Timu ya taifa ya Olimpiki ya Cameroun ambayo wachezaji wake saba, wakiwemo mabondia watano,  wameingia mitini jijini London wakiomba hifadhi nchini Uingereza ili kuendeleza michezo yao, wakisisitiza si kwa sababu za kiuchumi.  Wachezaji wanne wa DRC nao wamejilipua, na kufanya idadi ya wachezaji wa kiafrika waliobakia London kuwa 15.
  Cheki mavazi yao. 
Timu ya taifa ya Olimpiki ya Tanzania ambayo imeambulia patupu ila hakuna aliyeingia mitini. Cheki mavazi yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Una maanisha nini unaposema cheki mavazi yao? We kwani hujui kama hiyo ndo rangi yetu ya TAIFA?

    ReplyDelete
  2. Duh Nilijua lazima Baadhi ya washiriki wa hiyo OLYMPIC Watabaki.Kaazi kweli kweli ULAYA kumewatia watu UCHIZI.

    ReplyDelete
  3. Uwe una uhakika unapo toa habari, hiyo ni team ya Tanzania , lakini hapo haikua London hapo ni China kwnye Olympics mza miaka iliyopita. Mwaka huu wachezaji wetu walkua wachache zaidi na ikitawaliwa na Viongozi walio wengi huku wakiwa wamevaa Suti na vitambi njenje. Bendera yetu ilipeperushwa na Mwanadada !

    ReplyDelete
  4. hmmmmmm interesting

    ReplyDelete
  5. Sasa imefikia wakati ambapo michezo kama hii ikikaribia, washiriki wale kiapo na kuelezwa madhara watakayoyapata wakienda kinyume na kiapo hicho.Kwa sababu bila hivyo itapelekea kufungiwa kwa nchi za afrika kushiriki kwenye olimpiki maana baada ya olimpiki nchi husika inapaswa kujiandaa kuhifadhi wakimbizii. Mbayaeeeee

    ReplyDelete
  6. Sio mbaya kama ni 15 tu katika 1000 waliokwenda.

    ReplyDelete
  7. Poa tu walivyovaa wabongo.....nyie si bado mnatafuta vazi la taifa, wenzenu tayari wanalo.

    ReplyDelete
  8. Afadhali Wabongo jirudieni nyumbani pana njia zingine nyingi tu hapa Tanzania za kuyafikia malengo ya kimaisha zaidi ya kubakia kwenye Ukimbizi Majuu na kubebeshwa Mabox!

    ReplyDelete
  9. Viongozi wa timu hii wanapaswa kuwajibika au kuwajibishwa na si vinginevyo.

    ReplyDelete
  10. ...BORA MAVAZI HAYO, KULIKO YALE MA -SUIT MLIYOVAA WAKATI WA SHEREHE ZA UFUNGUZI, ...LAKINI HATA HIVYO BADO TUNAHITAJI VAZI LA TAIFA, AMBALO KILA MTU AKILIONA ANAJUA KUWA HIYO/HUYO NI MTANZANIA!!!

    ReplyDelete
  11. Hii ni timu ya Olimpiki ya Beijing 2008 sio ya London 2012.

    ReplyDelete
  12. Hiyo picha ya Tanzania ni Beijing 2008

    ReplyDelete
  13. Mbona hii picha ni ya Beijing Olympics na sio ya London Olympics 2012

    ReplyDelete
  14. HII JAMANI ILIKUWA PICHA YA OLYMPIC - CHINA NA SI LONDON HAPO...MSITAKE KUWACHANGANYA WATU..

    ReplyDelete
  15. Ankal Michuzi, hiyo picha ya watanzania sio ya London

    ReplyDelete
  16. Cha muhimu pia ni kushiriki katika Olimpiki na kujifunza mengi! Siku ipo tutapata medali tu...serikali isiwe bahili ianze kuwaandaa kuanzia sasa wanamichezo mbali mbali. Wizara ya michezo iongeze bajeti ya Olimpiki.

    ReplyDelete
  17. Hamkosi chakusema hata wangevaa khanga na vitenge mgesema unamaanisha nini kusema cheki walivyo vaa ulitaka waende uchi? wamependeza sasa na wakati wa ufumbuzi napo walipendeza sana tu! proud to be a Tanzania go Team Tanzania!

    ReplyDelete
  18. Ankal leo waosha vinywa wengi hawajakusoma, wanaosha vinywa tu bila kuelewa ujumbe ulokusudiwa.
    Waliwasema sana watanzania kwa suti walizovaa siku ya ufunguzi, na kuwapongeza sana hao walovaa mavazi yao ya asili. Kumbe ilikuwa ni magamba tu wamejivisha na wala hawakuwa na uzalendo na nchi zao.Lengo wala halikuwa kwenda kuwakilisha hizo nchi zao zaidi ya maslahi yao binafsi. Sisi tulovaa suti tumerudi kwetu kama tulivyokuja na wao wenye mavazi ya asili wamerudi pungufu. Endeleeni kuosha vinywa basi.

    ReplyDelete
  19. SASA MTOA MADA UMESHINWA KUPATA PICHA HALISI YA WATANZANIA LONDON. HIYO PICHA NI YA 2008 BEIJING, CHINA.

    ReplyDelete
  20. Uliona wapi serikali ikiandaa wanamichezo peke yake? Tunahitaji maandalizi ya nguvu ya kujituma na makocha wa ukweli. Maandalizi yanaanza leo sio 2015. Michael Phelps muogeleaji mashuhuri anakwambia anatumia miaka 4 minne kujiandaa sisi tunalemaa weee ikifika dakika za mwisho ndo tunakurupuka halafu tunaanza kulaumu serikali. Tunahitaji kuamka kwa kweli. Kama mliona story ya Rudisha mkimbiaji wa Kenya uliskia akiongelea serikali anajua ukitegemea serikali hufiki popote. Kwanza hata sijawahi kusikia mashinano ya qualifiers ili kupata washindi watakaotuwakilisha olympic. sijui hawa wanaotuwakilisha huwa wanapatikana vipi. Kwa kweli Mungu ibariki Tanzania tuondolewe na hii laana ya kutokuona mbali. Amen

    ReplyDelete
  21. Sasa viongozi turudi bongo tukashindane kunywa bia bila shaka tutatwaa gold hapo mji wa kilimanjaro lagger.ovyoooooooooooooo vitambi tuu.sirudi bongo kamwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...