Mhe. Prof. Makame M. Mbarawa (Mb.), Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa mamlaka aliyonayo anapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa ameteua wajumbe wafuatao ili kuunda Baraza la Chuo cha Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela - Arusha:
      Prof. Idris Ahmada Rai
      Bw. Arnold Kilewo
      Prof. Idrissa Mshoro
      Prof. Joram J. Buza
      Bw. Makuru James Nyarobi
      Dkt. Julie Makani
      Bw. Augustin J. Kajigili
      Bw. Nicolaus H. Shombe
      Prof. Evelyne Mbede.
Baraza la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela - Arusha litakuwa na majukumu ya kusimamia shughuli za Taasisi hiyo. Uteuzi wa wajumbe wa Baraza hilo ni kulingana na matakwa ya Hati Idhini (University Charter) ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela-Arusha. Baraza hilo litakuwa chini ya uenyekiti wa Mhe. Prof. David Mwakyusa (Mb.) ambaye aliteuliwa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela – Arusha ni wa kipindi cha miaka mitatu na umeanza rasmi kuanzia tarehe 27 Juni 2012.
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela – Arusha imeanzishwa nchini Tanzania kwa lengo la kuliwezesha Bara la Afrika kwa upande wa Kanda ya Afrika Mashariki kuweza kusonga mbele kwa haraka katika nyanja za sayansi na teknolojia. Hii ni moja ya Taasisi zilizopo katika kanda nyingine nne Barani Afrika. Taasisi nyingine zipo katika nchi ya Nigeria, Burkina Faso na Afrika Kusini.
Dkt. Florens M. Turuka,
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hii Haipendezi hata kidogo kuwepo na Wanawake wawili tu kati ya wateule Tisa! Hata ile 30% SADC Treaty ya 1997 haikuzingatiwa, mbali na 50/50 Africa Union na Maputo Protocal ambayo Serikali yetu imeridhia! Kumbe kweli katika hii mikutano ya Kimataifa viongozi wetu wanakwenda kiusanii tu na kusign makubaliano Kiusanii vile vile.

    ReplyDelete
  2. Mbona waislamu wawili tu?

    ReplyDelete
  3. Naona Mheshimiwa amejitahidi. Kwenye mambo ya Technolojia ni Technology ukileta siasa kila mahali unaweza kumweka Rubani mtu asiyejua kuendesha hata baiskeli. Tuwe makini tusije kung'ang'ania ambavyo havina taaluma. Tuwawezeshe kusoma na sio kuwateua tu kwa kuwa ni kundi fulani

    ReplyDelete
  4. Utajuaje Uislam kupitia Jina? Acha uzushi wewe? Bwana Edward Mhina kwa jina, ila ni Muislam. Bwana George kwa jina ila Muislam. Acha choko-choko za Uzanzibara na Uzanzibari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...