Viatu hivi marufu kama raizoni vilitokea kupendwa sana katika miaka ya 78 na 80 vilikuwa marufu kwa vijana wa enzi hizo waliokuwa wana jipenda na walio toka katika vita vya kumuondoa nduli iddi amini  bila kiatu hichi ulikuwa bado hujaonekana kama umeingia mjini lazima uwenacho pamoja na suruali ya bugaloo mwenzangu cha kwako kiko wapi leo mie bado ninacho kitunze kidumu. Hapo bei sh. 480/- - Mdau Chris Mfinanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. du, umenikumbusha moshi secondary (mosesco).

    ReplyDelete
  2. Assalama Lekko zako Ankal Michuzi!

    Hiyo zilipendwa uliifungia wapi?

    Au anayemiliki Raizoni hizo alifungwa Jela mwaka 1978 na leo ndio ametoka kifungoni na kukabidhiwa viatu vyake?

    ReplyDelete
  3. Duhhh Mjomba Michuzi ama kweli unatutoa kimaso maso na hazina uliyo nayo!

    leo umefunja sanduku na kutoa viatu vyako ulivyotesea Kinondoni Secondary?

    Au ndio maandalizi ya Sikukuu ya Idd El Fitri?

    ReplyDelete
  4. Hapo mziki wake ukipigwa watu wanagonganisha makalio yaani mtindo wa 'bumping'

    Kizazi kipya mpo hapo?

    ReplyDelete
  5. Ahhhahahaha

    Mwenye viatu hivyo alikuwa amefungwa kifungo cha miaka 34 tokea mwaka 1978 na leo ndio ametoka na Getini Magereza-Lupango wamempatia viatu alivyokabidhi ahifandhiwe wakati akianza kifungo!

    ReplyDelete
  6. hahaha jamani!

    zamani raha! niliyajua kwa jina la shuka tubonge au teremka tubonge.

    nilikua nayo pea mbili brown na black.

    masharo hawawezi hizi.
    ahsante saana.

    ReplyDelete
  7. Viatu hivi ninanikumbusha wimbo huu

    Ohhh Selina piga konde moyo ohhh Selina X 2

    Na kwa sababu imekuwa hivyo Selina, hiyo isiwe sababu na kutaka kuniuwa kwa ajili yako.

    Ohhh Selina piga konde moyo ohhh Selina X 2

    Ohhh Selina aahhhh!

    ReplyDelete
  8. Ankal una vituko wewe?

    Kipindi viatu hivi ninawika miaka ya 1977 - 1980 huko, Noti ya Tshs. 100 ilikuwa kama Tshs. 10 Milioni kwa sasa!

    ReplyDelete
  9. MaSaNTuLa lol:))

    ReplyDelete
  10. Tulikuwa pia tukikiita kiatu hicho mkuki moyoni.

    Halafu pia kulikuwa na shati lenye picha ya ndege mgongoni.

    lol

    Mdau Richard.

    ReplyDelete
  11. PASELEPA:

    Ohhh vijana tafadhali mjirekebishe vijana ohhhh X 3

    Sisi tunawahusia vijana wa kiumeee mchezo huo ni mbaya na tena ni aibuuu unaharibu heshima za wazazi wenu X 3

    ReplyDelete
  12. NUTTA JAZZ BAND:

    Miaka hiyo ya 1977-80 Kibao Kasimu:

    Unapokuwa huna pesa nyumbani hutoki eee Kasimu mwisho wa mwezi unapofika Kasimu huonekani X 2

    Unapotoka kazini unafikia kwenye Baa, unapowakuta marafiki unaagiza 'lete kama tulivyooo?' X 3

    ReplyDelete
  13. Nakumbuka bila raizoni hupati mke kule mji kasoro bahari..jamaa wanamsimamo koma..ukifika namshenga macho yote kwenye miguu ukisikia wanaguna ndio hakunaga...akisante mdau kwa kutunza raizoni.

    ReplyDelete
  14. Kwa kule Kae Marehemu Saidi Marizawa Beho ndio alikuwa championi wa mitindo ya raizoni na shati la kubana la slim fit!!! Shati ni la ndege aina ya tai au Diplomat la Burundi au Zaire.

    ReplyDelete
  15. Sasa hiyo enzi hizo wenyewe wakizivalia zile suruwali juu nibanie, chini nibwagie almaarufu buga, halafu kiunoni kwa nyuma na kwa pembeni mifukoni zimesukwa design fulani hivi na juu kashati kale kakubana mikononi kamechanuwa kidogo wakiita slim tight, ama kweli umekumbusha mbali saana kwa kutuwekea hii raizoni, wengine wakiita platform au stuli. Halafu ndo mtoko unakwenda kuirukia 'kamanyola bila jasho' kweli ya jana siyo ya le, thus nice!

    ReplyDelete
  16. mimi ni kizazi cha digital, ningependa siku moja ankal au mdau yoyote avae hizo swaga za zamani, shati la slim tight lenye ndege mgongoni, suluari ya pekosi na raizoni afu atupie picha humu ili sisi vijana wa sasa tuone swaga za zamani zilikuwaje, inaelekea wenzetu mlienjoy sana kwa sababu hakukuwa na uchakachuaji wa kichina.

    ReplyDelete
  17. pia liliitwa DIGANZA sio mkuki moyoni, mkuki moyoni kilikuwa na soli ya kawaida ila kimechongoka sana mbele.

    ReplyDelete
  18. Hhahahahah Raha kwa tuliokuwepo enzi hizo,hapa anko,shati lilikuwa slim fiti ,yaani ukitaka kulivaa unavuta pumzi nyingi ndani na tumbo unalivutia ndani ,ndo unafunga vishikizo.Mkanda mpanaa,nywele ndefu ,suruali ya BUGALO au PEKOZI,imeshonwa mifuko miwili ya mbele,kipindi kile tulikuwa hatuweki walleti mifukoni,kwahiyo nyuma unakuwa flat hivi.Hata hivyo hicho kiatu hapo ni ngazi nne tu ,vilikuwepo ngazi sita,nagzi ni nizo gorofa za kisigino hahahahahahahahah asante sana michuzi umenikumbusha mbali enzi za kupokea mashujaa wakitoka kupihana Uganda,wote walikuja na Radio kasseti,na hivyo viatu

    ReplyDelete
  19. Nyimbo hizi 1977 huku Selemani akiwa amevaa Raizoni:

    PART -I
    MARIAMU AMUIMBIA KAKA SELEMANI:

    ''Kaka Selemani ukifika mjini kwanza ujitayarishe kuhusu ahadi yetu.

    Nimesubiri sana hadi nimechoka kaka Selemani niamue vipi? X 2

    Ohhh Selemani! X 3''


    PART -II
    SELEMANI AMUIMBIA DADA MARIAMU:

    ''Nilipofika Mjini dada Mariamu, kusema kweli nilishika mambo ya mjini.

    Kuhusu ahadi yetu, dada Mariamu naomba unisamehe! X 2

    Ohhh Mariamu X 3''

    ReplyDelete
  20. Duhh Mjomba Michuzi kweli bahili sana!

    Yaani unaweka sandukuni viatu kufikia miaka zaidi ya 30 ?

    Ama kweli Uchumi unaufahamu vema!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...