Chama cha Watanzania Ufaransa (CCWU) kilituma salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki kufuatia vifo vya Watanzania vilivyotokea wakati meli MV SKAGIT ilipopata ajali tarehe 18/07/2012. 

Kwa bahati mbaya sana ujumbe wa rambirambi uliambatanishwna picha ya Watanzania wakiwa katika tukio ambalo halikuwa na uhusiano na salamu hizo za rambirambi na kwa ajili hiyo ikaleta hisia mbaya kwa wasomaji. 


Kuweko kwa picha hiyo hakukufanyika kwa kukusudia bali ni kosa la kibinadamu. Chama kimeona ni vema kuandika ujumbe huu ili kusahihisha kosa hilo na kuwataka radhi ndugu zetu.

Asanteni.
CCWU Ufaransa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nanyie mmekosa la kusema tu, hayo yamepita and life goes on, wengi wetu hatukuona kasoro kwenye hiyo picha ,of course kuna wengine walikosoa ,kama ilivyokawaida yetu sisi wanaadamu. wanasema , if you want to please everybody, you will please none. laiti kama ningelikijua kifaransa basi ningelikikoroga hapa-bonjour madam, oui . Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  2. Nassor A.SAugust 05, 2012

    Kweli, hata comments za wadau zilionesha kutoridhika na picha ile, lakini kama ni kosa la kibinaadamu na mumeomba radhi, basi kwa utamaduni wetu watanzania hatuna budi kuwaelewa.

    Kazi njema, ila musisahau kwenu hadi mukakukumbuka siku za majanga tu.

    ReplyDelete
  3. Ahsanteni Ufaransa!

    Uungwana ni vitendo.

    Tumewakubalia.

    ReplyDelete
  4. kukiri kosa ni uungwana na wala si udhaifu..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...