini makubwa:

    1.WANATUONDOA KTK DIRA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKI NA KUTUONDOA KTK USHINDANI NA MAJIRANI ZETU KTK ENEO LA EAC.

    2.WANAUA UWEKEZAJI NA KUWAFANYA WAGENI WA NJE NA WAWEKEZAJI KUIKWEPA TANZANIA KWA MAMBO YASIYO YA TARATIBU SAHIHI.

    3.WANATUKOSESHA MAPATO YA UTALII NCHINI KWA KUWAFANYA WATALII WASIICHAGUE TENA TANZANIA KUJA KUTEMBELEA NA PIA WATAKWENDA KUITANGAZA VIBAYA NCHI KWA KUCHAFUKA KWA WIZI NA RUSHWA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...