Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dr. Teresa Hovisa (kushoto) akipata maelezo ya kitaalamu juu ya Uchorongaji miamba kutoka kwa Bw. Mzee Kange ambaye ni Mtaalamu wa Miamba wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Nane Nane jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dr. Teresa Hovisa (kushoto) akipatiwa maelezo ya kitaalamu na Mkurugenzi Msaidizi wa Wakala wa Huduma za Misitu na Nyuki Tanzania Bi. Gladness Mkamba juu ya ufugaji nyuki alipo tembelea Maonesho ya Nane Nane jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dr. Teresa Hovisa (kushoto) akipata maelezo ya kitaalamu juu ya uendelezaji wa Mji wa Dodoma kutoka kwa Bw. Edward Mpanda mtaala wa mipango miji kutoka Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) wakati alipotembelea Maonesho ya Nane Nane jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dr. Teresa Hovisa (kulia) akimskiliza kwa makini Bi. Nobuko Nzulunge (kushoto) ambaye ni mjasiriamali kutoka Manispaa ya Dodoma anayezaliza bidhaa zitokanazo na Ubuyu wakati alipotembelea Maonesho ya Nane Nane jana, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Christopher Kangoye.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. wakubwa mliyoko majuu, angalieni kwa uzuri hiyo picha ya mwisho ya huyu mama mjasiliamali nahisi anatokea Mongolia,kaja bongo miaka nenda rudi na anachokifanya ndiyo hicho,bidhaa zinazotokana na UBUYU !!! narudia UBUYU. je ?? kwani sisi wazawa hatukuuona UBUYU ?? kuna mambo kadhaa katika maisha lazima tuyafuate (1) kuvumilia (subira)(2) jitihada. Tabia ya kukimbilia nchi za wenzetu kutafuta kazi,huo siyo uzalendo.Hapa hapa together we can do it. zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  2. wewe Zebedayo naona unabwabwaja mpaka povu la mdomo linakutoka. Hebu niambie wewe uliyekuwa huko mbona hukuuwaza huo ubuyu kila siku unaambiwa maisha ni popote pale na nyumbani ni pale mtu anapoamua kuweka makazi yake yeye na familia yake. Hata hapa Marekani wote ni wahamiji ambao vizazi vyao vilihamia kutoka mabara mbalimbali, kwani wewe unakerwa na kitu gani watu wakiamua kukaa ughaibuni? hebu ishi maisha kwa raha zako zote acha kuwaza maisha ya waishio ughaibuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...