Mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi na Mussa Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala wakisimamiwa na Kocha wa mchezo uho Kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D' jana. Class anajiandaa kupambana na Sako Mwaisege ' Dunga' siku ya Iddi pili katika Ukumbi wa Diamond Jubilee na Sunga anajiandaa kupambana na Mussa Seif 'Boda boda' katika Uwanja wa Bandari Tandika Dar es salaam.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hiki ndio haswaa Kipaji chetu!

    Nafikiri haya mambo Mpira wa Miguu (Soka),Riadha,Mpira wa Mikono (Basketi) tuwaachie wenzetu!

    Kama ni Soka tubaki na Ushabiki wa Timu za Vilabu vya Ulaya na Nchi za Ulaya ni wazi kabisa sisi hatuna chetu!

    Kilichobaki ni Tanzania kuhamishia nguvu ushabiki na Jitihada za Mchezo wa Masumbwi!!!

    ReplyDelete
  2. Jamaa wa upande wa kulia picha ya kwanza hapo juu inaonekana amefumba baada ya 'gumi jiwe' la maana kuzama usoni mwake!

    Ahhh maisha yetu haya jamani, baadhi ya ajira zinataka ujasiri hasa si mchezo, hapo kwa mtu legelege si anakula kona na kutunduka ukutani glovu?

    ReplyDelete
  3. Ohhh !

    Migumi mshike mshike babake.

    Mchezo huu Masharo baro, Ma bitozi na Mateja wanauweza?

    ReplyDelete
  4. Mbona hawakufika Olympic? Hata Wasaudia wanatushinda!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...