Waisiamu kutoka maeneo mbali bali ya jijini Dar es Salaam wakishiriki katika maandamano ya kuelekea Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kupatiwa ufumbuzi  juu ya kamata kamata ya Jeshi la Polisi dhidi ya waisilamu waliokataa kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi. Wameendelea na msimamo wao wa kupingwa kukamatwa wanaokataa kuhesabiwa Sensa.Jeshi la Polisi limekubali kuwaachia huru waislamu wote waliokamatwa.Waislamu watangaza ushindi, wasema Bado Mkuu wa baraza la Mitihani Joyce Ndalichako ajiandae na maandamano ya  namna hiyo hadi ofisini kwake na baadae Bakwata wanayotaka ifutwe. Muda huu wapo hapa Msikiti Kichangani,Magomeni wanapanga Mkakati wa kuandaa maandamano mengine.
Mabango yenye maelezo tofauti tofauti.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiwa yamefika nje ya Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani.
Waislamu wakiswali sala ya L'aasiri, mbele ya Wizara ya mambo ya ndani wakati wakisubiri viongozi wao waliokwenda kuzungumza na jeshi la polisi ili kupata ufumbuzi wa juu ya kamata kamata ya jeshi la polisi dhidi ya waisilamu wanaokataa kuhesabiwa.
Mmoja wa Waislam akiwa amenyanyuliwa juu juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. akili zingine..Jamani, hata Mungu si anasema tuiheshimu serikali iliyowekwa madarakani. Kuhesabiwa ni kwa faida ya watanzania wote..iweje watu wengine wakwamishe maendeleo kwa ajili ya ubumbuwazi wao..kuhesabiwa ni muhimu..hii ni desturi ya dunia nzima ili kuthamini watu na kutathimini maendeleo..badilikeni ndugu zetu..mnaiabisha nchi yetu kwa kufanya madudu ya chekechea. Nakumbuka madaktari walipokuwa wanapita mashuleni kutoa chanzo ya surua na polio tukiwa shule ya msingi watu walikuwa wanavumisha kuwa wanataka kutunyonya damu. Leo ni karne ya 21, watu hawataki kuhesabiwa, jamani tutumie utashi tuliopewa na Allah

    ReplyDelete
  2. Kwa nini serikali iwalazimishe watu kuhesabiwa, Is it a law of the country inayosema mtu lazima ahesabiwe na asipohesabiwa achukuliwe hatua za kisheria. Naomba nielekezwe kwa anaefahamu ? Au kama kuna reference website naweza kwenda nikaangalia.Sio swala la udini ni swala la sensa ninalouliza. Mdau usa

    ReplyDelete
  3. Mimi naona kama watu wangekuwa wanahesabiwa kisha labda kuna kitu flani watapewa,,hapo sawa,,lakini kusumbua mtu eti unamuhesabu,na toka azaliwe na akulie hapo katika nchi yake hajawahi kukonga mtu mlango eti amemletea kipato flan kilichotokana na mapato ya nchi yake,,labda enzi zile za UNGA WA YANGA,KWENDA DUKANI MPAKA UWE NA CARD.
    Mtu unakuja kusumbuliwa eti unahesabiwa what for?,,
    Mimi nimeipenda hiyo,na nahisi hao waliopanga hicho kitu walifocus mbali sana!!!Na nafikiri kweli sio tu kuhesabiwa!!!,,Ni Uonevu uliokithiri,,Na Inajulikana wazi kuwa Wajinga wasosoma,,na masikini wakubwa ni WAISLAM!Na kama wangeliona hili wakaanza maandamo hayo toka zamani,,sasa hivi tungekuwa mbali,,Haya ni maandamano ya amani wala sio vita,,
    Mwenyezi Mungu Akuongozeni Ndugu zangu
    Ijuma'a Kareem

    ReplyDelete
  4. Wewe anonym wakwanza wacha ujinga wako.Usiwatukane watu kwa maoni yako yakipuuzi.Mungu anaesema uiheshimu serikali ni Mungu wako ww sio wa watu wote.Ktk uislam serikali inayopaswa kuheshimiwa ni ile inayoongoza watu kwa mujibu wa sheria alizoziweka Mungu mwenywe na sio kila serikali tu.Wacha umbumbumbu wako km huna lakusema kaa kimya mlemavu wa mawazo na fikra ww.

    ReplyDelete
  5. MTOA MAONI WA KWANZA KABISA......jaribu kuwa katika dunia hii ya leo usitowe lawama za kipumbavu, hili kosa kwanza ujuwe nilaserikali wenyewe huwezi kumkamata mtu ukamuweka ndani kwa sababu ati kakataa sensa wakati hio serikali haina mipangilio na raia wake

    kwani kama unataka kumjuwa mtoto wako siku ya kuzaliwa tu unampa jina ...sasa leo hii ndani ya serikali hii hii ya nchi yetu mtu anazaliwa mpaka anakufa hutaki kumpa ID yake au passport kumtambulisha kuwa huyu ni raia wako ati leo unamuweka ndani kwa kukataa kuhesabiwa

    ujuwe vyema kuwa nchi zote duniani hakuna hii kitu sensa ya kijinga ila serikali zote zinajuwa takwimu ya watu wake wote wawe waislam au wakristo na wahamiaji wote kwanini basi ...nikuwa mtu anapotaka haki yake ya ID unampa na hapa ndio wewe kama serikali unapata kujuwa hio takwimu ya watu wako

    sasa wewe mdau wa mwanzo kabisa hapo juu usitowe lawama za kitoto na kijinga wakati hujatembea kwa watu ukaona mipangilio ya kujali raia wao

    wewe leo tanzania hii nenda kaombe passport utazame utadhani unaomba pepo na mapesa juu kukutoka wakati hii ilikuwa wewe ni haki yako ....unaomba pass unaulizwa unakwenda wapi , tuletee ticket hivi vitu ni vyakijinga kabisa haya masuala yote ya nini wakati mimi ni raia wa hii nchi na je kuna kitu gani mimi chakujitmbulisha kuwa ni mtanzania hapa, ukisema lugha ya kiswahili hii sio ID yangu mimi hata wazungu wanazungumza kiswahili

    sasa wewe mtoa maoni wa juu hapo usituletee PUMBA kwanye huu mtandao hapa kwanza jifunze kujuwa HAKI yako kama mtanzania usiwatupie lawama wanaodai haki zao za kimsingi huwezi kumueka ndani raia ati kakataa kumuhesabu je umesahau siku aliokuja uhamiaji akaomba pass na wewe hata fomu hukumpatia

    uwe na uweleo wa kimantiki ndio uweze kuchangia mada kama hii kwani sisi tuliosafiri tunajuwa shida gani inatupata tukitaka haki yetu hapa kwetu, na MIMI BINAFSI SIKUBALIANI NA HILI LA KUWAWEKA NDANI WATU ATI SENSA ....na musipoangalia vizuri kweli hizi vurugu zitamwaga damu

    ReplyDelete
  6. Swali langu ni moja tu siku zote tumekuwa tukihesabiwa bila mgomo what exactly happened mpaka sensa ya mwaka huu igomewe naombeni tu mnijuze.

    ReplyDelete
  7. Ujinga mtupu, sensa nikujua wa tz tuko wangapi ili serikali ipange bajeti, udini wekenini mbali ,kwani ukweli wa dini tz uko wazi na kila m2 anajua,na sio tatizo,jamani waislamu mbona mnadai mnaonewa?, lakini bongo mm naona hakuna anaeonewa kila m2 yuko free, uclete machafuko ss sote wabongo, kesho wakirustu nao wataanza kujibu mapigo then itakua balaa lakini ukweli ni mmoja ss sote ni wamoja haonewi m2, fuata dini yako asietaka kua muislamu muache na unakari wake,je ingekua ww unalazimishwa kuatofuata imani yako je utakubali?ukirustu au uislamu sio tanzania,tz ni uislamu na ukiristu na makifri pia.tujifunze mengine sio dini tu,kwani dini zote zina historia mbaya kwa m2 mweusi mpaka leo,ukienda ktk baadhi ya makanisa au misikiti ,hasa siria wanakuashangaa nakusema ondoka ww unajua wapi dini ww? wao walioanzisha dini hizi kwao poa ss ndo tunauana,jamani chonde chonde, nenda na imani yako middle east ilipoanza dini hizi kama kuna m2 atakuckiliza especially ukiwa mweusi,jamani mm nimeyaona kwa macho inauma sana, na ujinga huu tunaotaka kuuleta hapo bongo duh,sema saingine ni poa heshima haiji bila ncha ya upanga ,2chinjane then mtemi atatoa amri.allah akbar

    ReplyDelete
  8. Mungu Ibariki Tanzania. watanzania waislam kwa wakristo, tunaenda wapi? suala litabaki ref: "Akili Zingine"
    Issa Michuzi, tusaidie elimu ya uelewa ya mambo ya dini na kijamii tuokoe hii Tanzania

    ReplyDelete
  9. nachangia tu, sio kweli kwamba nchi zote duniani hakuna sensa kama wadau wachache walivyochangia huku.
    Sisi tupo huku ughaibuni tunahesabiwa pia. kumbuka vi vigumu kwa serikali yoyote kuwa na record kamilifu kwa muda wote, hata kama wanatoa ID.kuna mambo mengi yanayosababisha hali hiyo.

    swala hapa polisi isiwakamate watu kama sheria hiyo haipo, kama hipo basi sisi waisilamu tupiganie pia hiyo sheria iondolewe.

    ReplyDelete
  10. ngombe ndio wanahesabiwa lakini binadamu hawahesabiwi kama fungu la dagaa

    wenzetu nchi zilizoendelea wanajuwa idadi wa raia wake kupitia sehemu kama ofisi ya uzazi na vifo

    leo hii mtu akijipeleka uzazi na vifo kuomba cheti chake za kuzaliwa basi atasumbuliwa utasema anaomba msaada wa chakula

    nchi zote duniani zinatoa vitambulisho kwa raia wake tokea siku wanapozaliwa iweje leo hii mnataka kuwahesabu watu kama magunia ya mkaa

    serikali mmechemsha 2015 sio mbali tutahakikisha tunawapiga chini kwa nguvu zote na uwezo wa mungu.

    ReplyDelete
  11. Ndugu zangu kuna mambo mengine unaangalia unaacha tuu ndio maana mzungu alikuja akatutawala na mwarabu akatufanya kuwa watumwa ,naomba ni waulize haoo ndugu zangu waislam kuhusebiwa kunahasara ghani,au mtu kuku uliza wewe ni wadini ghani kuna kosa ghani ,yaani nashangaa watu wazima wengine wamesoma wanjiusisha katika kudanganya jamii yaani ndio maan mzungu na mwarabu walitutawala sababu ya upumbavu na ujinga wa watu wasiokuwanafikira wala kuona mbele ningependa kuwaambia waislam serikari haina dini dini ni yako mwenyewe na dini ya serikari ni sheria na katiba mambo ya misikiti na makanisa ni yako tuu wewe kiumbe kwa hiyo hapa nawaomba waislaam wezangu muamke msiwe nyuma kila siku kwa mambo yasiyo na maana kuhesabiwa ni jambo la maana sana katika utendaji wa serikari na upangiliaji wa maendeleo ya nchi na kuweza kufanya huduma zote za jamii zinawafikia wananchi, bwana michuzi asante sana tuko na kazi kweli .
    kila siku ni hoja za kipumbavu tuu wakristu mbona hawajakataa nahata uko dini ilikotoka mbona uwa wanahesabu je sisi ni wakinanani ?waislaam tusipende kudanganywa na wanao jifanya wanajuwa kumbe wanapotosha,asante

    ReplyDelete
  12. Naomba ieleweke kuwa Waislam hawajakataa kuhesabiwa, waislam wanafahamu umuhimu Wa kuhesabiwa toka enzi enzi. Wanacholalamika ni upotoshaji Wa takwimu za idadi yao dhidi Ya Dini nyingine hali inayopelekewa kukosekana kwa huduma wanazohitaji.

    ReplyDelete
  13. Mwarabu hawakuwa na watumwa. Waafrika wenyewe walikuwa na watumwa baada ya vita vya makabila na majimbo. Ndio hao walikuwa wanawauza kupata Chumvi, shanga, na nguo, na baadae bunduki za kupigania. Someni historia ya ukweli. Watumwa wengi waliuzwa na machifu waliowamiliki. Mtumishi wa nyumbani kwako ulimpataje, unampeleka shule kama watoto wako. Huo si utumwa. Ule ulikuwa ni wakati ambao utumwa ulikuwa ndio biashara, Mwarabu alikuwa anawauzia mapadri waliokuja kueneza ukristo kumbe walikuwa na ajenda nyingine za siri. Watumwa wengi walipelekwa marekani na carribean. Hivi huko Uarabuni mmeshasikia kuna African-Arabs?

    ReplyDelete
  14. Kwa nini suala la kuhesabu wanadini lisiwepo? Kuna tatizo gani, tunaogopa nini? Why all this. Iko namna. Matatizo mengi yanaletwa na hawa watu kwa nini tujiulize, wanaogopa. Wenzetu makanisani huwezi kuwa mwana kanisa bila ya kujiandikisha katika kanisa na ujulikane, zamani kule nyumbani wengi waliokwenda kubatizwa wako katika daftari na wengi ndio vyeti vya ubatizo ndio vyeti vyao vya kuzaliwa vyao mpaka leo.

    ReplyDelete
  15. jamani ya Mungu mpe Mungu na ya khaisari mwachie khaisari hata Yesu alipo ulizwa alijibu hivyo kwaiyo mambo ya kidini ni ya kidini na mambo ya kiserikari ni ya kiserikari viongozi wa dini siku hizi wana acha mambo ya kuwaongoza wahumini wao nao wamekuwa wanasiasa tena wakununuliwa na wanasiasa sasa tunapokwenda dini ndizo zinazotaka kutawala badala ya utawala wa sheria unao angalia watu wote, sote tupo kwenye boti moja ikizama hakuna atakaye pona so nilazima tuishi kwa kueshimu sheria na kueshimiana, waislamu walimsaidia nyerere kupata uhuru lakini nyerere alituongoza watu kwa kueshimiana na wazee wetu waliishi ivyo leo hii njaa ya madalaka ndiyo inayo tufikisha huku hasa kwa wanasiasa kuahidi ahadi ambazo ni batili na zingine wamediliki kuwaahidi hata viongozi wa kidini ndipo tulipo fikia leo hii.. Mungu ibariki afrika Mungu ibariki Tanzania..

    ReplyDelete
  16. MADAI YALIKUWA KUACHIWA WALIOKAMATWA KWA KUKIUKA SHERIA YA SENSA! NA SERIKALI KWAKUTAMBUA SHERIA IMEKIUKWA, MAKUSUDI INAWAACHIA HURU!!!! DAI LINGINE LIKAJA.."TUNATAKA NDALICHAKO AFUKUZWE KAZI" KESHO NA KESHOKUTWA WATADAI MAJAMBAZI NA WABAKAJI WA KIISLAMU WAACHIWE HURU KISA2 NI WAISLAMU!!! HUU NI UPOTOFU WA MAADILI YA KIUTAWALA NA NI JAMBO HATARI SANA KWA AMANI YA NCHI.....KUMBUKENI TU KUWA UKIONA KOBE KAINAMA....JUA KWAMBA ANATUNGA SHERIA....KAZI KWENU

    ReplyDelete
  17. jiulize kwanini wewe unataka kipengele cha wewe ni dini gani?ukipata jibu zaidi yakutaka kujua wakristo na waislamu nani wengi apa tz,hei nasikia harufu ya vita.usipo jua nyumbani kwako mpo wangapi unaweza nunua chakula cha kutosha idadi usio ijua?sensa ya kwanza mbona tuliesabiwa wote,thats means dini umebadilika now nakusema tusiesabiwe?jipende wewe pia natanzania yako,muslim and chrstian cme from abroad babu na babu zetu waleeeee ndo wanamajibu ya dini izi.

    ReplyDelete
  18. mimi naiyomba serikali kwamba kwanza ilikuwa ifanikishe zoezi lake la ID kwa raia wake wote na ndio njia hiyo pia itatumika kujua idadi ya watu wake waliopo duniani zaidi ya hapo ugumu utakuwepo kutokana na maendeleo ya dunia ya kila siku ujuwe vipofu nao wanelimika kiaina fulani serikali isitegemee kuona kila kukicha watu watakuwa wamelala kitu hicho hakipo tena,mungu ibariki TANZANIA na WATU WAKE, AMIN

    ReplyDelete
  19. Watanzania tuache Ujinga! Tufikirie mambo yenye tija kwa familia zetu na Nchi yetu. Mdomo mdomo mdomo maendeleo ziiii! Fikiria na tenda kimkakati maendeleo. Uhasama uhasama hatusongi. Fikiria na tenda Chanyaaaa!

    ReplyDelete
  20. KUNA KITU KINATUNYEMELEA MWALIMU ALISEMA TANZANIA SI KISAWA HAYO TUNAYOSIKIA KWA WENZETU NASI YATUHUSU SASA NAHISI MUDA UMEFIKA JAMBO SI JAMBO MAANDAMANO ,KUNUNA, KUTUKANANA NDO TANZANIA YA LEO TANZANIA YA LEO HAYA YANAWEZEKANA TUTAONA MWISHO WAKE KWA ATAKAE JALAIWA

    ReplyDelete
  21. Jamani..hivi watu hapa wamezaliwa lini? Maana hii sio sensa ya kwanza Tanzania...1988...2000 na kuendelea. Serikali zote duniani zina fanya sensa kwahiyo nyie mnaosema ni Tanzania tu nadhani inabidi kuangalia kwanza kabla ya kuongea ndio mwana filosofa mmoja alisema "No Research no Right to speak" Jifunzeni kutafuta habari kwanza kabla ya kuongea ita saidia kuongea vitu vya maana mbele ya watu. Sasa kama wananchi hawataki kuhesabiwa..Serikali itajua vipi wapi kujenga shule, wapi kuongeza hospitali..wapi kuongeza huduma nyingine za jamii? Jamani tujifunze kufikiri na kurisechi mambo. Information is power tusirukie mambo katika misingi ya udini..Kisha hapa mtu anakuja anasema waislam tuko nyuma kimaendeleo? Ni kwa sababu hizi hizi ndio maana katika maeneo hayo kutakua hakuna shule za kutosha,walimu wakutosha, huduma za afya, maji ma maengine mengi...Wazaai wangu wametoka dini zote mbili kwahiso sipendelei kokote..Mungu ibariki Tanzania,watu wake na viongozi wake!

    ReplyDelete
  22. Badala wa andamane Mafisadi Wapigwe chini...Wana andamana kukamatwa kwa walio kataa kuhesabiwa. Solidarity hiyo Mngeionyesha kwenye Mambo Mengine Muhimu. Mnafikiri Nchi inaongozwa na Mtu wa dini tofauti? na Je Jeshi La Polisi Ngazi zote Kubwa Ni dini hiyo hiyo..Unafikiri kwa nini Wamewakamata? Ili M Amke na Mpeleke watoto wenu shule na sio Madrasa tu. Na pia msiwa Ozeshe mabinti wenu wakiwa Angali wadogo-Wapelekeni shule, Then Watajua nini Umuhimu Wa sensa For Community Development and Planning_Sio Ushabiki wa dini tu wakati wengi hapo wazinzi..Mdau, Mu Islam anaependa Changes Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...