Familia ya Bwana na Bibi Fredrick Kaduma wa Kimara-Dar-es-salaam,Tanzania na watanzania waishio Toronto,Canada wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao, Ritha Kaduma (Fatima) (pichani) kilichotokea hapo jana tarehe 9th August, 2012 huko Toronto,Canada.Fatuma au Rita amefikwa na mauti katika hospitali ya St.Michael’s ya Toronto alipokuwa amelazwa kwa muda mfupi.

Taratibu na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu alipokuwa akiishi na kaka yake huko huko Toronto,Canada.

Ukiwa kama mtanzania,ndugu,jamaa au rafiki,popote pale ulipo, unaombwa kuchangia fedha,hali na mali kwa ajili ya kuwezesha kuusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi mapema kadri iwezekanavyo kwani kama wengi wenu mnavyofahamu, mwili unavyozidi kukaa Funeral-Home,gharama ndivyo zinavyozidi kuongezeka.

Mwili utasafirishwa punde tu zitakapopatikana fedha za kutosha kwa ajili ya kulipia gharama husika. Gharama zimekadiriwa kufikia kiasi cha $24,000 ambazo zinajumuisha kuutayarisha mwili,kuutunza na kuuhifadhi na pia kuusafirisha mpaka nyumbani Tanzania.

Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account maalumu ya wafiwa kama ifuatavyo:

BANK : RBC (Royal Bank of Canada)
ACCOUNT NUMBER: 5122551
TRANSIT NUMBER: 06742
INSTITUTE NUMBER: 003
SWIFT CODE: L0YCCAT2

Vilevile unaweza kutumia E-mail Money Transfer kwenye anuani pepe gilfa36@hotmail.com .Pia unaweza kuwakilisha msaada wako kwa kutumia anuani hii:

5-7 DRIFTWOOD CRESCENT
NORTH YORK,ONTARIO
M3N 2R1

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:

Kaka yake Fatuma (Issa) kwa nambari hii-647-760-1051.

Emmanuel -416-835-6778.
Gabriel- 416-631-7762.

Kwa upande wa nyumbani Tanzania,tafadhali wasiliana na Fred Kaduma kupitia nambari 0655-888268 kwa taarifa zaidi.

Tafadhali chukua muda kuwafariji na kuwaombea ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu. Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa na itakayotolewa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

- Amen.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Poleni sana wafiwa. Roho ya marehemu ipumzike kwa amani. Amen

    ReplyDelete
  2. NAWAKUMBUSHA TENA WATANZANIA WENZANGU MLIO NJE YA TZ KUHUSU HUDUMA YA NSSF YA MAZISHI NA KUSAFIRISHA MIILI, HUDUMA HII IMEZINDULIWA NA IMEANZA MUDA SI MREFU ITUMIENI MPUNGUZE KUOMBA MICHANGO, CHANGIENI DOLA 300 NSSF ILI MJIPUNGUZIE GHARAMA KUBWA ZINAZOZUILIKA, NCHI INAWAJALI NYIE HAMJIJALI, ITUMIENI NSSF AU MNAFAIDIKA NA HUO UTARATIBU WA MICHANGO YA MARA KWA MARA ? NA RATE YA WATANZANIA/WAAFRIKA KUFIA NJE IMEKUWA KUBWA KWA SASA HIVYO HII HUDUMA ITAWASAIDIA SANA NYIE DIASPORAs, pole sana familia ya KADUMA na watanzania kwa jumla !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...