Kundi la Simba likiwa limepumzika chini ya mti katika mbuga ya Hifadhi ya Taifa ya Wanyama ya Serengeti ambayo hivi sasa ina wageni wengi kwa kuwa ni msimu wa kutembelea mbugani, japo nyumbu wengi wako nchi jirani kwa mapumziko yao ya miezi miwili kila mwaka kabla ya kurejea tena nyumbani mnamo mwezi wa Oktoba katika kile kiitwacho the Great Animal migration
![]() |
Juu mtini kuna simba mwingine kajiopumzisha kwenye tawi |
Aghalabu simba wapanda miti huonekana sehemu za Hifadhi ya Manyara na hawa wa Serengeti wameonesha kuwa nao wanaweza kupanda miti bila matatizo
SHUKRANI NYINGI KWA ALIYELETA PICHA HIZI, JAMANI MIE NAPENDA SANA WANYAMA HASA KATIKA TASWIRA HII AMBAYO NI TAABU KUIONA UKIENDA MBUGANI, SI WOTE WENYE KWENDA HUKO WANABAHATIKA KUWAONA WANYAMA WOTE NA KATIKA MIKAO HIYO, AHSANTE TENA, ENDELEENI KUTULETEA VITU KAMA HIVI VYA NCHINI PETU ILI HATA KAMA HATUENDI WALIKO LAKINI TUNAJUA WAKOJE KATIKA PICHA.
ReplyDelete