Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa majadiliano ya kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuwasaidia na kuwahamasisha wanafunzi kushirikia katika masomo ya Sayansi, Tekinolojia, Uhandisi na Hesabu Mkutano huo ambapo uliandaliwa na Bi Savannah Maziya Mkurugenzi Mtendaji wa Bunengi Gropu kwa kushirikiana na Makampuni mengine na kupewa jina la la African First Ladies Roundtable, Umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Suisse America , jijini New York na kuhudhuriwa na baadhi ya wake wa marais, wakurugenzi wa makampuni mbalimbali, wanadiplomasia na wahadhiri.
Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Bibi Katalin Bogyay Balozi wa Hungary UNESCO na amebobea katika diplomasia ya utamaduni na mtetezi mkubwa wa masuala yahusuyo fursa sawa ya elimu kwa mtoto wa kike. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...