Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi amesema kuwa Viongozi wa Dini wanamchango mkubwa katika kufanikisha zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 26 mwaka huu.

Dr. Nchimbi aliyasema hayo leo hii kwenye ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Dodoma alipokutana na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kwa lengo la kuzungumzia ushiriki wa viongozi hao katika zoezi la Sensa ya watu na makazi ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika na kufanikiwa kama lilivyopangwa na serikali.

Dr. Nchimbi alisema kuwa viongozi wa dini wanadhamana kubwa katika nchi yetu kwa kuzingatia kuwa wanawakilisha au kuongoza jamii kubwa nyuma yao na kwa kuwa wao wanauelewa mpana wa suala la Sensa basi ni jambo la busara wakiwasaidia waumini wao pia kupata uelewa sahihi juu ya zoezi la Sensa. Aidha amewataka viongozi hao kwa dhamana walizonazo kwa Mwenyezi Mungu kuliombea Dua Taifa letu na Zoezi zima la Sensa kwani kwa kutoa ushirikiano kama huo zoezi hili litafanikiwa.

Dr. Nchimbi aliongeza kuwa anaamini viongozi hao wa dini ndio wataonesha mfano wa kusimama katika utiifu, uadilifu na unyenyekevu kwa Mungu wao kwa kuhakikisha zoezi la sense linafanyika vizuri. Akizungumzia kuhusu Sensa ya mwaka huu, Dr. Nchimbi alisema kuwa Sensa sio tu kuhesabu idadi ya watu bali ni pamoja na masuala mengine ya msingi kama idadi ya mifugo na shughuli nyinginezo.

Hii itasaidia mipango ya maendeleo na huduma muhimu kutolewa na serikali kulingana na mahitaji halisi, alibainisha Dr. Nchimbi na kuwataka wananchi wote watoe ushirikiano wakizingatia kuwa Sensa ni jukumu na wajibu wa kila mmoja hapa nchini na kuwa taarifa watakazotoa zitabaki kuwa siri na kutumika kwa matumizi yale tu yaliyopangwa kwenye Sensa.

Kwa upande wao viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini Mkoa wa Dodoma wamesema wako tayari kushirikiana na serikali katika kufanikisaha Sensa ya mwaka 2012. Akizungumza kwa niaba ya taasisi ya Dodoma Islamic Development Foundation, Katibu wa taasisi hiyo Alhaj Hussein Janab alisema kuwa viongozi wa dini wako tayari kushiriki zoezi la Sensa na pia wanafanya kazi ya kuhamasisha waamini na wafuasi wao.

Akizungumza kwa niaba ya kanisa la Mennonite Tanzania Kanda ya Kati Mchungaji Chacha Marwa wa kanisa hilo alisema kuwa viongozi wa dini wanawajibu wa kuisaidia serikali kwa kupeleka tarifa sahihi na za kueleweka zinazotolewa. Aliongeza kuwa serikali haina ubaguzi wa aina yeyote ile hivyo ni jukumu la viongozi wa dini nao kupinga aina yoyote ya ubaguzi au kiashiria chochote cha kuleta ubaguzi hasa kwenye mazoezi makubwa kam hili la Sensa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. WAISLAMU HAWATOSHIRIKI MPAKA MADAI YALIYOWEKWA NA WANAZUONI WETU YAMETEKELEZWA, KUTOKANA NA SHURA ILIYOKAA DODOMA NA KUTOA TAMKO. HATUTAKI HADAA, UKWELI NI MUHIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA VINGINEVYO HAKUNA MAENDELEO YEYOTE KATIKA NCHI AMBAYO INADHULUMU RAIA WAKE KWA MAKUSUDI.

    MASWALI HAYA YAJIBIWE NA WATENDAJI WALIOPEWA WADHIFA KUWAONGOZA WANANCHI:
    1. 1957 SERIKALI YA MKOLONI ILIHISABU KWA KUWEKA PIA KIPENGELE CHA DINI, MADHARA GANI YAMETOKEA?

    2. ILE SENSA YA 1967 AMBAPO KIPENGELE CHA DINI KILIWEKWA MATOEKO YAKE YAKO WAPI? NA MADHARA GANI YAMETOKEA???

    3. GHARAMA YA KUWEKA SENTENSI YA KIPENGELE CHA DINI NI SHILINGI NGAPI??? ILI WATANZANIA WACHANGIO HIYO HELA AMBAYO SERIKALI HAIWEZI KULIPA HATA KAMA TUNALIPA KODI, TULIPIE TU KWA MARA YA PILI KWA SABABU INAONEKANA WATANZANIA BADO HATUJAWA HURU.

    TUNAHITAJI SERIKALI YENYE KUWAJIBIKA, NA SIO KULETA HADAA KAMA ILE YA KWA BABU LOLIONDO AMBAPO IMESABABISHA WATU WENGI KUPOTEZA MAISHA. WALIOSABABISHA NI WATENDAJI HAWA HAWA BILA KUSUBIRI MATOKEO YA WATAALAMU WAKASHABIKIA NA KUWAHAMASISHA WANANCHI WAENDE. UNATEGEMEA MWANANCHI ATA REACT VIPI ENDAPO WAZIRI TENA OFISI YA RAISI ANASEMA DAWA NI KABAMBE??? SI ATASEMA KWELI INATIBU KWA KUWA MTU MWENYE DHAMANA YA WANANCHI KASEMA DAWA IKO SAWA KUTUMIKA NA INATIBU.

    MFUMO KRISTO NDIYO MKOLONI MWENYEWE, KWA KUWA HAWAKO KWA MASLAHI YA TANZANIA, YANI WANASEMA KANISA KWANZA TANZANIA BAADAE. KWA HIYO LIKIJA LA SERIKALI NA LIKIJA LA KANISA KWA PAMOJA, LA KANISA LITASHUGHULIKIWA KWANZA KWA GHARAMA YA YEYOTE HARAFU LA SERIKALI LITASHUGHULIKIWA HATA KAMA MIAKA YA MBELE IJAYO. HUO NDIYO MFUMO KRISTO, WATANZANIA WAPENDA HAKI WANA KAZI YA KUPAMBANA NAO KAMA WALIVYO PAMBANA NA MKOLONI KUDAI UHURU KWA KUWA NDIYO MKOLONI MWENYEWE.

    BWANA MICHUZI UNAWEZA KUIBANA MESEJI LAKINI WANASEMAGA MESSAGE SENT, HATA KWA WEWE ULIYESOMA PEKE YAKO YATOSHA.

    ReplyDelete
  2. Tuko pamoja mdau waislam tunaojielewa hakuna kuhesabiwa mpaka kieleweke...mfumo kristo utaondoka kweny nchi hii siku si nyingi....

    ReplyDelete
  3. NINAMUUNGA MKONO ALIE TOA MAONI WAKWANZA HAPO KUWA WAISLAM HATUTOFANYA SENSA.
    KWANI KUNAWATU WANAOA TAKWIMU KUWA WAISLAM NIKIDOGO KULIKO WAKRISTO.
    1:KIWEKWE KIPENGELE CHA DINI AU HAWA WANAO TOA TAKWIMU WAKATAZWEN WASITOE HIZO TAKWIMU KWANI HATUJUI WALIKO ZIPATA AKIWA WATU HAWAISABIWI KUZINGATIA KIPENGELE CHA DINI.

    ReplyDelete
  4. mmeshupalia dini badala ya kufikiria tutajikwamua vipi kutoka na huu umaskini tulio nao, wenzenu wanapaa nyie mnawaza dini, ooh tunaonewa mfumo ukristo bla bla mwisho wa siku wote tuna lala gizani, komaeni jinsi ya kuwaondoa mafisadi badala ya kupiga kelele dini hii, dini ile. mna kazi sana nyinyi watu.

    ReplyDelete
  5. Huo ndio msimamo wa waislam wenye nia ya kutaka usawa kwa kila mtanzania,tunaona jinsi gani wasio katika sisi wakipinga na kushangaa kwanini tunataka kipengele cha dini kiwekwe katika dodoso la sensa,takwimu za uongo zilizotolewa na tbc1 zinadhihirisha jinsi gani wasio katika sisi wanavyotwaalia nafasi katika nyanja mbalimbali za uongozi kwa kigezo kuwa wao ni wengi,wito kwa waislam wote tz tusikubali kuhesabiwa mpaka matakwa yetu yawe yametimizwa kikamilifu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...