Kaka habari yako,
Nimerudi tena mdau nina swali kwa ndugu zangu wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi hii nzuri.Nimezunguka na kuona miradi mingi ya barabara zenye kiwango cha lami nchi nzima na sasa nipo mkoani sumbawanga ambako zinajengwa barabara nyingi kutokea Tunduma hadi sumbawanga mjini,Sumbawanga mjini hadi Kasanga mpakani na nchi jirani ya Congo.Kutoka Sumbawanga hadi Mpanda mjini.Na maeneo kadhaa ndani ya majiji yetu hasa Dar es salaam.
Nchi yetu kwa kweli itapendeza sana ndani ya kipindi kifupi kijacho kwa kweli Watanzania tuliopo ndani tunajitahidi kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha kuwa nchi yetu inarudi kwenye heshima yake inavyostahili.mimi kama Mhandisi wa Power na Mawasiliano pamoja na baadhi ya Wahandisi wenzangu ambao tuliamua kubakia nchini na kupiga kazi tunaipongeza serikali kwa juhudi zake maridhawa katika kurahisisha maisha ya Watanzania masikini waliowengi.
Pia swali langu kuu kwenu ndugu zangu mnaoishi nje ya mipaka ya nchi yetu hasa Ulaya na Marekani je mmeifanyia nini au mtaifanyia nini nchi yetu??maana wengi wenu mmejisahau na mnasahau kwenu,nawasihi amkeni na mrudi nyumbani tujenge nchi yetu.Inasikitisha kuona tunaelekea kuzidiwa na nchi kama Uganda na Rwanda.
Unganeni huko mliko na tufanye kitu kwa nchi yetu ambayo kwa uhalisia ilikuwa inakwenda KOMBO.
Ndugu zangu Watanzania tuliomo ndani ya nchi tujifunze kuwa wazalendo kwa nchi yetu na tuache ubinafsi na uroho kama tunavyouona kwa baadhi ya viongozi wetu.
Naipenda nchi yangu na nitajituma kwa moyo wote kuhakikisha nchi yangu inarudisha heshima yake kiuchumi,kielimu na kiafya.Pia nitatumia juhudi kubwa kuwaelimisha Watanzania wenzangu maana ya Uzalendo kwa nchi yetu
NAWASILISHA HOJA
Mungu Ibariki Tanzania


I am paying over 100Millioni Shillings every year to the Customs office and TRA.
ReplyDeleteThose 100Millioni Shillings is helping you to get the job from the government, Road Constructions and most part to mafisadi.
I do hope when I come back to Tanzania, I will send the government to court by not using my hard earned money, which is currently recieved through TRA and other government coffers to build the country as you see it now.
According to statistics, the Diaspora send more money to Tanzania by eradicating Umaskini, than combine earning from the mines(riches of the country).
So this is the real question, what have you done to upstage the government as to where the rest of the funds paid by wabebamaboksi to the government,
Why no one is in jail since the government programme and propaganda war against Mafisadi ? it has only become a myth but no one accounted for their ufisadi?
secondly, dont you think based on Ufisadi, inefficiency, may be we could have done more, in Education, Health care and others...?
Unafahamu wewe na hoja zako lazima utumie akili kidooogoo...!! Hivi unajua unemployment Tanzania ni kiasi gani? Au kwavile wewe umebahatika kumfahamu karigabagaho mahali ukapewa kakazi sasa unataka watoto wetu walale njaa? Kuwa nje ya nchi haina maana hatuna mapenzi na nchi au hatuna akili za maendeleo...!! Kwa taarifa yako hata sisi tuna malengo na kama huelewi mchango wa Diaspora kwa mataifa inabidi urudi shule...kapige "Ungwini" kidogo labda utaelewa maana hesabu zimekuharibu. Watu walioko nje wanasaidia ndugu zao, wanaishi huku pia wanalipa bills, wanalipia nyumba ambazo wengine wamezinunua wengine wanapangisha...!! Hata wakiamua kurudi hamthamini michango yao ya mawazo na upeo badala yake ni wivu tu na kuwazibia maana wanamawazo mapana kuliko ninyi...sasa mnataka warudi ili iweje? Muwachore? Wewe endelea kujenga nchi bila kulalamika...na unakaribisha majuu pia ukitaka...njoo hata utembee tu labda utakuwa na mawazo mapana zaidi ya ulichoandika...!! Mdau-CA, USA
ReplyDeletemimi na furahi sana kusoma hoja hii nanina penda kuona watu kama wewe wanaoifikiria nchi yetu.ila hatuta weza kubadilika kama hatuta fundishana kupitia magazeti,tv na redio. hizi zikitangaza vitu vizuri kama kuonyesha barabara za wenzetu zilivyo wakaonyesha na za kwetu,ndio wanaangalia tulipo kosea. na kuelimishana pia halafu waonyeshe kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya wenzetu halafu tuangalie wapi tumekosea tuelimishane.sio kuandika kila siku wema,diamond,wolpa,uwoya.na kutoa picha za watu wako uchi au watu wanakunywa,au watu wachawi wamekamatwa.kwani ukiweka picha nzuri ya kuonyesha miundo mbinu ya china,japani watu hawanunui gazeti halafu unaelezea kuhusu miundo mbinu ya kwetu.na kusema tubadilike tujenge nchi yetu kwa mda wa miezi mitatu baadhi ya watu watabadilika nakufanya kazi kwa bidii,na alie kwenye kitengo chochote akisoma anabadilika.maana wanaosoma magazeti sana ni watu wa ofisini,wa mtaani wanaotembea n,klabda hivi itasaidia.yperrea
ReplyDeleteUzalendo wa kweli uletwa kwa vitendo, kwamba unaona watu wanvyoadhibiwa kwa kuitafuna rasilimali ya taifa! Lakini kama baadhi ya viongozi, na watoto wao wanaifisadi nchi, na hawafanywi chochote, ni ndoto kuleta uzalendo. Hata ukilazimisha namna gani, watu wataimba tu lakini ndani hakuna uzalendo!! ndio maana nchi kama China wanatoa adhabu za aina yake japo kuulazimisha uzalendo!
ReplyDeleteVazi la Taifa, wimbo wa Taifa, Bendera vitabaki nembo tu zisizo na thamani ya ndani (intrinsic worthy).
Uzalendo unaletwa na jinsi mnavyoona Wananchi wenzako wanafanyiwa, sio kuumizwa viungo hata kuondolewa uhai! Ndo maana nchi kama USA zinaweza kutumika rasilimali nyingi sana kumuokoa mtu mmoja aliyekwama sehemu yoyote. Hapa wanakuwa wanawekeza kwenye "collective patriotism", yaani uzalendo wa pamoja kwa manufaa ya baadaye.
Nchi unaifanyia nini?? Hili ni swali gumu, cha maana, ni je wewe unajifanyia nini (sio kwwa kuiba au dhuluma). Kila mwananchi akifanya hivyo, basi kwa ujumla nchi itapiga hatua kubwa ya maendeleo!
La sivyo, tutabaki kuwa na nchi iliyojaa kunguru kuliko njiwa. (na ukitembelea nchi/mji wowote (especially tropical countries) uwiano wa kunguru na njiwa itakujuza kama hapa kuna amani na utajiri au dhiki na vita!!)
Mhandisi uleyebaki nchini:
ReplyDeleteUmesema kweli kabisa, hao watu wa Majuu wengi zao ni dharau na lawama nyingi huku wenyewe huko Majuu wakiishi bila malengo, hawana ushirikiano ubinafsi kwenda mbele.
Ndio maana Wahenga walisema undani wa mtu hutokea yanapomfika mauti, imefikia wandugu zetu huko Majuu wanaishi maisha holela bila mipango iantokea mtu anaanguka kwa kifo marafiki ndio wanaitisha mchango ambao ni wa kudunduliza ili kufanya mazishi ama kusafirisha maiti kuja nyumbani Tanzania.
Tunashukuru sana Uongozi wa NSSF chini ya Mkurugenzi Mkuu Dr.Dau kuanzisha Mpango wa WESTADI ili kuwanusuru ndugu zetu na madhila yanayotokana na Misiba, kuugua na mambo mengine pia.
Ni wakati sasa wa Majuu mkajipanga na mkazinduka kwa machahe yenye tija kama haya:
1.Mfungue Vikundi mkiwa huko Majuu ama kwa mtu mmoja mmoja vya kujadili na kutahtimini njia za kuakisi maendeleo na kuchangia jitihada huku nyumbani Tanzania.
2.Mfanye Tafiti (Research) za Kisayansi na Maendeleo zinazoelekezwa kwa nchi yetu ili muweze kushiriki ktk jitihada ilhali mkiwa nje ya nchi.
3.Mfanye mialiko kwa Washirika (Development Partners) kutoka nchi mlizoko na kuwaalika kuja kuwekeza Tanzania kwa ubia na ninyi ktk Miradi mbali mablia mfano:
-Ukuzaji wa Uchumi kwa njia Masoko ya Hisa na Dhamana.
-Miradi ya Gesi na Mafuta (kuanzia ngazi ya utafiti ktk matumizi ya rasilimali kwa manufaa ya wengi nchini achilia Mitaji ya uwekezaji inayohitaji Mamilioni kwa Mabilioni ya $) ambayo neema ndio imefunguka.
-Ukuzaji ktk Sekta zingine lukuki nchini ambako fursa zimezagaa.
-Mjenge utamaduni wa Kushirikiana miongoni mwenu na kutathimini changamoto zilizopo mbele yetu hasa huku nyumbani Tanzania.
-Kuwepo na Vikao angalua vya Wana Tanzania kwa mwaka mara moja kuwakutanisha WALIOPO NCHINI NA WA MAJUU ILI KUJADILI MAENDELEO NA CHANGAMOTO ZINAZOTUKABILI.
-Kwa ujumla muwe MABALOZI WAZURI WA KUITANGAZA NCHI KWA NAFASI ZA TIJA ZILIZOPO NCHINI NA SIO KUWA MABALOZI WA LAWAMA NA KEJELI DHIDI YA NCHI YENU NZURI SANA.
katika vitu ambavyo vinge fanya tanzania kuwa kama ulaya ni hivi. 1;barabara 2;usafiri wa treni kupunguza msongamano 3;nyumba kuwa kwenye mpanglio mzuri 4;umeme wakutosha watu wweze kutumia kufua kupika wasipoteze muda kufua masaa au kupika masaa kuweza kumsaidia mtanzania kutumia vyombo vyote vya umeme. 5;alama za barabarani kuonyesha unaelekea wapi unakwenda wapi nanyinginezo mji uwe na geograf au uwe una ramani kumuwezesha mtalii kujua anataka kwenda wapi. 6;kuwe na vyoo kila eneo linalo onekana kuna watu wanahitaji huduma hiyo na isiwe ya kumlipa mtu unaweka mwenyewe hela ndio unaingia.7;kunapo tolewa huduma yeyote kuwe kuna mashine ya kutoa namba mlangoni ukifika huna haja ya kuweka foleni unajua namba yako ikifika utakwenda bila kupitwa na mtu hata hapo mileniam tower ipo ziwe nyingi hadi hospitaliofisi za serekalina kungineko,8;makondakta watolewe basi ziwe zina kengele za kumsimamisha dereva kituo unachokitaka.kuondoa makelele nakuibiwa na makondakta 9;msoko yote yaliop yajengwe super market badala yakuwa kama yalivyo ukienda gengeni unakanyaga matope unanyeshewa mvua matakataka yananuka hakupitiki wabadili system 10;tiketi ya daladala na mabasi yaendayo mkoani mtu unaweza kukata tiketi kupitia mashine za kulipia na unapata tiketi bila usumbufu na uhakika.wale wanao katatiketi wakafanye kazi nyingine ili kupunguza uwizi msongamano wa watu wasio fanya kazi warudi vijijini kulima tupate mazao mengi. kama tunataka tanzania iwe kama ulaya mengine mengi tume wazidi hawa watu na sijsviona huku na hawataki tuendelee sababu tutawazidi utajiri ndio maana kila tunapo taka kusonga mbele mara wanaturudisha nyuma kwa lolote kama sio vita magojwa,au chochote ili waturudishe nyuma,ni hayo tu
ReplyDeleteMhandisi umenena vyema sana,
ReplyDeleteTanzania imejitahidi saaana tuacheni unafiki, Wamajuu acheni dharau, lawama na ubinafsi !
Raisi wetu ndugu yetu mpendwa JK ameshawashukia mara kwa mara Madiaspora Majuu na kuwaalika mrudi nyumbani.
Amekwisha fanya mengi sana kuwaelekezeni huko angalieni NSSF Westani na Mkurugenzi Dr. Dau na mipango mingi kama Dual citizenship (Uraia wa nchi mbili) kama Mhe. Bernard Membe anavyowaeletea n.k.
Mlio fanikiwa endeleeni kukaa Majuu ila mchangie maendeleo nchini Tanzania ilihali mkiwa huko, na wale wenzangu na mie waliokosa Makaratasi mrudi nyumbani sio uongo kasi ya Maendeleo ni kubwa na neema imeshafunguka Gas na Oil mkononi acheni kukbeba maboksi mje mfanye kazi ktk mitambo ya gesi na mafuta Tanzania.
Zindukeni mtazame Dunia inavyokwenda!
Wamajuu tumieni akili,
ReplyDeleteHivi ni Mzungu gani amekuja beba magunia Tanzania?
Acheni ubwege rudini Tanzania nyumbani!
Hivi sasa nchi yetu imepata neema kubwa kabisa chini ya aridhi, rudini nyumbani haraka Wandugu neema imefunguka, mmeona Mabasi ya Kasi tunaelekea kuwa nayo kama Majuu!, tuna Treni za Mjini kama Majuu!.
Angalieni tuna mali lukuki:
-Oil
-Gas
-Uranium
-Steel
-Nickel
Ya nini kuota vigimbi vya mikono, mkawa Vijeba ilhani mkiwa bado wabichi Handsome boys?,,,na kuota sugu za mabega na mgongoni huko Majuu kwa kubeba mabox?
Jamaa wote manotuongelea ndugu zenu tulio nje', samahani, kwanza mnanikwaza sana. Nyie kila siku mnajifanya ndio mnafanya mambo zaidi au ndiyo mnasaidia TZ kuliko mtu mwingine yoyote kwa vile mpo bongo. Wacheni hizo. Sipendi kulumbana na afadhali Mithupu amesema mapema tusichafue hewa kwani nimejawa na jaziba mno, lakini basi tu. Siye tunasaida Bongo sana na mambo ni mengi hata kuyasema hapa. Na wala sidhani kama ni jamii ya kweli inasema yote haya, nadhani ni vibaka fulani mmewekwa kupima kitu. Kwani mnaju jamaa wa nje' ndio tishio kwenu kwa sasa kwani wanaelewa mambo sana. Hata mseme vipi sie ni wa Tanzania tu, kwa hiyo tutabanana tu wachemi mdomo mdomo. Kama wewe unasadia jamii nisiri yako,au unaona hupewi sifa?!!
ReplyDeleteMbona hueleweki unajichanganya?
ReplyDeleteHatua ya kwanza ni kuzuia wizi Serikalini ambao unafanyika kwa kasi kubwa.
Mengine yatafuatia baadae
Sasa ndg yangu si umeona mwenyewe watu walivyo vyichwa maji wewe utataka kwenda kulia wao wanataka kuelekea kushoto,akuna asiye taka kurudi nyumbani ila tunajiuliza utaanzaje na kama ukuwa mtoto wa vingunge walio kwenye system miaka nenda miaka rudi ataukiwa na kajielimu chako lakini kama una line utajuta bora uhazilikie huku ughaibuni ambapo kazi ni kazi kuliko huko kwa wajuaji wa kuhoji utasikia yule anabeba box kesho yake mtu huyo huyo anakupigia simu kaka naomba unitumie dolla mia,wabongo badilikeni hicho chuo cha hmlimani kilianza mia ya sabini utataka kuifananisha elimu yako au uje huku akae ofisini na kashaada chako cha hapo hawa vyuo wameanza toka karne ya 17 na 18 fikiri hao maprofesa wako wangapi hapa huku hata gardener lazima awe shahada,msiwe mnachagua kazi na kuropoka hovywo wakati tupo mbali mno kwa kila kitu.
ReplyDeleteMDAU HOJA YAKO NI NZURI SANA,,ILA UNASHINDWA KUELEWA,KUWA WATANZANIA WOTE WALIOPO NDANI NA NJE YA NCHI HAWAJAWAHI KUITUPA NCHI YAO HATA SIKU MOJA,,HII NCHI INADIDIMIZWA NA VIONGOZI WALA RUSHWA NA MAFISADI,,NA WENGI WAO WENYE ROHO ZA KWA NINI..
ReplyDeleteKWA MFANO MTU UKIWA UNATAKA KUFANYA KITU CHOCHOTE,UKAAMUA KUPITIA KATIKA NJIA ZA HALAL BILA VICHOCHORO,BASI WEWE NDO UTADHURUMIWA,,UTAONEWA,,UTAOMBWA RUSHWA,,NA VITISHO!!!HII INATUFANYA HATA SISI WASOPENDA KUPITIA NJIA ZA VIPANYA TUFANYE HIVYO,,MIMI NAONA WATZ KAMA HUWA TULILAANIWA KWA KUTOTAKA MEMA,,,MTU ANAE PENDA KUPITA NJIA ZA MKATO NDO HUYO ANAEHESHIMIWA NA WALE WANAOOMBA CHOCHOTE HAWAKUMBANI NAE,,ANAWAPA CHOCHOTE WALE AWATAKAO
SIJUI KAMA UNANIELEWA MDAU,,,SIO WATZ WALIOPO NJE WAMEITUPA NCHI YAO,,HATA UKITUMA CHOCHOTE NYUMBANI KWA FAMILIA YAKO,,STILL UNAIJENGA NCHI YAKO.TATIZO LINGINE UKIWA HAPO HOME KAZI HUWEZI KUPATA WANAPEWA WALE KINA FLAN,,NIMESIKIA WATU WENGI WANALALAMIKA KUWA WAMEENDA NYUMBANI NA MASHINE ZAO ZA KAZI AU WENGINE NA UJUZI WAO WAMEPIGWA CHINI,,SASA HAPO UNAFIKIRI MDAU SISI TUFANYE NINI ZAIDI YA HAYO..
MS AHLAM,,,LONDON,
Tumeifanyia nini nchi?? tumetuma hela nyingi saaana kuliko hata Tanzania inayopata kutoka kwa wafadhili. Kila mwaka watu tulio nje tunatuma hela nyingi nyumbani.
ReplyDeleteHuwezi kuona msaada wetu physically ila ukweli tunasaidia sana.
Swali ni kwamba wewe uliyeko nyumbani umeifanyia nini nchi? Tukirudi wote kazi ziko wapi? Kama wewe ni engineer na mimi ni engineer wa fani moja, nikirudi wewe utakosa kazi!!! ni kukupa taarifa tu
Hivi Sumbawanga siku hizi ni mkoa?
Ni vipi tutashawishika kurudi wakati Maofisa wa Serikali wanatumia vyeo vyao kupora mali za raia na kufanya mauaji wakisingiziwa ni majambazi??
ReplyDeleteHABARI NDUGU?NIMEGUSWA SANA NA HII MADA MIMI KAMA MTANZANIA NINAYEISHI NJE.KWANZA KABISA NADHANI WABONGO WENGI WANAOISHI NJE MCHANGO WAO KWA TAIFA NI MKUBWA KULIKO WEWE ULIYEBAKIA HAPA KUTUNZA FAMILIA YAKO,PILI SISI WACHACHE TULIOPO NJE HASA UK TUMEKUWA MSTARI WA MBELE KUSAIDIA SANA NA KUWEKEZA VITEGA UCHUMI NYUMBANI.MDAU LONDON.
ReplyDeleteWengi wenu Wandugu zetu Majuu maisha yenu mnayaendesha bila malengo na mipangilio.
ReplyDeleteNdio maana unakuta mtu anakaa huko anafanya kazi hata kama ni kupiga box akipata pesa anajirusha na anakuwa hana future!
Siku ikitokea anarudishwa nyumbani kwa amri unakuta hana hata kijiko wala Dola $ 1 anarudi yeye na jikaputula lake na li fulana na mara zote watu wa namna hii akifika mtahesabu muda mfupi mtaona amechanganyikiwa ama amekuha taahira na muda si mrefu anafariki!
Majuu muishi kwa malengo bandugu!
Madiaspora mkumbuke ya kuwa:
ReplyDelete1.Ukipanda Mchicha utavuna mchicha!
2.Ukipanda bangi utavuna bangi!
3.Kosa lolote ukifanya maishani mwako litakuja kuakisi ktk maisha yako ya baadae!
Kama mnavyoona ktk Maduka pana Picha inayoonyesha Katuni ya watu wawili mmoja mnene mwingine mwembamba:
Mnene : I sold on Cash,
Mwembamba: I sold on Credit,
Muishi Majuu kwa kujipanga, pia
Tazameni dunia inavyokwenda!
Maendeleo?
ReplyDeleteSuala la maendeleo nchini ndio ilikuwa kisingizio eti hamtaki kurudi nyumbani hakuna maendeleo!
Sasa bandugu mnafikiri nani ataleta maendeleo kama sio ninyi?
Kama mnalalamika Ufisadi, mnafikiri nani atawaondolea hao Mafisadi kama sio ninyi Wasomi Majuu mkirudi Tanzania na kutoa ushindani ktk mchakato wa kuwapata Viongozi bora?
Sasa mnaona kukaa kwenu nje huku mkiwa mnavyo vigezo vya Taaluma mmevikalia mnakuta nafasi zinashikwa na watu Mafisadi na wasio stahili kabisa!
Sasa imetosha Madisapora huko Majuu, mmekwisha mtumikia Kafiri vya kutosha na huu ni muda wa kuja kutumika Nyumbani Tanzania!
ReplyDeleteMambo hunda kwa nyakati Mfano Industrial Revolution Mzungu alikuja tafuta malighafi Afrika na Watumwa miaka ile 1800 hukoo, lakini baadae miaka ya 1900 hawakuwa wanakuja na ninyi mmekuwa mkienda huko kuomba kazi kama Ubaharia na kubeba mi box hiyo.
Mambo yamebadilika Duniani, sasa imekuwa hakuna kwenda Majuu hivi sasa Fasheni kwenda Machini-Yaani Afrika!
Sasa ni zamu ya Afrika na kama mlivyosikia:
1.MSUMBIJI-Hivi karibuni kumeripotiwa wimbi kubwa la Raia wa Ureno wakija kujikita kimaisha baada ya kuuza Majumba yao na kuchukua akiba zao Mabenki kwao Ulaya wanakuja kimaisha moja kwa moja.
2.ANGOLA-Vivyo hivyo kuna wimbi kubwa la Wareno kutoka Majuu kwao Portugal wanakuja kuanza maisha na kuweka maisha kwa makao ya kudumu.
3.TANZANIA-Kuna kasi kubwa ya wahamiaji mfano Sensa tuliyofanya mwezi uliopita imekadiriwa na Mashirikisho kama UN, World Bank na IMF kuwa na ingezeko la wastani wa 33% la kukua kwa idadi ya watu kutokea 45 Milioni kabla ya Sensa ina maana panakadiriwa ongezeko la watu 14,850,000 na kuwa idadi itakuwa 59,850,000 ambapo chanzo kitakuwa birth rate na wahamiaji (ikijumuisha halali na haramu).
WANDUGU CHANGAMOTO NI KUBWA KAMA MTACHELEWA MTAWEZA KUKUTA WACHINA NA WAHINDI WAMESHIKA NA KUHODHI NAFASI ZENU HUKU TANZANIA,,,SASA HAPO NI NANI WA KULAUMIWA?
Kasi ya maendeleo nchini hiyooo!
ReplyDeleteWIMBO WA KIZALENDO:
1.Neema neema neema imefunguliwa!
Gas huku Tanzani imezidi onekana!
2.Neema neema neema imefunguliwa!
Mafuta huku Tanzania yanalekeaa!
3.Neema neem neema imefunguliwa!
Kasi ya kukua uchumi imeonekanaa!
Utumwa Majuu sasa basi!,,,bandugu huko Ulaya na Marekani ni wakati wa kurudi nyumbani Tanzania mmeona 'Treni la mwisho' atakaye chelewa shauri zake!
Bongo inazidi kuwa Tambarale!!!
ReplyDeleteWimbi la kasi ya maendeleo nchini Tanzania na mimali tuliyo thibitika kuipata Gesi, Mafuta, Urani, Chuma na Bati,,,nani atataka asiitwe Mtanzania?,,,ebo?
Pana umhimu wa kuongeza kasi ktk zoezi la vitambulisho vya Uraia na Ukazi kwa Wageni na Wakimbizi nchini ili tufahamiane na tuweze kudhibitiana, ama sivyo rasilimali hizo pamoja na ongezeko la kasi la idadi ya watu nchini zinaweza zisitusaidie kwa vile tutahudumia Wageni wasio stahili kwa rasilimali zetu na kuwaacha Wakonongo kamili!
Pana kila dalili ongezeko la 33% litakuwa limezaliwa na Wahamiaji haramu badala ya kiwango chetu cha kasi ya uzazi!
Watanzania eeeeeeeeeeeeeee!!!!
ReplyDeleteKumekuchaaaaaa!!!
Huko Majuu bwageni miboksi chini kutoka vichwani na migongoni mwenu mtoke mbio kurudi TANZANIA!
Habari ndio hiyo Bongo Sasa Maziwa kwa Asali sahuri zenu chelewa chelewa utamkuta mwana si wako!
Nugu yangu nashukuru sana kwa mawazo yako lakini kuna kitu kimoja naona huelewi.Sisi tunaoishi nje ya nchi tunafanya vitu vingi ambavyo wengi waliopo hapo nyumbani hawafanyi.Sisi tunatuma pesa kwa ndugu zetu kila wakati ili wajikimu kimaisha,tunajenga nyumba, tunanunua mashamba na pesa zetu ndio zinazolipa kodi ambayo inatumika kutengeneza hizo barabara na mashule. Suala la kurudi ni hiari ya mtu,na pia sio kwa sababu wewe upo nyumbani basi kila mtu arudi huko tutakuwa kama wendawazimu.Nikuulize swali,je wasomi wote wlioko nje wakiamua kurudi nyumbani watapata ajira na kulipwa kiasi cha pesa wanacholipwa huku nje?Jaribu kufanya utafiti nakujua ni kiasi gani pesa zinazotoka nje kuja kwa ndugu zao zinakusanywa kwa mwaka?Hongera kwa kubaki nyumbani lakini jua kuwa tuko pamoja nawe tunaijenga nchi yetu sio kwa kukaa bongo ila kwa kuipatia pesa za kigeni serikali na kuzisaidia familia zetu.
ReplyDeleteMbona hakuna jipya naona yote ni marudio yaleyale tu? Mimi nnachotaka nchi yetu ibadilike na watu wapate haki zao za muhimu! Hapa nnapoishi mimi kila mtu asiye na kazi mradi anaishi kihalali, awe raia wa hapa au mgeni au mkimbizi. Kila mwisho wa mwezi anapokea mshahara wake ili aweze kuishi na kupata mahitaji ya kibinadamu. Zaidi ya hapo unapewa nyumba na serikali inakulipia kila mwezi! Sasa hapo nyumbani nani anaweza kufanya jambo kama hilo kwa watu wake na wageni? Tunachokiona kila siku ni masikini ambao ndio wengi kupita hao ambao wanaiba pesa, wanahangaika kutafuta mlo wa siku moja tu, na wala hawajui wataupata wapi! Sasa ndugu yangu we umepata bahati kuwa muhandisi shukuru kwa hilo! Kuna watu hawajui hata maana ya neno hilo! Sasa mtu bila kuiba hapo nyumbani au kupokea rushwa hawezi kuishi! Maisha yakibadilika kwa jambo hilo hapo nyumbani mimi ntakuja kuwekeza katika yote nnayopata huku. Niliwahi kuleta Conteiner langu na mizigo wakati wa sabasaba nilifika mwezi wa kwanza mpaka sabasaba ilifika sikulitoa! Niliamua kuliacha huku nikiwa nimeshakipia maonyesho yote! Sijawahi kuona nchi kama hiyo.
ReplyDeleteMKITAKA TULIO KUA ULAYA NA MAREKANI TURUDI...WAPENI WAPINZANI NCHI WAIONGGOZE KWANZA.
ReplyDeleteMTAENDA KUTUONEA DONGE TU TULIOKUA MAJUU.NA UKIZINGATIA VISA ZILIVYOBANWA SASA HIVI..HAMTAWAHI KUPAGUSA MAJUU NG'0 MBAKI WENYEWE NA VUMBI LENU PLUS UFISADI
mie nakuwa mkweli,nikisaidia nitasaidia kidogo na 70% percent nitasaidia jamii niliyopo ambayo inanionyesha daily hela inapokwenda free medical care and education,good infrastuctures etc well kama huna ndugu nje imekula kwako,wanadiaspora wanachangia pato la taifa kwa kusaidia ndugu zao!by the way uzalendo ni myth lol nashangaa mnakaaa vibarazani kupiga umbea likija swala la maendeleo basi watazania waishio nje ndio waonyeshe uzalendo,sitatuma hela yangu ng'o kwa yeyote muitafune vizuri maana mmeitafuna nchi imeoza...yaani mtu kufanya kazi TRA tayari ni kibosile...tayari anahesabika anakula kny kamba ndefu..nyie wenyewe mliopo hapo kila mtu anawazia tumbo lake tu....hatutaendelea kamwe kwa mentality za aina hii.....
ReplyDeleteWananchi wa Tanzania bado wanaishi miaka 20 ishirini ya nyuma itachukua muda mrefu kuwa na maendeleo.
ReplyDeleteKimfaacho mtu chake:
ReplyDeleteBANDUGU HUKO MAJUU MASHARIKI YA MBALI JAPAN, ASUTRALIA ,ULAYA NA MAREKANI,
RUDINI MJE KUPANDA MATRENI NA MABASI YA KASI MLIYOANDALIWA KWA KODI YENU NA VIONGOZI WENU BABA NYERERE ALIYEWEKA MSINGI, MZEE MWINYI, MHE. BEN MKAPA NA SASA NDUGU YETU MHE. JK !
ACHANENI KABISA NA VITU VYA WENYEWE HUKO VYA MANYANASO UNAPANDA TRENI AU CHOMBO CHA USAFIRI YANAKUTOKEA MOJA YA HAYA HAPA:
1.ABIRIA WENZAKO WEUPE WANAKUACHIA KITI UNAKAA PEKE YAKO!
2.KILA ABIRIA MWEUPE ANAKUWA NA TAHADHARI KWA UWEPO WAKO EWE MTU MWEUSI NDANI YA CHOMBO!
3.ABIRIA KARIBU CHOMBO KIZIMA WANAKUKODOLEA MIMACHO NA WENGINE WANAKUANGALIA KWA KEJELI NA DHARAU!
HARUFU KUBWA YA UBAGUZI WA RANGI INANUKIA KWA NUKUU HIZO 3 JUU.
HIZI ZOTE 3 NI DALILI ZA AKUFUKUZAYE HAKWAMBII TOKA
YA NINI MTESEKE NA VYA WENGINE HUKU MKIBAGULIWA?
Madiaspora Majuu>
ReplyDeleteHamuoni raha kwa Treni au Basi la Kasi kwa safari ya Manzese-Posta au Mbagala Rangi 3-Posta mkiwa nyumbani kwa Bi.Mkubwa na Babu nchini Tanzania Bongo Tambarale?
Ya nini kunyanyasika kwa Treni ya Chini ya Ardhi ya London-Belfast ama Treni ya Boston-New York?
Mdau wa 27 hapo juu Anony wa Fri Sep 14, 05:44:00 AM 2012
ReplyDeleteKumbuka:
MAN and DEVELOPMENT, must be MAN FACED WITH CHALLENGE!
Unafikiri maendeleo yanakuja kama mvua au muujiza?
Zinduka, maendeleo yanatafutwa tena ni ajabu penye changamoto ndio kasi ya maendeleo na ufanisi vinapatikana.
Angalia mifano ya nchi 3 hizi:
1.UJERUMANI:
Baada ya vita kuu ya Pili ilikuwa masikini wa kutupwa sasa nagalia sasa ipo wapi?
2.JAPAN:
Baada ya kupigwa bomu la Atomiki na Marekani ilipondeka pondeka na sasa ipo wapi?
3.CHINA:
Iliyochomoka miaka ya 1980-1990 kutokea kwenye Ukomunisti na Ujamaa sasa iko wapi?
Wewe unafikiri maendeleo hayo ya hiyo miaka 20 mbele ataleta nani kama sio Watanzania wote pamoja na wewe?
Ni kweli kabisa mdau wa 30 hapo juu,
ReplyDeleteMfano mojawapo ya Challenge au Changamoto iliyo mbele yetu kuyafikia maendeleo ni kuvunja ukuta wa Mafisadi ili tuweze kuyafikia maendeleo na vingine pia!
Na sio kulaumiana kamwe maendeleo hayapatikani kwa kurushiana lawama kama Wamajuu wanavyofanya!