Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa wosia kwa wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2012 bungeni leo mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti , kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.
Wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2012 wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti na Waziri Mkuu, kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.Picha na Anna Nkinda – Maelezo

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewataka wanafunzi wote nchini kuwa na nidhamu , kujituma na kufuata maelekezo vizuri ya walimu wao na kuepuka makundi mabaya ili kuweza kupata mafanikio katika masomo yao.

Aidha Waziri Mkuu Pinda amewaasa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kuhitimu kidato cha sita wa mwaka huu kutumia uhuru vizuri watakaoupata kwenye maisha ya vyuo vya elimu ya juu bila kurudi nyuma katika maendeleo ya masomo yao.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri Mkuu, Pinda Bungeni mjini Dodoma kabla ya kuwatunuku vyeti vya kuwapongeza wanafunzi hao 19 kati 20 waliofanya vizuri katika mtihani huo,kutoka shule mbalimbali nchini, ambapo mmoja wao, Jamal Juma yuko nje ya nchi.

Wanafunzi hao ambao wote walipata ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani huo, saba kati yao wanatoka katika shule ya wasichana ya Marian, watatu Mzumbe, wawili Fedha na wengine wawili Kibaha. Waliobakia mmoja mmoja anatoka Kilakala, Ufundi Ifunda, Tabora girls, Tabora boys, Minaki na Mpwapwa.

“Mmefanya vizuri. Mnastahili ! Hongereni Sana. Tunataka ufaulu wenu uwe mzuri zaidi kwa vile sasa ninyi mnakweda kujenga weledi. Mnakuwa wataalamu wa fani Fulani. Tumieni muda wenu kujifunza zaidi kutafuta maarifa zaidi na kuvumbua mambo makubwa zaidi yatakayowasaidia ninyi wenywe na jamii kwa ujumla kujiletea maendeleo,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Aliongeza kuwa ni vizuri utaratibu huo wa kuwatambua wanafunzi bora uwe endelevu na ikiwezekana wapatiwe fursa ya kuendelezwa katika vyuo vikuu vya kipekee nje ya nchi hususan kwenye fani zitakazojenga uwezo kwa taifa.

Waziri Mkuu alisema kati ya shule 10 ,ambazo wanafunzi hao wanatoka, wawili ni kutoka shule za kata, ambao ni Ester Marcel toka shule ya sekondari ya wasichana ya Olele Kilimanjaro na Brighton Lema toka shule ya sekondari ya Kitangiri, Mwanza.

“Napenda niwape pongezi za pekee wanafunzi hawa kwa jihudi kubwa walizozionesha. Kufaulu kwao kunadhihirisha kwamba shule hizi za kata tukiweka bidii kwa kuziwezesha zaidi zitafanya vizuri zaidi kama ilivyo katika shule nyingine,” alisisitiza .

Waziri Mkuu pia aliwataka walimu wote nchini kushirikiana na wazazi na serikali kwa pamoja kufundisha watoto kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao kama wanafunzi hao waliotunukiwa vyeti hivyo.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema wanafunzi hao watazawadiwa pakato (laptop) na sh. 200,000, pia kila shule iliyotoa mwanafunzi bora itazawadiwa sh. milioni moja katika hafla maalum itakayofanyika jioni.

Wanafunzi hao wanatoka katika mchepuo wa PCM ambao ni 16 na mmojammoja toka mchepuo wa PGM, CBA, ECA na HKL.

Naye Spika wa Bunge la Jamhuri, Anna Makinda aliwataka wanafunzi hao kuwa makini na makundi kwa kuyasilikiza huku wakitumia akili zao huku akitoa changamoto shule nyingine kujitahidi kufanya vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Inasikitisha sana kwa top 20 meaning the best students wa 2012 kupewa cheti, laptop na laki mbili.

    i would expect hawa wanafuzi watafutiwe scholarship to the best schools in the world na wawe fully paid mpaka watakapomaliza ili wakirudi wafanyie kazi nchi yetu kwa maendeleo ya wote. Ayway God Bless Tanzania, tunasonga hivo hivo kibishi

    ReplyDelete
  2. Mbona hakuna mwanafunzi ambaye si Mkristo hapo?

    ReplyDelete
  3. Ambao si wakristo wanakaa kwenye viti....si mkekani!

    ReplyDelete
  4. Kazi nzuri Anna. nami naunga mkono commenter wa kwanza, ingefaa zaidi hawa wanafunzi watafutiwe scholarshi. nimeshaona wengi waliopitia hapo, kutoka hapo basi tena hawana mbele wala nyuma kwakuwa hatuna uendelezaji mzuri wa vipaji maalumu.

    ReplyDelete
  5. Mchangia hoja wa pili umejuaje hilo unalolisema na una maanisha nini?

    ReplyDelete
  6. Huyo anonymous wa pili nafikiri uwezo wa akili zake umedumaa. Hayo majina mawili yamemfanya aandike "Mbona hakuna mwanafunzi ambaye si mkristo hapo?" Huyu nafikiri ahamie kule kwenye uamsho.

    ReplyDelete
  7. mwanzo niliona wametajwa kwa majina lakini sasa yametolewa, nadhani baada ya watu kudadisi kulikoni wawe ni wakristopeke yao ndio waliofaulu vizuri..haingii akilini hata kwa mpumbavu ajilia mbali mmjinga..
    LAKINI ya pili ni kuwa MIZENGO anasema eti watafutiwe vyuo nje ya nchi ambapo nasikitika kuwa hata baadhi ya wachangiaji wamemuunga mkono, hivi kila kitu kizuri kipo nje ya nchi yetu?.mbona hawa waliofaulu vizuri hawakutoka nje basi...tudhamini vyetu na tuachane na upuuzi huu..
    NAPENDEKEZA katika KATIBA MPYA hili suala lipigwe marufuku kwa mtanzania yeyote kwenda kusoma nje hata kama awe na uwezo gani isipokuwa kwa wale wanaoenda kusomea kuanzia ngazi ya uzamili na uzamivu au kwa ngazi ya digrii ya kwanza lakini fani anayoenda kusomea huku iwe haifundishwi hapa nchini. hii itasaidia sana serikali na hasa viongozi kuweka mkazo katika shule pamoja na vyuo vyeti vinginevyo watoto wa maskini wataendelea kuwa mbumbumbu na wa matajiri/viongozi wataendelea kuonekana wana vipaji maalumu na hivyo kuridhi uongozi toka kwa wazazi wao kitu ambacho si kweli..

    ReplyDelete
  8. Mdao hapo juu naona umasikini wako unakufanya uone wivu kwa wanaosoma nje pole sana naona na wewe unatakiwa ufanye kazi kwa bidii ili watoto wako wakasome UDSM ambapo ma lecture wana kuja na stress zao za nyumbani na ku waaletea wanafunzi..

    ReplyDelete
  9. Na uliza swali hawa wanafunzi bora au best students wenu wanatoka shule zipi? ni za kata au shule bora (best Schools).Naomba wizara isijisifu kabisaaaa.Je wapo wanaotoka shule zao za kata walizoanzisha au zao za serikali.It is Shame to our country. Maana hao wate hapa wanatoka familia bora na wamesoma shule bora toka utoto wao, kuna aliyesoma shule zetu za KIDUMU MFAGIO na kuendelea katika shule za Kata?? Kama wapo naomba jibu.
    Sasa hao raia wa kawaida watoto wao lini watakuwa best students kwenye shule zisizo na madawati,usafiri shida,walimu wana migogoro na serikali,vitabu hakuna na mitaara mibovu.Serikali liangalie hili si kila mazuri ni ya watoto wao tu.Ndio maana mimi hata sitaki kurudi huko nyumbani maana maisha ni ya ubaguzi mno kuliko hata huku tuliko.Jamani inatisha kama hata Serikali hailioni hili,Saidieni hao watoto jamani wasio katika familia bora hata kuwapa elimu nzuri tu inatosha.

    Mdau kutoka Brighton - UK

    ReplyDelete
  10. Hii ni kawaida ukiwa muislamu unapigwa chini, labda ubadili jina ujiiete josefu, ndio maana baadhi ya wazazi waliita watoto wao majina ya ajabu ili wasome, mfano zitto kabwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...