Ankal,
Naomba uwashauri wakubwa  watumie ramani zilizopo kwenye taarifa mbali mbali za miaka ya enzi za ukoloni hasa zilizoko kwenye maktaba (wakati Tanzania inaitwa Tanganyika; na Malawi inaitwa Nyasaland) watapata ukweli kuhusu mipaka yetu. Wakitumia ramani za siku hizi hawataambulia kitu kwani wenzetu wanatumia IT kubadilisha ramani hizo. Nimeona hata baadhi ya ramani zinaonesha kuwa mlima kilimanjaro upo Kenya. Hizi ni njama za majirani zetu wanazozitumia ili siku za baadae watumie kuporea rasilimali zetu.
Cheki mwenyewe hizi ramania
Mdau Nick

 Moja ya stempu ya Malawi ya mwaka 1945
 Ramani ya Nyasaland (Malawi) ya mwaka 1935 iliyopatikana kwenye “Colonial Reports” za Uingereza kama inavyoonekana hapo chini.


1: The map of Tanganyika that Garth Hoets and Nigel Roberts used in 1959 when climbing Mt. Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. Jamani me naona wana haki ya kusogeza kwani hata wakifanya exploration wakapata hayo mafuta watafaidika nayo lakini sisi hata tukipata hayo mafuta tutakua kama nigeria tuu hamna kipya

    ReplyDelete
  2. WEWE UNAYETUTOLEA HII RAMANI,INAMAANA HUKUSOMA GIOGRAFIA YA DARASA LA TANO MDAU?ACHA UTOTO.

    ReplyDelete
  3. Ushahdi wa Madai ya Malawi hauwezi kuzingatiwa kwa kuwa Sheria haigandi ila huenda na wakati.

    Pamoja na kuwa Mkoloni aliweka Mipaka kama ushahidi unavyoonyesha, sheria za Mipaka na Tawala za nchi zikapata mabadiliko kipindi hadi kipindi kadri maisha na changamoto zimekuwa zikijitokeza.

    Haiwezekani kuzingatia Sheria na Mipaka ya Mkoloni ambayo aliiweka kwa maslahi yake.

    KWA SASA NCHI ZOTE DUNIANI ZINAZOPAKANA KWA MAJI NI LAZIMA ZIGAWANE KATI KWA KATI KWA MPAKA KUWA NDANI YA MAJI.

    KWA KUWA CHINI YA KANUNI ZA UN-UNESCO, RASILIMALI ZA DUNIA ZINAGAWANWA KWA WAKAZI WA DUNIA NZIMA KWA USAWA KULINGANA NA MGAWANYIKO NA PIA KWA MAENEO YA HISTORIA NI MALI YA DUNIA NZIMA NA SIO NCHI PEKEE.

    MIFANO:
    1.MAREKANI NA CANADA, WANA MIPAKA YA GREAT LAKES LAKINI MPAKA UMEPITA KATIKATI YA MAZIWA NA NDANI YA MAJI PANA UPANDE NI USA NA UPANDE NI CANADA.

    2.ULAYA, MTO WA RHINE UNAANZIA USWISI HADI UHOLANZI NA PANA SEHEMU UNAPITA MIPAKANI BAINA YA NCHI VIVYO HIVYO MTO RHINE UMEGAWANYWA BAINA YA NCHI KWENYE KINGO ZAKE KUANZIA UNAPOPAKANA USWISI NA UJERUMANI, UJERUMANI NA UFARANSA HADI UJERUMAJI NA UHOLANZI.

    HIYO NI MIFANO MIWILI YA KIMIPAKA KWA KANUNI ZA KIMATAIFA ZA UN ZA MIPAKA YA NDANI YA MAJI.

    HIVYO HUTAWEZA KUSIKIA MAREKANI AU CANADA IKIDAI UMILIKI WA PEKEE WA MAZIWA MAKEE.

    NA WALA HUWEZI KUSIKIA NCHI MOJAWAPO YA ULAYA IKADAI UMILIKI WA MTO RHINE PEKE YAKE.

    SASA MADAI YA MALAWI SIO SAHIHI, YAPO NJE YA KANUNI ZA MIPAKA ZA KIMATAIFA KWA SABABU HUWEZI KUJIMILIKISHA RASILIMALI ZA DUNIA KWENYE NCHI YAKO WAKATI ZINATAKIWA ZIGAWANWE KWA WAKAZI WOTE WA DUNIA KULINGANA NA MGAWANYIKO ULIVYO.

    CHA ZAIDI MALAWI NI MUHIMU WAELEWE YA KUWA SHERIA INAENDA NA CHANGAMOTO, MUAMKO PIA, MABADILIKO YA MAENDELEO YA JAMII NA SIYO KWA MUJIBU WA HISTORIA.

    NA KUWA SHERIA NYINGI ZA MIPAKA ZA MKOLONI ZIMEVUNJWA NA SHERIA MPYA ZA KIMATAIFA ZA UMOJA WA MATAIFA.

    ReplyDelete
  4. Watanzania hatutakiwa kuanza kutafuta mpaka ulipo. Maisha ya watanzania zaidi ya 600000 yanategemea ziwa Nyassa, kwa hiyo swala la mpaka kupita katikati ni lazima liwepo. Tunachotakiwa kufanya ni kutafuta njia mbalimbali za kidiplomasia za kuwafanya Malawi wakubaliane na hilo. Hata hivyo opitons zote lazima ziwepo mezani, no option is to be lesft aside. Kuliacha ziwa lote kwa Malawi ni kuwasaliti watanzania wanaoishi kwa kutegemea ziwa hilo enzi na enzi.

    ReplyDelete
  5. Malawi nao wanasema kuwa hawajali na wapo kwa lolote,nakumbuka wakati tukiwa wadogo miaka ya 1969 au 1971 kama sikosei Kamuzu Banda alisema mbambabay mpaka mbinga nisehemu yake,lakini kama sikusahau Nyerere aliwaambia mjaribu muone.kwanza hawa malawi wapo chini yaani unajiwekea makombora kwenye milima ya livinstone huna haja ya kutumia ndege za kivita wewe unaagiza tu toka juu,waache wajaribu ,nchi za kiafrika akili zetu choka kabisa wakati huu si wa kugombania mipaka ni wakati wa kuungana na kutafuta maendeleo

    ReplyDelete
  6. Busara itumike sana,majadilianao,mahakama,vita iwe suruhu ya mwisho.

    ReplyDelete
  7. Ni mkanganyiko mtupu

    David V

    ReplyDelete
  8. Hii biznes ya kuita hili ziwa Lake Malawi imeanza lini kwanza, au zilikuwa propaganda za Kamuzu Banda?

    ReplyDelete
  9. Huyy ndugu Nick ni Mzalendo sana. Namshukuru sana kwa utafiti wake. Inaelekea ndygu zetu wa Malawi wamebadilika kwa sababu huenda hiyo oil and gas prospecting waliyoifanya inaonyesha wingi wa mali hizo upande wetu. Lakini wadau wa hapa Tukuyu wanasema wameshuhudia usiku wa manane vifaa (vya IWTZ??) vikitermka kuelekea Kyela. Kwa hiyo hata Bwana Membe alipokuwa akitoa onyo wakati wa hotuba ya wizara yake jusi bila shaka alikuwa anajua si maneneno matupu lakini jamaa wamekwisha jizatiti. Ile hotuba ya Memebe ilisharushwa kwenye blogu hii? Nakumbuka alitaja mikataba na makubaliano ya enzi za ukoloni nilipomuona kwenye TV.> Nataka kuitafuta hiyo ikataba kwenye Google ili tujiweke sawa kihoja na kifikra na kihistoria. Maana wanyasa wanatukana sana kwenye blog ya Nyasa Times bila hoja za msingi zinazonukuu madokumenti ya kihistoria. Nimefurahi sana kwa hiyo kuona stempu za kwao wenyewe zikionyesha mpaka uko katikati. Lakini ukiwpelekea hiyo Nyasa Times sijui watasema tumeiunda sisi hiyo stempu?

    ReplyDelete
  10. Ninachoelewa mm Kama kesi itapelekwa icj Wao wataangalia mipaka waliyoiacha wakoloni kutatua Tatizo lililopo. Hatawatakurupuka tu. Naamini Kuwa diplomasia itatumika Zaidi kutatua Tatizo la mpaka baina ya tz na mlw

    ReplyDelete
  11. Mimi ni msomaji mzuri wa blog hii naomba wadau wote uchungu na nchi hii kama wanaweza kutoa vielelezo vya uthibitisho kuhusu ziwa Nyasa hii ramani ni moja ya vielelezo nzuri sana, watoe maana wenzetu huko Malawi hawaambilikiwanadai Ziwa Nyasa ni Mali yao na kumbe wananchi wa mbeya wanaoishi miaka mingi huko pia wanadai kuwa wangechukua eneo hilo wakitaka inauma sana!

    ReplyDelete
  12. Simply, BRILIANT! Hongera sana mdau.

    Kwa kweli tusingependa ugomvi na nchi kama Malawi, ambao ni ndugu zetu kabisa jamani. Isitoshe ni nchi ambayo hivi sasa ina Rais mwanamke, sasa kupigana nao vita itatushushia hadhi sana, kwani all the time Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusuluhisha mizozo kibao hapa Afrika.

    Yaani tumekuwa kama watoa nasaha fulani hivi when it comes to peace matters. Hivyo ushahidi kama huo aliotuonesha mdau mwenzetu wa stempu za enzi hizo, utasaidia sana kupunguza jazba na kuingiza some senses kwenye vichwa vya wale wanaodhani kuwa hilo Ziwa Nyasa ni la nchi ya Malawi zima zima!

    Be blessed people.

    ReplyDelete
  13. Malawi waache madai yao ya kibwege na kipumbavu!

    Hatuwezi kuheshimu sheria za Mipaka za Kikoloni, hivi Mkoloni ana mamlaka gani kwetu kwa sasa?,,,achilia mbali sisi Tanzania wao Malawi?

    Hakuna nchi Duniani inayozingatia Sheria ya Mkoloni iliyopitwa na wakati huku kukiwa kuna Sheria za wakati tulio nao za Umoja wa Mataifa!

    ReplyDelete
  14. Njaa mbaya!

    Hii yote ni njaa kali waliyonayo Malawi kudai umiliki wa ziwa lote kuwa lao.

    Ni kama ndugu zetu wa kuvuka maji wanaotaka kutengena na sisi, yote hiyo siyo suluhisho la njaa waliyonayo.

    Wao na Malawi ni damu damu kwa madai ya kijinga!

    Dalili ya yeyote mwenye njaa ni hulka ya roho mbaya,uroho na uchoyo!!!

    ReplyDelete
  15. Kama wanatuletea Sheria ya Mkoloni ya Mipaka ya mwaka 1890 sisi tutawapa Sheria za Mipaka za UN , na tutataka ktk Mahakama zao tuone je wangali wanatumia sheria za Mkoloni?

    Au sheria hiyo wameileta pekee kwa suala la madai yao ya kibwege?

    ReplyDelete
  16. Kama ndio hivi waliostahili kudai umiliki wa Maziwa mipakani ni Marekani ktk The Great lakes,

    Pale maziwa 'great lakes' yapo upande wa Marekani, lakini kwa kuwa kanuni ya UN ya mipaka ya majini inazingatiwa imebidi mpaka wa Canada na USA uwe ndani ya maji na kuipa nafasi Canada umikili wa sehemu za maziwa yale ingawa kieneo yapo ktk USA.

    ReplyDelete
  17. Ningekuwa Mkuu wa Majeshi TZ ningetuma kwa kupiga Kombora moja kubwa hadi ku ktk kona ya mpaka wa kwenye maji ndani ya ziwa ktk ramani ya chini!

    Hiyo ndio itakuwa salamu kuwa Tanzania hatutaki ujinga!

    ReplyDelete
  18. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA:

    KUANZIA ZANZIBAR HADI ZIWA NYASA,

    TUTAILINDA MIPAKA YA NCHI HADI DAKIKA YA MWISHO!

    ALUTA KONTINUA!!!

    ReplyDelete
  19. Safi sana ramani ziko wazi kabisa. Enzi hizo miaka ya 1950's nikiwa primary mpaka secondary school tulikuwa tukichora ramani ya Tanganyika ni ilikuwa sawa nahiyo hapo juu. Wamalawi waache ngebe

    ReplyDelete
  20. Hii yote madai ya Malawi ni ari ya kazi ya huyu mama Raisi mpya Joyce Banda.

    Akifanya mchezo ataikimbia Ikulu na ulimbukeni wake wa Uraisi.

    Mmeona mwanamke akipewa anavyokuwa?,,,mbona walivyotawala wanaume hakukuwa na madai ya kibwege ???

    ReplyDelete
  21. Raisi Joyce Banda na Malawi, wawaulize Uganda wasikie kuhusu Tanzania?

    ReplyDelete
  22. Inaelekea wakati Idd Amin wa Uganda anapigwa na Tanzania, huyu Raisi Joyce Banada alikuwa hajazaliwa!

    ReplyDelete
  23. Au wanataka kuongeza ukubwa wa Tanzania?

    Tutawatumia majeshi na kuwachapa!, hawawezi kusisitiza madai kwa misingi ya Sheria ya Mkoloni, je wao bado hawajapata Uhuru?, hivi bado wangali Sheria za Mkoloni kwao wanazitumia?

    Hawa jamaa wakifanya mchezo tutaigeuza Malawi kuwa Mkoa wa Tanzania!!!

    ReplyDelete
  24. Safi sana.umeleta ushahidi muhimu sana

    ReplyDelete
  25. Ramani zako hazina faida katika kutatua mgogoro wa mpaka. Suala kubwa katika mgogoro huu ni mkataba upi utumike na sio ramani zilizokwishatumika na nchi zote mbili.Kwa kigezo hicho hicho ulichotumia hapo juu, ramani nyingi katika mataifa mbalimbali duniani kwa sasa zinaipa Malawi ziwa lote.
    Mgogoro huu unatakiwa kupelekwa ICJ na kupatiwa ufumbuzi. Siasa na mazoea ya kwamba sehemu ya ziwa liko Tanzania aziwezi kutatua mgogoro.

    ReplyDelete
  26. thank you very much for that piece of research!watanzania tukizungumza sana "tutatukana",na kutukana sio jadi yetu.Tuutumie mgogoro huu kama changamoto ya kuzidisha jitihada ya pamoja na wenzetu wote wa Msumbiji,Malawi na Tanzania (nchi zinazopakana na ziwa nyasa)katika kuanzisha Mamlaka ya Kuendesha na Kusimamia Maendeleo ya Ziwa Nyasa katika nyanja zote kwa manufaa ya nchi zote tatu (The Lake Nyasa Development Authority).Kelele zote hizo hazitapata nafasi.Lakini kukimbilia "mikataba iliyoachwa na wakoloni kwa manufaa ya wakoloni" ni kufilisika kisiasa.Tusahau yaliyotokea, tuanze mwanzo mpya.Na kwa bahati nzuri sana Wana Msumbiji wanatuelewa sana katika hili.Kwa hiyo mwenzetu mmoja hawezi kutushinda sisi wawili,besides, anatutegemea sana katika mengi!

    ReplyDelete
  27. thank you very much for that piece of research!watanzania tukizungumza sana "tutatukana",na kutukana sio jadi yetu.Tuutumie mgogoro huu kama changamoto ya kuzidisha jitihada ya pamoja na wenzetu wote wa Msumbiji,Malawi na Tanzania (nchi zinazopakana na ziwa nyasa)katika kuanzisha Mamlaka ya Kuendesha na Kusimamia Maendeleo ya Ziwa Nyasa katika nyanja zote kwa manufaa ya nchi zote tatu (The Lake Nyasa Development Authority).Kelele zote hizo hazitapata nafasi.Lakini kukimbilia "mikataba iliyoachwa na wakoloni kwa manufaa ya wakoloni" ni kufilisika kisiasa.Tusahau yaliyotokea, tuanze mwanzo mpya.Na kwa bahati nzuri sana Wana Msumbiji wanatuelewa sana katika hili.Kwa hiyo mwenzetu mmoja hawezi kutushinda sisi wawili,besides, anatutegemea sana katika mengi!

    ReplyDelete
  28. na sisi akili zetu zingekuwa zimepinda,tungeanza na madai yasiyo na msingi kwamba Ziwa Tanganyika madhali lina jina letu basi ni ziwa mali ya watanganyika peke yao!LAKINI SISI TUMEKOMAA KISIASA,tunajua mipaka hiyo iliwekwa na nani na kwa maslahi ya nani.Angalia Maziwa yote ya mipakani Afrika ya Mashariki mpaka unapita katikati ya ziwa,kuanzia lake Albert,lake Edward,lake Kivu, Lake Tanganyika,lake Mweru,Lake Victoria, lake Chad,lake superior (marekani na canada),lake Huron,lake Erie,lake Ontario,Caspian Sea na Black Sea nchi za Urusi na majirani zake,etc. Why Nyasa be the exception? Maanake na bandari zetu za Itungi,Mbamba Bay, Lupingu,Manda,Chiwanda zitakuwa bandari bila ya maji (maana ziwa si lao!).Acheni utani Malawi!

    ReplyDelete
  29. Hakuna mazungumzo sisi tunafata vile vile ilivyo wakiingia kwetu kamata tu weka gerezani. wakiingia jeshi lao au polisi zamisha tu.wakikamata watu wetu tuwafuate na mashine zetu tuchukue watu wetu.

    ReplyDelete
  30. Hii yote nadhani ni effects za Partition of AFRICA, ambapo masuala ya kugombania mipaka ya nchi zetu barani Afrika, yalipojadiliwa huko Ulaya na kuamuliwa huko huko ( just in the piece of paper) wakati huo, bila hata ya kuwahusisha watawala wetu wa jadi kwa wakati huo (wakuu wa nchi husika), as a results ndio maana imekuwa ikileta migogoro mingi sana ya kugombania mipaka barani Afrika.

    Na Mlima KILIMANJARO kwa ilivyo khasa ni wa nchini Tanzania, sijuwi kwa nini wanawaachia hawa wakenya wajilabu kuwa ni wao na upo nchini kwao. Wakati ramani inajionyesha wazi upo ndani ya mipaka ya Tanzania. Historically was rewarded to TANZANIA for specific reasons, they have to recall what does history say abaout those things to resolve hizo border disputes zisizokwisha barani Afrika. Mungu libariki Bara zima la Afrika na usaidie migogoro yake iwe inamalizika kwa salama na amani bila '"bloodshed" wala ghasia nyinginezo.

    ReplyDelete
  31. Mdau unayesema mikataba ndo muhimu kuliko ramani nakuunga mkono lakini jiulize kwamba mkataba uliingiwa mwaka 1890, ramani zilizochorwa baada ya hapo (miaka ya 1935) zinaonesha mpaka upo katikati. Na aliyechora mipaka hiyo ni huyohuyo Muingereza aliyepewa ziwa lote. Haiingii akilini upewe ziwa lote halafu uchore ramani mpaka upitie katikati ya ziwa. Huoni kama kuna uchakachauaji ulofanywa kwa makusudi? Na kwa nini mkataba huo uwe wa Uingereza na Ujerumani 1890 na usihusishe waliogawa Africa 1884?

    ReplyDelete
  32. yaani hawa ndugu wasi tu beep, maana tunamakombora mpaka yanatulipukia wenyewe (Mbagala),tutawapa kibano na kuchukua ziwa lote

    ReplyDelete
  33. Mungu atuepushie hili la vita na kuweka mazungumzo mbele .Rais huyu mwanamke anataka kuonyesha uwezo wake kwa nguvu ya silsha anazoziona kwa macho nasiyo uwanjani kwenye vita.Watanzania tukatae vita Malawi Hawana chochote cha kutshinda, wako hoi wakiwa kariakoo ndo utajua kweli hali zao ni mbaya.

    ReplyDelete
  34. wapeni tu maaana tulivyokuwa navyo vyote totally mismanaged ushahidi uko wazi
    tanzanite
    gold
    natural gas
    diamonds
    ocean
    games and national parks
    beaches
    coal
    bandari tatu za bahari
    reli mbili za nguvu
    magugu maji ziwani
    etc
    wakipata wanaweza kuwa wabunifu zaidi yetu nasi tukatoka kupitia kwao maaana ukikaa karibu na waridi utanukia waridi.

    ReplyDelete
  35. wameambiwa mazungumzo wamegoma...then kinachofuata ni force..

    lazima tuilinde mipaka yetu na ardhi yetu kwa gharama yeyote...kwani tukiachia hili..kesho kenya watasema Arusha ni yao...keshokutwa Uganda wataitaka Kagera na siku inayofuata Rwanda na Burundi zitaona nchi zao ni ndogo sana so waziongeze kidogo kwa upande wa Tanzania na tena na tena na tena....

    ReplyDelete
  36. Mtaji na uwezo tano!

    Makombora kufyatuka Mbagala na Gongolamboto ile ilikuwa ni ajali !

    Sasa yanatakiwa yaelekezwe kwa adui (Malawi)

    Ni bora kabla ya kesi kufika huko ICJ -Mahakama ya Dunia Malawi wanastahili kwa ghadhabu tutume Majeshi tuwapige kwanza!

    Ili nchi zingine zijifunze kuwa Tanzania sio mahala pa kubipu!

    ReplyDelete
  37. Jamani mie sikuleta hizo ramani ili kuchochea vita. Nilitaka watu tuzitumie kuibua maswali ambayo yanaweza kuelekezwa kwa wamalawi. Mfano. Kwa mfano iweje mkoloni aliyepewa ziwa lote mwaka 1890 aje baade 1935 achore ramani inayoonesha mpaka upo katikati ya ziwa?

    Na hawa jamaa wa tanzania waliozaliwa maeneo hayo waklikuta Ziwa lipo na wakaanza kulitumia wao sehemu yao ni ipi?

    Na kwanini mkataba uingiwe kati ya muingereza na mjerumani mwaka 1890 peke yao bila kushirikisha wadau wote walioligawa bara la Africa?

    Binafsi nadhani maswali kama haya yanaweza kupatiwa majibu UN haraka iwezekenavyo ili ukweli ujulikane watu waendelee na shughuli zao za kiuchumi hapo ziwani na sio vita. Kama UN watatoa maelezo ya kutosha kuwa ziwa ni la malawi, basi hata vita haitasaidia kwani tutashitakiwa na kupigwa fine kubwa sana. Na kama UN watakubaliana na hoja zetu, basi hatutakuwa na haja ya kupigana bali kuanza jitihada za kuweka mipaka wazi na kuwaambia wachora ramani wa google waanze kuchora ramani kama zilivyokuwa miaka ya ukoloni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...