Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, aliwasili London, Uingereza juzi usiku (Jumanne, 11 Septemba 2012) kwa ziara ya siku nne akitokea Marekani alikokwenda kuhudhuria Mkutano wa Democratic Party, kwa mwaliko rasmi wa chama hicho. Maalim Seif jana (Jumatano,  12 Septemba 2012) alitembelea Ubalozi wa Tanzania uliopo  hapa London na kuzungumza  na Maafisa wa Ubalozi  huo na baadae kula nao chakula cha mchana. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar leo asubuhi amekutana na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Uingereza, Mheshimiwa Mark Simmonds na mchana huu anakutana na mabalozi  wa nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki waliopo hapa London. Kesho Mheshimiwa Maalim Seif anatarajiwa kukutana na Watanzania wote walioko London katika sehemu itakayotangazwa hapo baadae, kabla ya kuanza safari ya kurejea Tanzania Jumamosi asubuhi.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, akiweka saini kwenye Kitabu cha Wageni kwenye Ofisi wa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi hizo za Ubalozi. Pichani: Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, akishuhudia uwekaji wa saini, mara baada ya kumkaribisha Ofisini hapo.



Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, akitoa taarifa mbalimbali za utendaji wa Kituo, kabla ya kumkaribisha, Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar, Meshimiwa, Maalim Seif Sharif Hamad kuzungumza na Maofisa wa Ubalozi



Makamu wa Kwanza wa Rais, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa. Peter Kallaghe,  wakiwa kwenye Picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi, Wajumbe na Wawakilishi kutoka Serikali ya Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kukutana na watanzania siku ya ijumaa, sasa sie tulioko makazini siku ya ijumaa inakuaje. kwa nini asikutane na watanzania siku ya jumamosi...

    ReplyDelete
  2. mbona hizi picha hazifunguki?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...