Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Paul Kagame wa Rwanda(kushoto),Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda(Watatu kulia) na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wakiwa katika mkutano wa viongozi wan chi za Maziwa Makuu unaofanyika jijini Kampala Uganda leo jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakifurahia  jambo wakati wa mkutano wa Viongozi wa nchi za Maziwa Makuu unaofanyika jijini Kampala Uganda. Picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. JK .Enhe Kijana kuna tetesi za chinichini eti una ajenda ya siri na huyu jamaa eti kuhusu DRC hebu tuambizane bwana sote si wajua majirani?

    Kgm. Leka aliko nibhisanzwe bizashira tulavyifashamwo ga.

    JKbl. Teh teh teh teh

    ReplyDelete
  2. hahahaha Museven na kofia yake!

    ReplyDelete
  3. No its M7 who is loughing teh-teh-teh.

    Our leaders when away from their electorate they are trying to portray unity and harmony.

    Its so nice to see this.

    lol

    Richard.

    ReplyDelete
  4. Jk...jamani wenzangu yani katika wote hapa mimi ndio karibia nitamaliza muda wangu wa uraisi lakini nyie wote mnaongoza tokea kabla yangu na mtaendelea mpaka baada ya mimi



    Wote kwa pamoja kwikwikwikwi unajuwa kuongoza afrika ni lazima utumie maguvu hata wewe ukitaka lianzishe tutakupiga tafu kwikwikwikwikwi

    ReplyDelete
  5. MIKUTANO KILA MARA HAKUNA NA LA MAANA WANANCHI WA MASHARIKI YA CONGO DR,WANAKUFA KWA MAELFU SHIDA KUBWA KATIKA NCHI YAO SIJUI KWA NINI NCHI HIZI ZA MAZIWA MAKUU HAZIWEKI JESHI LAO AU NCHI ZA SADCC HAPA UNAONGELEWA UNAFIKI TU,WAKATI WATUI WANAKUFA CONGO,HAKUNA UBISHI KAGAME/MUSEVENI WANAHUSIKA ETI WANATAKA DR CONGO IGAWANYIKE KAMA SUDANI

    ReplyDelete
  6. Jamani kuacha utani, mimi huwa namfagilia sana Kagame. Nchi yake ni ndogo sana kwa size, lakini anayo mipango na mikakati mikubwa kuliko nchi yetu na ukubwa wake!

    Kwa waliokwishatembelea jiji la Kigali, ni msafi ajabu. Pia angalia mkakati wake wa kila mwanafunzi na laptop! IT ndiyo inaingia Rwanda kisawasawa mzee!

    Miaka mitano, kumi baadaye haka kanchi katakuwa mbali sana kwa nyanja zote. Ukiangalia kwenye list ya nchi ambazo zina mazingira mazuri ya kuwekeza Rwanda iko juu!

    Hongera Kagame, hongera sana. Watu wanakuona uko uko tu, na kamwili kembamba lakini baba..... mambo yako makubwa!

    ReplyDelete
  7. KAGAME waambie yale maneno uliyotoa kwenye hotuba yako kuhusu international community.

    ReplyDelete
  8. hapo wamwzidiwa kete na mmarekani wanashidwa hata pa kuanzia. uganda na rwanda wanawaibia congo madini kimya kimya wala haikuwa tatizo kubwa kwani unaambiwa huko huchimbi unazoa tu juu juu. sasa mmarekani kwa pupa na uroho kaingia na machine kubwakubwa kachimba mpaka kakutana chini kwachini na mchina anayechimba kutokea zambia. kwa sababu mmarekani yuko ndani ya congo anaanzisha vita ya wenyewe kwa wenyewe (nchi majirani)ili aibe madini zaidi. hivi huyu mmarekani anataka dunia ya namna gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...