Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkaribisha Makamo Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Watu wa China  Mhe. Hui Liangyu,mara alipowasili Ikulu Mjini Zanzibar
 Waziri wa Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Omar Yussuf Mzee,kwa Upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitiliana saini   Mkataba   wa  Mashirikiano ya Kiuchumi  na Kiufundi,na Naibu Waziri wa Biashara wa China ZHONG SHAN,kwa Upande wa jamhuri ya Watu wa China,katika mashirikiano hayo Zanzibar itapatiwa RMB 60 Milioni sawa na Fedha za Tanzania 14,8 Bilioni,ambapo fedha hizi ziatatumika katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.
Waziri wa Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee,kwa Upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akibadilishana  Mikataba baada ya kutiana saini Mashirikiano ya Kiuchumi  na Kiufundi,na Naibu Waziri wa Biashara wa China ZHONG SHAN,kwa Upande wa jamhuri ya Watu wa China,katika mashirikiano hayo Zanzibar itapatiwa RMB 60 Milioni sawa na Fedha za Tanzania 14,8 Bilioni,ambapo fedha hizi ziatatumika katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo. Picha na Ramadhan Othman, Ikulu Zanzibar
==========================

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China leo zimetiliana saini Mkataba juu ya Mashirikiano ya Kiuchumi na Kiufundi ambapo Zanzibar itapatiwa jumla ya RMB 60 Millioni sawa na TZS,14.8 BILLIONI.
Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Waziri wa Nchi Fedha ,Uchumi na Mipango ya Maendelro Omar Yussuf Mzee ndie alietia saini na kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Naibu Waziri wa Biashara Zhong Shan ndie alietiana saini ambapo ulishuhudiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sief Ali Idd na kwa upande wa China Naibu Waziri Mkuu wa nchi Hui Liangyu.
Kwa mujibu wa Mkataba huo wa Mashirikiano Zanzibar itafaidika katika Ujenzi wa Majengo mapya na Ukarabati mkubwa wa Majengo yaliopo katika Hospitali ya Abdulla Mzee ..Pia Ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Mwananakwerekwe.Halkadhalika Zanzibar itafaidika katika utiaji wa Taa za Barabarani zitakazotumia Nishati ya jua katika baadhi ya Barabara kuu za Mjini.
Aidha Mkataba huo unaelezea kuwa Zanzibar itapata Mafunzo Mafupi na Marefu katika Fani tofauti ambayo itapendekezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar . Mbali na hayo pia  kutakuwapo Uchimbaji wa Visima vya Maji pamoja na maeneo mengine ambayo Nchi mbili zitakubaliana.
 Pia ujumbe huo wa China  umetiliana saini na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya msaada wa Wataalamu wanne(4) kutoka China ambao watakuwepo Zanzibar kwa miaka miwili(2) ambao watawafundisha Mafundi wa Mitambo wa Studio yakurushia matangazo ya Redio pamoja na kutoa Vifaa mbali mbali kwa ajili ya Studio hiyo.
Ujumbe huo  wa China ukiongozwa na Naibu Waziri Mkuu  uliwasili Zanzibar leo jioni na kupokelewa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwamo Mawaziri. Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu pamoja na maofisa mbali mbali wa Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein jioni hiyo hiyo alikuwa na Mazungumzo na  Naibu Waziri Mkuu wa China Hui Liangyu Ikulu ambapo walizungumzia juu ya Ushirikiano kati ya Nchi  zao.
Usiku huu Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi  Seif Ali Idd Amemuandalia Chakula Naibu Waziri Mkuu wa China  pamoja na ujumbe wake huko katika hoteli ya Lagemma Nungwi.
Kesho asubuhi Naibu Waziri Mkuu wa China na ujumbe wake watatembelea kanisa la Anglican Mkunazini na baadae kuelekea Beit el Ajaib na Jumba la Wananachi Forodhani na kuelekea  Uwanja wa ndege kwa kurejea Dar es Slaam.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
6/9/2012



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...