January Makamba ndani ya studio za Magic FM akihojiwa na Fina Mango
  Mheshimiwa January Makamba akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na Fina Mango
Fina na January Makamba baada ya kipindi cha Makutano
----
Mbunge wa Bumbuli na  Naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia Mhe January Makamba amesema hana mpango wa kugombea Urais. Makamba aliyasema hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango. Alisema anaamini nafasi ya urais inahitaji mtu ambaye amejiandaa Kisaikolojia, Kisiasa na Kifikra na kumalizia kwa kusema kuwa Urais sio uamuzi wa mtu mmoja kwa sababu nchi haiendeshwi na mtu mmoja na inahitaji watu ambao wanashauriana, kuandaa dira ya pamoja na kupeleka ujumbe wa kuwaunganisha Watanzania.

 Alipoulizwa Rais anayekuja anatakiwa aweje alisema anatakiwa awe ni mtu atakaewaunganisha Watanzania huku akisema mianya ya ukabila, udini na rushwa ambayo baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliitaja imeanza kuonekana. Pia Makamba alisema rais ajaye anatakiwa asiwe mtu mwenye hulka ya visasi na atakiwa  awe na uwezo wa kuwaambia wananchi kuwa yeye sio masiha wa kuyafanya maisha yao yabadilike papo kwa hapo kwa kuwa nchi ni ya watu wote, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutumia nafasi yake kuleta mabadiliko

Alipoulizwa katika wanasiasa wa upinzani ni yupi anamkubali, alimtaja Zitto Kabwe kwa sababu ana uwezo wa kusema na kusimamia kile anachokiamini, ujasiri wa kuomba ushauri kama kuna jambo ambalo halielewi na pia anapenda kusoma na kujifunza. Pia alitaja kuwa anamheshimu sana Profesa Ibrahim Lipumba.

Mheshimiwa Makamba  alimalizia kwa kusema kuwa atagombea ubunge wa Bumbuli kwa kipindi cha pili na baada ya hapo atajikita katika shughuli za Shirika la Maendeleo ya Bumbuli (Bumbuli Development Corporation) alilolianzisha likiwa na lengo la kuleta washirika wa maendeleo ili kuwawezesha kiuchumi wananchi bila kutegemea miradi ya serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. JANUARY OYEEEE, OYEEEEEE

    ReplyDelete
  2. Sasa ni zamu ya Mgosi naye Uraisi!

    Janury Makamba now is your time, we want you!

    ReplyDelete
  3. Sawa Kiongozi hata kama hutagombea Uraisi msimu huu, hatukubali ungali mdogo na umri wako unaruhusu kipindi kijacho,,,PIGA JALAMBA UJIANDAE KWA AWAMU ZIJAZO TUMEONA UTENDAJI WAKO,TUMEONA MSIMAMO WAKO,TUNAKUAMINI NA TUNAKUTEGEMEA !

    Ahsante sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...