Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kushoto) na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (Mb) kwa pamoja wakiwa na mazungumzo ya kina leo na ujumbe wa Tume ya Huduma za Bunge la Malawi ulioko nchini hivi sasa, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia uhusiano mzuri wa mabunge ya nchi mbili hizi. Kushoto kwa Mhe. Ndugai ni Naibu Spika wa Bunge la Malawi Mhe.Juliana Mpande (Mb) ambaye ni mkuu wa msafara. Wengine ni Kamishna Alfred Mwechumu (Mb) na Kamishna Christina Chiwowo (Mb).
Spika wa Bunge la Tanzania akiwa na mazungumzo na Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliofika ofisini kwake Dodoma leo. Spika Makinda amewataka na kuwaasa kuwa na uzalendo kwa nchi yao.Picha na Prosper Minja - Bunge


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...